Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema hali ya upatikanaji wa maji katika kijiji hicho ni shida na wanalazimika kuamka saa tisa usiku ili kutafuta huduma ya maji.
Wamesema wanapoenda katika Kituo cha Afya hususani Wanawake wanaotaka kujifungua wanalazima kuchota maji dumu sita hadi 12 ili waweze kupatiwa huduma kwenye vituo vya afya.
Akizungumzia changamoto hiyo, Diwani wa Kata ya Mwangeza, Samwel Charles Bosco amesema Wananchi hao sasa wana rangi mbili yeupe na yeusi, hiyo yote ni kutokana na uhaba wa maji unaowakabili katika eneo hilo.
Aidha, Muuguzi wa Zahanati hiyo, Madili Adhyambo ameiomba serikali kuwaangalia kwa jicho la karibu kwani bila maji ya uhakika kituoni hapo inawafanya kutokutoa huduma katika mazingira salama.
Ufafanuzi wa Mamlaka, soma hapa ~ Singida: Serikali yakiri Kijiji cha Dominiki kina changamoto ya maji, yaelezea mipango