Single mothers njooni tuzungumze kwa mapana na ufupi

Single mothers njooni tuzungumze kwa mapana na ufupi

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,095
Reaction score
22,731
Habarini wanajamvi.

Imeshakuwa ni wimbo wa taifa kuwatuhumu single mothers kwa uzembe na kuwa number one suspects katika kushiriki kuibomoa taasisi nyeti sana ya familia.

Upo ukweli katika hili wapo wengi wao sana walijiingiza katika mahusiano kwa tamaa aidha kwa kujihusisha na wanaume wenye ndoa zao na wakijua ukweli wote, kutoka kimahusiano na wanaume ambao hawana haiba ya kuwa mume wa mtu na bado wanauvulana mwingi kichwani na hatimaye kushindwana nao, walijishikisha ujauzito kwa makusudi ili kuwakamata wanaume ambao mwisho wa siku wakashindwana na kujikuta wakilea watoto wao wenyewe, lakini kubwa kabisa ni asilimia kubwa ya mabinti kuwa na mienendo na tabia ambazo hazisadifu au kuakisi sura ya mke wa mtu na hivyo kujikuta wakiachwa kwenye mataa bila ndoa wala mahusiano ya kueleweka na hatimaye kukata tamaa na kuamua kuwa bila mwanaume.

Hizi pamoja na sababu nyingine nyingi zilizozoeleka ndizo zinapelekea wanawake wa sampuli hii kuonekana ni kitu cha ajabu na fedheha katika jamii.

Lakini basi, tusisahau pia kuwa wapo ambao kuwa single mothers ilikuwa sio by choice wala tabia mbaya, bali ni kupitia mikono mibaya tu ya wanaume waongo na walaghai na hatimaye kuwa victims wa kulea watoto bila msaada wa kiumeni. Hawa ni wachache sana ila wapo katika jahazi hilo hilo la single mothers linalopigwa na dhoruba ya lawama na kejeli kila uchao.

Ni vema tukajua kuwa aina hii ya wanajamii ni wenzetu, wanaweza kuwa ni dada au wadogo zetu wa tumbo moja, rafiki, school/classmates, X's wetu, wanawake ambao tuliwatamani ila walitupuuza na sasa wamenasia hapo.

Na kama wanajamii na tumeiona hii hali basi tujue tukipuuza inayoathirika ni jamii yetu. Tuna wajibu wakuwapa sapoti na kuwapa tena nafasi ya pili ya uyajenga mahusiano upya na watu wapya au wale ambao walishindwana kwa kupishana vitu vidogo sana.

Huku katika jamii wapo wanaume ambao wapo tayari sana kujitoa kuanza maisha na kuishi na hawa single mothers na kurejesha heshima yao ya kuwa mwanamke na pia mama wa familia ili tujenge taifa lenye msingi mzuri wa familia.

Lakini changamoto huja kutokana na sababu nyingi baadhi zikiwamo mtazamo wa jamii juu ya maamuzi ya kijana kuanza maisha na mwanamke ambaye tayari ana mtoto, lakini mbaya zaidi ni wanawake wenyewe wenye watoto kutokuwa na utayari wa kuanza upya na kuheshimu mahusiano na mtu mpya aidha kwa kujistukia na kutojikubali, kujihami, na mbaya zaidi kuwa negative juu ya mwanaume anayekuja kuanza nae sababu anajua haiwezekani kutokea hali kama hiyo.

Leo napenda niwape hints ama dokezo chache za namna ambavyo hili janga la single mothers linaweza kupunguzwa kutokomezwa kama jamii tutashikamana pamoja kulitatua.

Na pia napenda nitoe angalizo kuwa kwa ninyi wasichana ambao bado hamjaingia katika hali hii mchunge sana matendo na mienendo yetu na muhakikishe mnaanza mahusiano na watu wa kueleweka na sio kubahatisha mwishowe mje kuongezea namba mkitarajia wapo watu wakuwachukua na hizo hali zenu za kuwa na watoto, acheni huo upuuzi na muwe serious na maisha yenu. Ni vema kujua kuwa jamii yetu inamtazamo hasi juu ya mwanamke ambaye ana mtoto na yupo single. Hivyo ukisha jua hili itakufanya kuelewa upo katika jamii ya aina gani na kuweza kuchukua hatua kubadili hiyo hali na si kujifanya kichwa ngumu na kukomaa na hiyo hali ukidhania ni ushujaa kumbuka tupo tanzania sio marekani hapa.

Haya ni mambo ambayo nitayagusia leo katika kuwashauri wanawake wenye watoto kuweza kuingia katika mahusiano mapya na kulisongesha gurudumu la familia bora.

