Single Moms njooni tuelimishane kitu hapa

😍 Hakika tuheshimiwe 🙏🙏🙏
 
Pole Kipenz na pole kwa Single Moms wote😊its not easy at all na hongera sana najua ww ni fighter am so proud of you🎀💪
 
Sheemeji leo umeniuzunisha sana 🤨🤨 Zulu man naomba uzibe pengo vyema mama wa watu bado moyo unavuja dam



Sema kuna wanaume jau sana na majeuri ole wake mwanaume wa hivi aje kwa dada yangu mwangu naua
Usitoe hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu. Baharia naye angepata nafasi akaja kusimulia hapa ukasikia kilichomkimbiza pengine ungekuta ana sababu zenye mashiko.

Huwa siamini kama kuna mwanaume ambaye yuko vizuri kiuchumi anayeweza kukimbia jukumu lake muhimu na takatifu la kulea kiumbe kisicho na hatia alichoshiriki kukileta hapa duniani.

Kwa wanawake kuzalishwa na kuachwa huwa halinishangazi sana maana watu wakubwa mkishindwa kuelewana njia nzuri na bora ni kuachana kwa amani. Japo always wao ndiyo victims tu walioonewa na kuachwa bila sababu lakini ukichunguza vizuri utakuta waachaji nao wana sababu zao....

Tatizo sasa hawa dada zetu hawa. Leo anamsema vibaya mzazi mwenzie na kesho na kesho kutwa unakuta tena huyo huyo anakwenda kupasha naye kiporo. Hata wakiolewa chanzo kikuu cha ndoa zao kuyumba ni hawa hawa mabaharia waliozaa nao kabla. Huwa hawawezi kumalizana nao moja kwa moja kwa kisingizio cha mzazi mwenzangu!

Ila mleta mada nimemwelewa mno - kama kweli ana msimamo huo. Na ameongea mambo mazito sana. Yote kwa yote kongole kwenu singo mazazi kwa kutokutoa mimba za hao viumbe wasio na hatia. Mungu Atawalipia kupitia watoto hao na vizazi vyao! 🙏🏿
 
Amina
 
Bora wewe mwenye akili timamu wengi wao ni hovyo sana,mtu alishakudhalilisha,akamkana mtoto,ukadharaulika,mwisho wa siku anaomba penzi anamkubalia,anabeba na mimba nyingine halafu jamaa linaingia mitini tena...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…