Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Hapo waweza tazama movie moja inaitwa "Rules of Engagement" kwa kusindikizia hii story...
Naona wazee wa defender walitangulia kufanya yao..
Ya mwaka gani
 
Hapo waweza tazama movie moja inaitwa "Rules of Engagement" kwa kusindikizia hii story...
Naona wazee wa defender walitangulia kufanya yao..
Kuna kitu nilijifunza vitani ,wakati vita inapiganwa si ajabu kuna watu wengine wanapigana hiyo vita hiyo hiyo lakini hawaonekani inakuwa ni siri ya nchi na nchi,yani inakuwa kwa mfano kama ugomvi wa mtaani mnachokozana mkianza kupigana wakati mnandelea kupigana na mchokozi wako jamaa zake au watu wengine kwa maslahi yao binafsi wanakuwa wanakusachi kiaina au wanakuwa wanapenyeza ngumi mbili tatu kwako kumsaidia jamaa yao au kukusaidia wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hi kali
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inatisha sana. Vita ya wenyewe kwa wenyewe sio kitu cha kushabikia kabisa aisee. Hii stori yako, ni kama vile unaangalia movie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daah so sad!!! Hivi mkuu bossless itaendelea kwa leo au mpaka kesho? Manaake Kama vipi ntakaa kuisubiri tu
 
Sio mabasi kulikuwa na maroli tu halafu huyo mnyarwanda ni yupi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Napata wasiwasi kuna baadhi ya mission balozi alikuwa akizichezesha ndio maana kuna vitu umevifungafunga anyway nahisi kuna mkono wa tanzania ulihusika katika kifo cha huyo Rais...

Embu ngoja tuone muendelezo utakuaje...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiangalia mbelgiji ndo chanzo Cha mauaji ya kimbari na vikundi vya waasi kivu ya kaskazin na kusini, sababu zile identity card za kuonyesha huyu mhutu yule mtusi ndo chanzo Cha tatizo

Na umoja wa Africa ulionyesha udhaifu mkubwa sababu tokea 1960's division tayari ilishaonekana ilikuwa ni matter of when,

Ila watutsi wanaonekana Wana akili japokua walikua wachache yaana walidhihira "wingi sio hoja" waliwaongoza wahutu walio wengi sitaki niongelee mbinu walizokua wanatumia,
 

Ndege hio wakati inadunguliwa nilikua Kigali usiku huo. Eneo ndege hio ilipodunguliwa linaitwa Kanombe jirani kabisa na uwanja wa ndege na ikulu ya wakati huo.
1. Mleta uzi ametaja kua ubalozi ulikua eneo la Kicukiro jambo ambalo kama lingekua kweli ukiwa eneo hilo huwezi kuona anga ya eneo la tukio.
2. Ubalozi wa Tanzania ulikua eneo la Kacyiru ni karibu na eneo la tukio na ilisikika milipuko miwili hivi na mwanga sisi hatukuona wingu.
Note: Balozi zote na mashirika makubwa ya UN au ya kimataifa yalikua katika maeneo matatu (Kacyiru, Kimihurura na Kiyovu)
3. Njia waliopita hao ni ndefu sana na unavuka na unavuka wilaya kama tisa hivi kama sijasahau.
4. Diplomats wengi na wafanyakazi wa UN agencies wengi ilikua wakipata shida wanaita wanajeshi wa UNAMIR sijui kwa nini wao hawakuwajua!!!
Nina historia mbaya katika safari nilizofanya kule kati ya 1990-1994.
Mleta mada usichoke kuwahadithia watu humu kuna mengi ya kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akimaliza tu!.Na wewe tuletee ya kwako.Anza kuiandaa kabisa,usije na mikasa nusunusu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…