Single mothers njooni tuzungumze kwa mapana na ufupi

Single mothers njooni tuzungumze kwa mapana na ufupi

Wanaume pia muache kuwatengeneza hao single moms, utakuta mwanaume kazaa na wanawake watatu tofauti, amewaacha hana mpango nao, lakini anasema hawezi kuoa mwanamke mwenye mtoto. Sasa hao uliozaa nao nani awaoe.....ufala mtupu.
 
Acha tu niwe single mama kuliko kujibana na mtu ana kiba100
Wewe sio mwanamke. Unachukulia utani maswala wanayopitia wanawake wenye watoto sio poa.....
 
Mi nikikutana na singo maza, najua tayari kuna mwanaume mwenzangu kashazingua!
Negative perception......not good at all. Ikiwa ni dada yako wanaume wanamtazama hivyo na alishafanyiwa tukio na kutengwa na jamaa utafurahia watu wakimcheki kwa jicho hilo?!
 
Nimeshindwa kusoma ,ni ndefu mnoo
Elimu haikuwahi kuwa kitu rahisi kwa mtu asiyependa itumikisha akili yake.

Ndio maana tunakizazi cha wasomi ambao wanataka zitto kabwe asome takwimu then azichanganue na kuzijengea hoja kisha aseme wao wameze na kuzerepost hizi hoja mitandaoni na kuishia kuitwa wachochezi.

Kosa ni uvivu wa kuruhusu akili isome.......jirekebishe uokoe kizazi chako.
 
Asante umeeleweka lakini je,single father unawashauri nini na wao?
Katika hili janga la kuvunjika uhusiano ambao wanaonekana kukichezea cha moto ni wanawake.

Ila kwa wanaume naweza kuwashauri wanavyowachezea watoto za watu wakumbuke nao wana dada wanawadogo zao wa kike ama watakuja pata watoto wa kike huko mbeleni wasije lalamika kibao kikigeuka. Na mbaya zaidi kupata mtoto then kutelekeza mtoto na mama yake hiyo ni laana kwa MUNGU na itakurudi kwa namna yoyote
 
Mi nikikutana na singo maza, najua tayari kuna mwanaume mwenzangu kashazingua!
UZI UNAHUSU "SINGLE MAMA'S" WEWE DUME JENZANGU UNAFATA NINI KWENYE HII KITCHEN SINGLE MAMA'S PARTY YAO?!
 
Umeandika ujumbe mzito mnoo!!! Nikushukuru kwa hilo, lipo la kujifunza Mkuu!!!

Hebu agiza soda hapo kwa mangi naja lipa!!!
Ha ha ha ha ha ha shukrani. Nimeshakunywa hapa kwa mangi tabata segerea hapa.
 
Yan niache kuinvest kene mambo ya msing ya kuniingizia pesa n invest kene mahusiano na kiumbe mwanaume mapenz hayana formular na mapenz ya kwel huja automatic,hizi thread zinachoshaaaaaaa mnooo yan!
Kila mtu apambane na hali yake aisee
Rejea kipengele namba sita na namba saba vinakuhusu. Unaonekana unaelewa tatizo lipo wapi ila ni jeuri na viburi ndivyo vinakuponza.

Anyways, bado miaka kadhaa, utatoka kusema mapenzi hayana formula kuja kusema eeeh yebeneza, nipe hata konda wa daladala nitamuheshimu.

Bora upigwe kofi na binadamu mwenzako, ila sio maisha yakupige kofi.
 
Kapambane na hali zenu na za watoto wenu tutoleeni kiwingu hapa.!
 
Back
Top Bottom