1. Tambua unapokutana na mwanaume mpya ambaye ameonyesha interest ya kuwa na wewe na ametambua uwepo wa mtoto wako na akakukubali ulivyo, amefanya hivyo kwa moyo wa huruma. Itakuwa ni ujinga wa karne ukaanza kufanya jitihada za kumlazimisha ampende mtoto kwanza ndipo awe na wewe. Kumbuka alikuja kukufuata wewe na sio mtoto angekuwa na shida ya mtoto wako angekuja kuomba adoption na sio uhusiano na wewe.

2. Hakikisha unamalizana na mzazi mwenzako kabla ya kuingia uhusiano na watu wapya. Pale unapoona mambo hayaendi kati yako na baba wa mtoto, basi keti chini na kujadili juu ya hatima ya mtoto kisha mkubaliane kuwa mtoto ataishi na nani maisha yake yote na kama ni kwa muda atakaa na wewe atakaa muda gani kisha baba yake aje mchukua.

Usijenge mazingira ya ukaribu tena na mtu ambaye umekiri mlishindwana au mguu nje mguu ndani maana utaendelea kuchezewa akili na huyo baba wa mtoto kwa kigezo cha mtoto na hatimaye atakuzibia fursa ya kuwa na mtu mpya.

Na hata pale ukiwa na mtu mpya akabaini kuwa unamazoea na baba wa mtoto wako ni rahisi kwake kukudharau na kuanza kukusaliti ama kuvunja uhusiano maana atakuwa ameshahisi mapenzi yamepungua kati yenu na bado unakitu na baba wa mtoto.

3. Kumbuka wewe kupata mtoto na kutengana na uliyekuwa nae si ulemavu wa mwili na haikushushii utu wako. Kama unahisi wewe unadosari mbona mwanaume yule hajisikii hivyo na wote mtoto ni wenu.

Bado unahaki na uhuru wa kuingia katika mahusiano mapya na kuweza kuwa na furaha na kupata familia mpya. Hivyo basi acha kujiona dhaifu na unadosari kiasi kwamba mwanaume anapokufuata unakuwa unamkatisha tamaa kwa kujihisi kuwa anataka kukuchezea na kukutupa.

Kuna wanaume waoga sana kumpa mwanamke ujauzito na kuanza naye familia ila akikutana na wewe atajifunza na uoga wa familia utamtoka na hatimaye mtaweza kuanzisha familia na kuunganisha watoto ama kulea watoto wapya na huyu mwanaume wakati yule wa kwanza akienda kwa baba yake au kuishi na wazazi wako.

4. Kumbuka kuwa na mtoto sio kosa bali kosa ni wewe kucheza na maisha yako na kuharibu utu wako na nafasi ya kuitwa mama wa familia na mke wa mtu, hivyo kulirekebisha hili si kwa kujikubali kuwa single mother, la hasha, huo ni ujinga wa akili na utomvu wa nidhamu kwa hadhi ya mwanamke.

Hivyo basi endelea kupambania hadhi yako kwa kurejea wapi ulijikwa, kama ni tabia zako zilikukosesha mahusiano bora basi uzirekebishe na kama ulikutana na mtu siyo basi safari hii kuwa makini sana kujua ni mtu gani anastahili kuendelea na wewe, washirikishe wanawake watu wazima ambao wapo katika ndoa imara sio mashangingi wa mjini ambao wanajiita maboss lady hawa watakupoteza na fikra zao hasi juu ya mahusiano.

5. Penda kusoma vitabu vya kujenga, badala ya kugoogle namna ya kumkomoa mwanaume uliyezaa nae, basi kugoogle how to a woman with a child can start a new happy relationship and family with a new man. Wanawake wa sampuli ya single mothers wengi kutokana na maumivu ya kutendwa au majuto ya kukosea kutokana na uzembe wao, ubakia na ukoko wa fikra hasi vichwani mwao na hii huwafanya kuwa negative, wabishi, uelewa mdogo wa mambo ya msingi na mbaya zaidi hupenda kujiridhisha kwa kusikiliza na kusoma mawazo au maandiko ya watu wanaowajaza ujinga wa kutokuamini kuwa kuna bright future ya wao kuanza upya. Hii huwafanya kuwa hasi na kushindwa kujipanga upya kwa maana huwa na muonekano wa kufeli zaidi badala ya muonekano wa kujaribu upya na kujikuta wakipata vichaa vya mchana kweupe ili hali hawaokoti makopo.

Futa kabisa tabia ya kuhisi wewe ni victim wa kuachwa na kuona wanaume wabaya, kumbuka huyo aliyekutenda ulimpa nafasi wewe mimi sikuwapo na wala sikumwambia akukomoe au akuache au kukushauri wewe kufanya uzembe uliopelekea yeye akutelekeze na kushindwana na wewe. Hivyo basi nikikufuata kukutaka, jaribu kuwa mstaarabu na kutonijaribu au kufanya mambo ya kitoto kuwa mtu mzima na uonyeshe utashi wa kustaarabika, kiburi na jeuri havikuwahi kumsaidia farao wewe ni nani vikusaidie?!


