Uchafuzi wa mchakato mzima wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 kumeleta kitu kinchoitwa aibu kubwa kwa taifa
Chama dola kongwe pamoja na umri wake mkubwa kilijigamba kuwa makada wake wasimamizi wakuu wakurugenzi maDED na wasimamizi wasaidizi wamekula kiapo cha kutenda haki, lakini kama kesi ya wananchi watatu mwanaharakati Dr. Annanilea Nkya, Buberwa Kaiza mwandishi nguli mkongwe na Bob Chacha Wangwe walivyosema katika kesi kwa niaba yetu raia wote wa Tanzania kuwa serikali ya CCM ina maslahi mgongano.
Pia kuwa TAMISEMI haina utashi, uwezo na nia ya kutenda haki, Bunge la chama kimoja CCM kujiburuza kutunga sheria INEC isimamie uchaguzi wa 2024, na Mahakama ikapinga hoja za raia 3 ikitaka ushahidi kwa kusema tusubiri tuone kwa kuwa imefungwa mikono na sheria za bunge la CCM , lakini Mungu si Athumani mambo hadharani mkwe wa mheshimiwa rais wa Tanzania aliye pia mwenyekiti wa CCM chama dola na TAMISEMI wamevurunda mapema kweupe