Nina jamaa yangu tunafanya nae shughuli pamoja na rafiki wa karibu, mwaka juzi alikutana na binti mmoja wakawa wameingia kwenye uhusiano na binti akamwambia yeye ni single mother alipata mtoto alipokuwa chuo na walishaachana na baba wa mtoto hata mawasiliano hawana kabisa, jamaa akawa anahudumia binti na mtoto (alimpeleka mtoto shule ya kulipia).
Mwaka huu kijana akaenda kwao binti kujitambulisha na akatutuma (mimi na babaake mdogo) tukaenda kwao kupanga mahari na tarehe ya harusi na ilikuwa mahari itolewe mwishoni mwa mwezi huu na harusi mwezi wa 10.
Juzi jamaa alimpigia simu mke mtarajiwa akawa hapokei akaamua kwenda kwao binti kujua kimemsibu nini?
Kwao wakasema hawajui ameenda wapi ameondoka na begi na mtoto, jioni kabisa binti akamtumia meseji jamaa kuwa asimtafute ameamua kwenda kwa mzazi mwenzie hataki watoto wake wawe na baba tofauti.
Kwa kweli jamaa amechanganyikiwa hata kazini haendi tena anashinda ndani anakunywa pombe, single mother sio wa kuwaamini kabisa.