6. Achana na makundi ya wasichana wenye mambo ya kitoto au wanawake wakubwa wenye mambo ya kisichana. Mifano ya hawa wanawake wa kuavoid ni akina wolper, wema sepetu, diva wa clouds na wengineo wenye kariba hii. Ukiona mwanamke ambaye hadi anafika miaka 27 bado kauli zake ni negative juu ya mahusiano, usitegemee atakushauri vema juu ya mahusiano, atakupoteza. Kumbuka wewe ni mama yake mtu sasa na aunatakiwa kulinda hiyo heshima kwa kumtafutia mtoto familia ya kueleweka na baba mlezi mpya ama yule wa awali kama mtamaliza tofauti zenu na kuanza maisha vizuri.

Heshima ya mwanamke ipo katika kuwa na familia yake, hakuna mtu asiyejua hilo. Kukaa na company ya wasichana au wanawake wenye mambo ya kitoto sio tu kutakufanya ufananie nao kitabia na kimwenendo bali kutakufanya kupoteza muda wako ukifanya ujinga na kuzungumza ujinga na pengine wakakurejesha kule kule kwa kukushawishi utoke na mwanaume mwingine wa sampuli ya kwanza akakupoteza tena. Jenga mahusiano na wanawake wa rika lako ambao wapo katika mahusiano yanayoeleweka na yenye afya, pia watu wazima ambao wanafamilia zao watakushauli kama walezi na kukusaidia kufikiria upya kuhusu swala la kuwa na familia yako.

7. Kana kiburi cha tabia. Wanawake ambao wanawatoto hujenga haiba ya kiburi kama self defense inayotokana na kuwa na lower self-esteem na stigma ndani yao kwakuwa hujiona hawana hadhi tena na kupelekea kukosea zaidi. Si hapa leo ukamkuta msichana mwenye mtoto na ukamtaka kuwa nae na yeye kwa kujihami akaanza kukupa majibu ya nyodo as if hana shida ya mwanaume kwa kusema "nyie wanaume sina hamu nanyi wote wale wale", " si babaishwi na mwanaume maisha ni mimi na mwanangu".

Hizi kauli si tu zinakera bali zinakatisha tamaa na kufukuzisha nia nzuri yoyote ambayo mwanaume anaweza kuwa nayo katika maisha ya mwanamke huyu. Ni vema kujijenga na kubadili tabia ya kujikubali kulikopitiliza. Wewe ni mkosaji kama wengine na umeshapotea, kujikubali ni swala moja ila hatua gani inafuata baada ya kujikubali hapo ndipo muhimu. Ni vema ukajijenga kuwa na heshima, mnyenyekevu na rafiki mwenye lugha ya adabu, ili basi huyu mwanaume atakayekubali kuwa na wewe apate nafasi ya kujadili na wewe muafaka wa maisha yenu na kuanza upya.

8. Tumia muda wako mwingi kuwekeza katika uhusiano wako huu mpya na usiwe mtu wa kujifanyia mambo yako ili hali upo na mtu ambaye ameamua kuanza maisha na wewe. Kumbuka mtoto hatobakia na wewe maisha yote. Atasoma na atapofika ngazi ya chuo ataanza maandalizi ya kuanza maisha yake, wewe utatakiwa uwe na maisha yako sasa utaishi vipi pekee yako kama jini, ni vema kuinvest katika uhusiano mpya na kuimarisha misingi ya kuanzisha familia mpya ili uweze kuwa na kwako na kuweza kufurahia maisha upya bila kujiona unadosari. Pia hii itampa nafasi mwanaume uliyenaye kuweza kukusaidia kurudi sawa maana atakuwa ameishi akiwa na imani kutokana na namna unajitoa kwake, weka hofu ya kuachwa tena kando jitoe kadiri ya uwezo wako.

Haya ni machache nimeweza kusema leo, natumai kila m'moja kwa nafasi yake anaweza toa mawazo ya ziada ya kuwasaidia wanawake hawa ambao wanaonekana ni tatizo katika jamii yao .
 
single mother wameshageuzwa FOREx huku MMU
maana kila siku wanatungia thread tyu daaahh
single mother kama nikweli mnahayo madhaifu wanayo yataja wadau basi mtazeeka bila NDOA Aiseeeee

lazima muolewe nakina baba dangote wakati mmeshakuwa maajuza
 
single mother wameshageuzwa FOREx huku MMU
maana kila siku wanatungia thread tyu daaahh
single mother kama nikweli mnahayo madhaifu wanayoyataja wadau basi mtazeeka bila NDOA Aiseeeee

lazima muolewe nakina baba dangote
Tunakutana Sana
 
Ukijitangaza wewe ni single mom halafu ukanikuta pm kwako usinune
 
Ujumbe mzuri Mkuu. Ila mie imenifaa zaidi hiyo namba sita nadhani kipo kitu kikubwa cha kujifunza hapo.

Sababu asilimia kubwa ndio wako hivyo.
 
Back
Top Bottom