Sawa, sikukatalii. Mimi mwenyewe napenda sana uwazi.
Lakini bado hujaelewa point yangu.
Unategemea vipi mabadiliko ya kutoa habari zaidi yaje kwa kumbadilisha waziri wakati tatizo ni kuwa na serikali ambayo kwa makusudi kabisa inafanya usiri?
Huoni kwamba ikiwa ni kweli serikali inataka usiri, hili si tatizo la waziri wa sasa, na hata ukimbadilisha, huyo mwingine mpya itambidi afanye kazi kwa usiri huo huo, na hivyo zoezi lako la kutaka waziri abadilishwe litakuwa halina maana?
Huoni kwamba unajaribu kutibu dalili ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ya kukohoa kwa kumpa mgonjwa dawa ya kupooza kikohozi ya Cofta, wakati hujatibu igonjwa wenyewe wa Kifua Kikuu, na kwa hivyo, dalili ya kikohozi itaendelea tu, kwa sababu ugonjwa wa msingi haujatibiwa?
Wewe unafikiri kweli hawa mawaziri ndio wanaamua watoe habari au wasitoe?