dumbi
JF-Expert Member
- Jan 15, 2018
- 988
- 1,542
Ya mwaka ganiHapo waweza tazama movie moja inaitwa "Rules of Engagement" kwa kusindikizia hii story...
Naona wazee wa defender walitangulia kufanya yao..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ya mwaka ganiHapo waweza tazama movie moja inaitwa "Rules of Engagement" kwa kusindikizia hii story...
Naona wazee wa defender walitangulia kufanya yao..
Mkuu kama ulipatia mi mwenyewe naisoma story naelekea zangu jozy natoka cape ..ibana endelea jamaaNipo ndani ya bus.Mkuu umeikatiza,hebu endelea Basi,ili nikaribie Dar,muda huu nipo mikese.Daa bonge la story
Sent using Jamii Forums mobile app
Waliozaliwa chini ya 96 ni waliozaliwa 97,98.99..... ama waliozaliwa 95,94,93....?Hao wengi wao walizaliwa 96 kwenda chini....hawezi jua kitu msamehe tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
2000.Ya mwaka gani
Kuna kitu nilijifunza vitani ,wakati vita inapiganwa si ajabu kuna watu wengine wanapigana hiyo vita hiyo hiyo lakini hawaonekani inakuwa ni siri ya nchi na nchi,yani inakuwa kwa mfano kama ugomvi wa mtaani mnachokozana mkianza kupigana wakati mnandelea kupigana na mchokozi wako jamaa zake au watu wengine kwa maslahi yao binafsi wanakuwa wanakusachi kiaina au wanakuwa wanapenyeza ngumi mbili tatu kwako kumsaidia jamaa yao au kukusaidia wewe.Hapo waweza tazama movie moja inaitwa "Rules of Engagement" kwa kusindikizia hii story...
Naona wazee wa defender walitangulia kufanya yao..
Inaendelea...................... 49k viewers si mchezo.
Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....
Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.
Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.
Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.
Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.
Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .
Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.
Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.
Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.
Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...
Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.
Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.
Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................
Itaendelea...........................................
Sent using Jamii Forums mobile app
Napata wasiwasi kuna baadhi ya mission balozi alikuwa akizichezesha ndio maana kuna vitu umevifungafunga anyway nahisi kuna mkono wa tanzania ulihusika katika kifo cha huyo Rais...
Ukiangalia mbelgiji ndo chanzo Cha mauaji ya kimbari na vikundi vya waasi kivu ya kaskazin na kusini, sababu zile identity card za kuonyesha huyu mhutu yule mtusi ndo chanzo Cha tatizoKuna kitu nilijifunza vitani ,wakati vita inapiganwa si ajabu kuna watu wengine wanapigana hiyo vita hiyo hiyo lakini hawaonekani inakuwa ni siri ya nchi na nchi,yani inakuwa kwa mfano kama ugomvi wa mtaani mnachokozana mkianza kupigana wakati mnandelea kupigana na mchokozi wako jamaa zake au watu wengine kwa maslahi yao binafsi wanakuwa wanakusachi kiaina au wanakuwa wanapenyeza ngumi mbili tatu kwako kumsaidia jamaa yao au kukusaidia wewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yani nasoma hadi mwili unasisimka...but naona umejitahidi sana kuna codes( classified info) nyingi kwenye hii hadithi...funguka tu ni zaidi ya miaka ishirini sasa.
Lile wingu lilisababisbwa na nini?ama ndege iliyotunguliwa ilikua karibu na eneo la ubalozini?
Akimaliza tu!.Na wewe tuletee ya kwako.Anza kuiandaa kabisa,usije na mikasa nusunusu,Ndege hio wakati inadunguliwa nilikua Kigali usiku huo. Eneo ndege hio ilipodunguliwa linaitwa Kanombe jirani kabisa na uwanja wa ndege na ikulu ya wakati huo.
1. Mleta uzi ametaja kua ubalozi ulikua eneo la Kicukiro jambo ambalo kama lingekua kweli ukiwa eneo hilo huwezi kuona anga ya eneo la tukio.
2. Ubalozi wa Tanzania ulikua eneo la Kacyiru ni karibu na eneo la tukio na ilisikika milipuko miwili hivi na mwanga sisi hatukuona wingu.
Note: Balozi zote na mashirika makubwa ya UN au ya kimataifa yalikua katika maeneo matatu (Kacyiru, Kimihurura na Kiyovu)
3. Njia waliopita hao ni ndefu sana na unavuka na unavuka wilaya kama tisa hivi kama sijasahau.
4. Diplomats wengi na wafanyakazi wa UN agencies wengi ilikua wakipata shida wanaita wanajeshi wa UNAMIR sijui kwa nini wao hawakuwajua!!!
Nina historia mbaya katika safari nilizofanya kule kati ya 1990-1994.
Mleta mada usichoke kuwahadithia watu humu kuna mengi ya kujifunza.
Sent using Jamii Forums mobile app