Mayu
JF-Expert Member
- May 11, 2010
- 8,686
- 14,373
Ofkoz tambara ni zuri sana kwa wanaopenda muvi zenye hisia za kusikitishaView attachment 3367723
Huhitaji utajiri Wa pesa kuelewa maisha ya mwingine Bali upendo ndio daraja pekee la kuokoa maisha ya mwezako anayepitia nyakati Ngumu.
Nimetazama filamu ya Straw kutoka Tyler Perry nimeona picha ya ndani wanayopitia single mothers tuache kuwakebehi kwa lolote hasa pale ambapo huwezi kumpa msaada.
Nimejifunza, msongo Wa mawazo uliopitiliza ni hatari. Mwana mama mtoto wake Aria alishakwisha fariki lakini aliishi Kwenye ndoto za mchana Hali iliyomfanya kuchanganyikiwa. Hapa Cha kujifunza ni lazima mtu ujifunze kukubaliana na nyakati Ngumu ili kuepuka kuingia katika msongo Wa mawazo ambao ni hatari kuliko Hali yenyewe na mnaona kabisa fujo alizofanya mwishowe akiwa tayari amechanganyikiwa.
Pili, Kila jamnii watu wema wapo, mpelelezi Nicole na Meneja wameonyesha picha hii. So, ukiwa katika Hali Ngumu usidhani binadamu wote wabaya amini kwamba Kuna ambaye atakusikiliza na kukuelewa.
Niwaambie kuwa zawadi pekee unayoweza kumpa mtu mwenye maumivu ni kumsikiliza.
Tatu, tusiwadharau single mothers kwa malezi ya watoto wako aisee wanapitia magumu lakini wanajitahidi sana kuonyesha na kutoa upendo kwa watoto wao. Kama mwanaume unaweza kumsaidia bila kuhitaji chochote basi fanya hivyo.
Lakini mwanaume kama umemwacha mtoto na Bado upo hai hapa Dunia huku mama akiteseka aisee!! Rudi ukatubu na uwe Kwenye maisha ya mtoto wako.
Hapana Tanzania naona utani na dharau nyingi sana kwa single mothers kupitia mtandaoni. Wengine wakiwakashifu na hata kutoa Elimu ya kwamba hawafai kuoa na usijaribu.
Acheni jamani narudia acheni na kama huwezi kumpa upendo Wa dhati usimtukane Wala usimdharau kwani wanayopitia ni mateso tosha kiakili na kimwili.
Nahisi tatizo alilopitia Janiya na kazi alionyeesha Tyler Perry ikawa sehemu ndogo sana ya matatizo wanayopitia single mothers Kwenye jamnii zetu hasa Tanzania ambao uhuru Wa kuongea bila kujali maneno kama silaha hatari umepitiliza Wa kuendelea kuwaumiza wanawake.
Mwisho, single mothers wanahitaji upendo, kusikilizwa na kuheshimiwa ili waweze kukuza kizazi Bora na pia kuwa salama kiakili kwa ajili ya maisha Yao.
Pia, Serikali iongeze sheria Kali Kali katika malezi ya watoto kunusuru jamii ili wanaume wanaokimbia watoto wawajibishwe vikali.
Taraji P kauvaa haswa uhusika pamoja na meneja wa Bank Sherri na Tayana Taylor aliye cheza kama Detective Raymond
Ila naona kama u “single mother” unakuzwa sana kwenye hili tambara
Kwangu mimi sioni tatizo kubwa kama ni usingle mother kwasababu wapo masingle mother kibao wana maisha ya chini na watoto kibao lakini wanaishi fresh tu kiubishi ubishi
Tatizo kuu la Janiyah ni kuwa na mtoto mgonjwa ambaye ana changamoto kubwa kumtunza na dawa na matibabu yake ni gharama kubwa mmno kwa mtu wa kipato cha chini kumudu
Nilipokua naangalia movie hii ikanikumbusha movie ya John Q ya Denzel Washington jinsi alivyo lianzisha kuhangaika na mwanae ambaye alikua na ugonjwa wa moyo unaotakiwa kubadilishwa na yeye uwezo hana
Na pia kama umeipenda sana Straw basi angalia na tambara moja linaitwa Breaking kacheza John Boyega
Mshkaji ni mwanajeshi mstaafu mwenye madhara kibao ya vita ambayo yanamfanya anashindwa kumudu kufanya kazi, kipato pekee ni pensheni yake kama muathirika wa vita
Shida ilikuja pale pensheni hiyo ilipo kuja kusimamishwa kiaina na jamaa akawa homeless, ikabidi avamie bank anakochulia malipo yake na kudemand serikali imrudishie malipo yake
Senario ni kama ya Janayah kwenye bank
Inasikitisha sana