Singida: Rais Magufuli awasihi Watanzania kuchapa kazi. Corona haikuanzia Afrika na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo

Singida: Rais Magufuli awasihi Watanzania kuchapa kazi. Corona haikuanzia Afrika na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo

Kahutubia Singida muda si mrefu atakuwa Manyoni then Dodoma. Kaifuata Corona halafu anaiponda. Hii Corona ukiiponda ndo inakuja kukuonyesha yenyewe ni nani.
Miezi kadhaa iliyopita alikuwa anakukosha sana ila saivi.... Duh! Humuelewi kabisa yaani
 
JPM baada ya likizo ndefu amerudi kuendela kulisukuma gurudumu la maendeleo ya Watanzania. Wenye wivu wajinyonge.
 
JPM baada ya likizo ndefu amerudi kuendela kulisukuma gurudumu la maendeleo ya Watanzania. Wenye wivu wajinyonge.
Mkuu siku hizi unabadilika kutokana na upepo unavyovuma..mwanzo ulisema anasukuma kurudumu la maendeleo akiwa ikulu Chato na wala hakua likizo.
Leo tena unasema baada ya likizo ndefu ameamua kurudi kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo.

Kesho akigeuza kurudi Chato kumwona mama then utasema amerudi tena kuendelea na majukumu.
Ukishindwa kusimamia jambo unakua kama hayawani flani hivi. Wajenzi wa uchumi wa kati.
 
Amewaponngeza Watu wa Singida na kufurahi mnama mkoa huo unavyopendeza. Amesema amefurahi kuona Watanzania wakiwa wandelea kuomba kuhusu #COVID19

Rais #Magufuli:

Janga la #COVID19 limepungua sana pamoja na kuwa bado hailijaisha

Ndugu zangu tuendelee kuchukua hatua. Katika mkoa wa Singida kwenye vituo vyetu wamebaki wagonjwa 3 na wanaendela vizuri. Ni taarifa nzuri tuendelee kuomba na kuchukua tahadhari

Tusiongope tusitishane, na uzuri Singida hamjaogopa na hata waliovaa barakoa ni wachache, hata mimi sikuvaa hata RC kwa kuwa Mungu yupo pamoja nasi. Endeleeni kuchukua tahadhari. Ugonjwa huu ukijifungia uwezo wa mwili kupambana na magonjwa unapotea

Sikutaka kuwafungia watu nyumbani kwa maana wanaolima mpunga wangelima nini? Wanaouza mtumba wangeuza nini? Sikufunga mtu ndani kwa Kisukuma wanasema 'lockdown' endeleeni kuchapa kazi.

Taa hizi (za barabarani) zimefungwa wakati wa COVID19. Tuchape kazi. Uchumi wetu ni muhimu kuliko kitu chochote

Kenyatta alinipigia simu nikiwa Chato. Leo pia kanipigia tumezungumza pia. Tumezungumza kama migogoro kule mipakani. Kenya ni marafiki zetu. Tumekubaliana mawaziri wetu wa uchukuzi na wakuu wa Mikoa watakutana mpakani na Kenya wazungumze hili walimalize.

Hii korona isiwe chanzo cha migogoro. Haiwezekani kila dereva anayekwenda huko awe na korona. Nawaomba viongozi wa mikoa inayopakana na Kenya wasitatue matatizo yao kwa jazba. Wazingatie uchumi wa nchi zetu.

Ninafahamu mtu ukichokozwa kidogo ukanyamaza, na wewe unachokoza kidogo. Nataka Wakenya na Watanzania wafanye biashara vizuri”

Naomba, na kwakuwa tumezungumza vizuri na Mheshimiwa Kenyatta, sisi tumeyamaliza.

Haiwezekani mtu anasafiri anaenda nchi jirani anaambiwa akae mpaka sijui siku ngapi wakati amepakia bidhaa

Korona haikuwanzia Afrika. Na imewakoromea wote hata wale wenye uwezo.

Huu ni wakati wa kujenga uchumi. Tunataka Kenya waje wachukuwe maziwa hapa. Tunataka vitunguu vya Singida viuzwe mpaka Kenya.

Tunataka Kenya mafuta ya alizeti yafike mpaka Kenya. Huo ndiyo uchumi wakweli

Ndugu zangu Madereva endeleeni kutulia kwani hili litatatuliwa na serikali zote mbili

Maendeleo ya Singida ni tofauti sana na nyuma.

Endeleeni kushikamana, Musibaguane kwa sababu ya vyama, musibaguane kwa sababu ya dini, musibaguane kwa sababu ya rangi. Sisi wote ni Watanzania na lengo letu kubwa ni kujenga uchumi wa nchinyetu.

Kumbe Makonda akisema anasikika.
 
kwenye janga la corona unaposema uchumi ni muhimu kuliko kitu kingine una maana uchumi ni bora kuliko UHAI. daah kama ni rais tunaye
 
Mkuu siku hizi unabadilika kutokana na upepo unavyovuma..mwanzo ulisema anasukuma kurudumu la maendeleo akiwa ikulu Chato na wala hakua likizo.
Leo tena unasema baada ya likizo ndefu ameamua kurudi kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo.

Kesho akigeuza kurudi Chato kumwona mama then utasema amerudi tena kuendelea na majukumu.
Ukishindwa kusimamia jambo unakua kama hayawani flani hivi. Wajenzi wa uchumi wa kati.
Kama umechukia jinyonge.
 
kwenye janga la corona unaposema uchumi ni muhimu kuliko kitu kingine una maana uchumi ni bora kuliko UHAI. daah kama ni rais tunaye

Nchi tajiri wameshindwa kutokana na ulaghai wao itakuwa Tanzania? Tena wao wanauwezo wa kuchapish noti tu bila exchange rate yao kutetereka unaishi dunia ipi?
 
Back
Top Bottom