Single mothers na vilio vya kushangaza

Single mothers na vilio vya kushangaza

Naona kubishana na wewe ntapoteza muda
kumbe nikianzisha thread lazima niwe nahusika binafsi?
akili ndogo hizo

humu naanzisha thread kutetea waandishi wa habari..kwani mimi mwandishi habari?

Wewe wanawake walio support umewasoma na kuwaelewa?
Uko sahihi The Boss. Ulichoongelea ni wale walalamishi ambao walizaa makusudi na baadae kulalamikia wanaume. Huenda huyu mama ni mmoja wapo.
 
Wanawake wenzangu jamani tuwe makini na hawa viumbe, its about time sisi ndio tuishi nao kwa akili maana hali sio hali tena. Mwanaume sio ndugu yako,just through hizi threds unapata picha ya ni aina gani ya wanaume tunaodeal nao so akili kumkichwa, zaa kwakuwa umeamua na una uwezo wa kumlea huyo mtoto, huyo sperm donor mpotezee tu, akiona bora amlee mwanae its okey.

Ila kabla ya kuchukua maamuzi hayo pia basi utafakari pia kuhusu huyo mtoto atakaezaliwa ni aina gani ya maisha unataka aishi,ist worth it?
Hahaha
 
Tuseme tu ukweli kuna wadada wengi au wamama siku hizi wanaamua kuzaa tu....hasa umri fulani ukifika na wengine wanaamua kuzaa kabla hata wa kuzaa nae hajatokea...

Sasa kimbembe kinaanza anaposhika mimba....au akishazaa na mtu ambae si ajabu hakuwa na mipango ya kuzaa na huyo mwanamke

Wadada wengine wanaamua kutumia mimba kulazimisha commitment au ndoa......Asipopata hiyo ndoa au hiyo commitment ni kumlaani huyo mwanaume na kutumia mimba au mtoto kama njia ya kumkomesha huyo mwanaume..

Siku hizi unakuta vilio vya wadada kuwa 'wanaume hivi na wanaume vile'
lakini ukweli sio wote walidanganywa wataolewa au waliahidiwa commitment

Wengine kupata mimba na kuzaa ilikuwa ni mipango yao binafsi..lakini wakishazaa wanaanza kubadili maneno...utasema waliahidiwa kweli kuolewa
au waliahidiwa matunzo ya mtoto in the first place kabla hawajashika mimba...

Ni busara kwa kila mwanaume kushiriki matunzo ya mimba inayomhusu
na matunzo ya mtoto wake......lakini wote tunajua busara sio kila mtu anayo
na wadada wanaojichukulia maamuzi binafsi ya kuzaa ni busara pia wakaacha kulialia.....kama vile maamuzi hayo yalikuwa ya watu wawili
na wengine husingizia kwa ndugu kuwa waliahidiwa ndoa...kumbe ni maamuzi yake binafsi kuzaa.......dunia imebadilika.... tupunguze lawama tukabili changamoto za maamuzi yetu...
Naam
 
Hakuna mtu aliyechagua kuwa single mom, it just happens na hakuna jinsi. Hawa single moms mimi nawaheshimu sana, they're stronger than us all, they are fighers, breadwinners kwa watoto wao, mara nyingi wanakuwa bullied lkn still they keep going.

You need an iron chest kuwa single mama. Ni watu kamwe siwezi kuwasimanga.

Hats off to all single mama who are disrupting status quo. Salute!
Mmmh
 
Yani sababu zote zilizotajwa hapo za mimi kuwa single mom hazipo. Second embu niache nipumue basi. Naona hasira za kusumbuliwa na baby mama wako unataka kunimalizia mimi. Mtafute mmalizane usinitolee mimi machungu yako sawa kaka cjui baba?
🤣🤣🤣
 
Thanks nishapoa kabisa kitambo, nina A very responsible husband na wanetu wawili, ila likija suala la hizi discussion za usingle mom, ntapiga kelele mpaka watu wadhani mimi ni victim, yes mi ni victim kwa sababu mi ni products ya single mama, kwa maana babaetu alitutelekeza kwa mama since tukiwa wadogo (mi na kaka yangu). Sitaki sana kujua sababu ya sisi kutelekezwa pengine ndio gubu za wanawake lakini itoshe tu kusema hatukudeserve kuishi tulivyoishi ikiwa babaetu mzima wa afya na anauwezo wakutosha tu kutulea.

Speaking of single mothers nikivaa viatu vyao huwa vinanibana kabisa, hawa watu wanahustle, wana suffer ili tu watoto wao wasurvive, hawa ni wale wenye vipato hata kama ni vidogo kama alivyokuwa mamangu, sometimes wanafanya dirt games for wellbeing ya familia, nakumbuka kuna kipindi nilikuwa nikifukuzwa ada nikirudi nyumbani mama hadi pressure itampanda, lakini atafanya chochote apate ada mwanae nirudi shule, ikafika kipindi nilivyokuwa mdada nikifukuzwa ada hata nyumbani sirudi, ntaitafuta hadi niipate (hapa baba yupo na ukipiga simu anakujibu mwambie mamaako anipigie we unanipigia kama nani)

Kuna time nikiwa 1st year kaka yuko 4th year mama akinitumia hela mi namtumia kaka namwambia we tumia mi ntapata zingine hii yote ni kuepusha usumbufu kwa bimkubwa, yaani nikiwaza mama alivyokuwa akivuja jasho kututunza napata hasira kuana single mothers wanakuwa mocked na kutukanwa kila siku kwenye jamii, naumia naumia naumia. Mngejua nyie wanaume jinsi hawa wadada/ wamama wanavyoishi ndani mwao wakitoka nje wameoga wamependeza kuficha dhiki zao msingesema chochote juu yao.

Single mamas wanatakiwa kuthaminiwa, kutiwa moyo na kusaidiwa ili kuheal vidonda vyao na kufuta machozi sio mnavyowafanyia. Ni vile tu hamuwezi kuelewa mpaka mtakapoelewa !
Mmh pole sana
 
Back
Top Bottom