Google mzee au nenda wizara ya mambo ya nje kaulizie ila jua tu alikuwa mmama jina lake sitaji.Mzee baba kama hautajali taja jina la balozi wetu aliyekuwa Rwanda wakati huo serikali ya Rwanda ilipofanya majaribio ya mauaji ya watutsi mwaka 1992 na baadae mauaji rasmi mwaka 1994. Sidhani kama jina la balozi yeyote katika nchi yoyote na kwa mwaka wowote ni siri yoyote kwa mtu yeyote yule. Hivyo sioni sababu kwa nini usitaje jina la huyo mwanadiplomasia wetu kwa wakati huo.
Hii story kama sinema vile kila hatua inaleta hamu ya kujua ya mbeleni.
Kuna CD jina nimesahau inaelezea mauaji ya watutsi daah baba mmoja mhutu akapoteza mke na watoto kisa mke ni mtutsi
Wanafunzi wakachapwa risasi darasa zima kisa watutsi
Baadae nilikuja gundua kuwa alikuwa anaongea na mkuu wa interahamwe ( jina lake nimelisahau jamaa babe liuaji hatari sijui kama bado lipo hai, kama bado yupo hai hajasakwa na kufikishwa ICC basi haina haja ya kuendelea kuwahukumu wengine) ila jamaa hilo ndo lilikuwa kama Li-mkuu la majeshi kigali nzima huyo ndo top akisema ua umekwisha akisema acha umepona, unajua mabalozi lazima wawe na koneksheni kubwa sanaa wakati mwingine kwa upande wa serikali, waasi (kama wapo) na wapinzani. Mtakufa wote lakini balozi atapona, atalindwa atasindikizwa na kuwekwa sehemu salama. Nyinyi mnahenyeka tuu na vipassport vyenu.Labda alikuwa akiongea na mbobezi wa nchi ya Rwanda wa wakati huo yaani waziri wa mambo ya nchi za nje kumlalamikia kile wanachokifanya watu wake kwenye ubalozi wa Tanzania.
HapanaMzee baba kupitia kisa hiki unapata vitisho vyovyote huko PM?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Interesting story. Balozi mwanamke jasiri kweli! Atakuwa TISS au katokea Military Intelligence.
Sent using Jamii Forums mobile app
Inafikirisha sana ndiyo! Kwa maana ya kuitazama siasa yetu lakini ukitembea nje tu nyumba uliopo utagundua lifestyle ya watanzania ni tofauti sana na huko Rwanda, hakuna mtanzania mwenye munkari wa kushikiana mapanga achilia mbali ak47! Hata mambo ya kuchoma moto vibaka yamepungua sana.
Pengine wanasiasa ndo wangechochea vuguvugu za vijana kupigania ukombozi dhidi ya mkoloni mweusi! Wanasiasa hao wako wapi!!? Hao walozeekea kwenye vyeo vyao na sasa wanakwenda kugongeshana miguu na mkulu!? Hakuna anaependa vita ila na sisi tumelala mno.
Sent using Jamii Forums mobile app
Humu kuna wasomali (anaebisha huwa hao wasomali wanaongea hadi hicho kisomali humu) ,kuna Warundi, Wanyarwanda etc mataifa yanayoongea kiswahili wamo humuInawezekana unachosema coz kuna watu hawapendi kusikia ukweli huu kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Watu kama hao wapuuze tu humu tuna watu wenye tabia aina zoteWe umezaliwa mwaka gani? Unajua dola moja ilikuwa sawa na bei gani mwaka 1989.? .hii elimu bure imeleta shida sanaa kwa vijana halafu wapi niliandika nilipigasimu? Hizi akili bwanaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Jifunze kuandika mkuu, mwandiko wako unatia aibu.Of all jf members wewe ndio nimekuspot direct Kama tiss employee directorate ya IT pale eagle wing maana huuu uzi Kuna infiltrators wawili wa kagame walioko umangani wanaufwatilia kila post na katika cloud chek ushawasiliana nao mwakajanadesembanakwenyejambolinalohusuuzihuunawewekwawikitatumweziuliopitaulikuwakigalibishanianike
Naungana na wewe.CCM iko wapi mkuu! Hii ambayo wamo kina Waitara, Mtatiro, Polepole, Kafurira, Mashinji, Dr. Slaa, Kabudi, Mgwira, Masha n.k? CCM ambayo imemtimulia mbali Membe na kumpa onyo Kinana! Tusikalili sana kuhusu neno CCM maana tayari wamechangamana na wapinzani waliopigania mabadiliko kwa kiasi kikubwa hapo awali. Kama hawawezi kuyaleta mabadiliko hayo wakiwa huko chamani, ni dhahiri unafiki wetu watanzania utakuwa ni wa kiwango cha kutisha.
Hivyo vikosi uchwara vya vyama havijaweza kuleta impact ya vita hapa nchini. Huko mitaani watu hata hawajali kabisa wapo kwenye harakati zao. Harakati za mnyukano wa kisiasa nchini hazizidi hata 5%, watu wapo bize na soka, kukanyaga mafuta, ubuyu wa instagram, kusaka noti... Hata CORONA tu hawana habari nayo.
Vita hapa kwetu si kesho wala mwaka kesho! Ni kama haipo forever. Watu wetu wengi, hata akina Seif Sharrif, Zitto, Mbatia wanaamini katika "Mwenye nguvu mpishe" na "Mpiga ngumi ukuta huumia mwenyewe"
Sent using Jamii Forums mobile app
Kama sio mhutu ni Interahamwe huyoWe ndo mpumbavu unashindwa kutofautisha stashahada na shahada halafu unajiona mjanja kumbe empty, ukipigwa ban utakuja na iD nyingine humu kulalamika unaonewa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wahutu mpo wengiBossless,
We Muongo, ulienda mwezi WA sita hahahaha.
Vita imeanza mwezi WA nne imeisha mwezi WA Saba but wewe ulipata KAZI mwezi WA sita wakati serikali ya Rwanda imevurumishwa na Rpf na kukimbilia Gisenyi Kwa kina Haruna Niyonzima huku mapigano makali yakiendelea.
Anyways wakati unapata hiyo KAZI Rais wa Rwanda alikuwa anaitwa Nani?
Jibu huna Mpira uishie hapa.
" falsus in uno falsus in omnibus" false in one thing false in every thing.
@moderators futeni uzushi huu unachafua hadhi ya jf
Mhutu kama sio interahamwe huyoLIKUD,
Mbona inaonekana wewe ndiye una haraka? Wengi tunafahamu kwamba vita imeanza mwezi huo wa nne hadi wa saba tena mwaka 1994.
Yeye ameanza na mwaka aliomaliza masomo ya stashahada mwaka 1989 na kupata kazi kwenye ubalozi huko Rwanda. Bado anaendelea na background hajafikia kipindi vita imeanza.
Inaendelea.....Habari zenu wakubwa kwa wadogo.
Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.
Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.
basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..
Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.
Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.
Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.
Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.
Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .
Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.
Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .
Itaendelea...........
Sent using Jamii Forums mobile app