Bahati mbaya mlolongo wa masimulizi haujapewa namba ili nikurejeshe katika kipande husika,
Bossless alidai ubalozi wa Malawi na nyinginezo zilivamiwa siku chache kabla ya hawajapandishwa malori kuondoka Kigali, wakati huo mambo yalipamba moto. Vamizi za balozi hazikulenga wanadiplomasia bali wale wanyarwanda walokimbilia hapo kusaka hifadhi kama ambavyo walikuja ubalozi wa Tanzania. Na hadi watanzania wanaanza safari yao, hakukuwa na shambulio wala uvamizi mkubwa kwenye ubalozi wetu.
Yaani kitu ambacho akili yangu huwa haikiamini katika mikutano ya usuruishi ni nia ya dhati ya wenyeji wa mikutano hiyo. Mara nyingi wasuruhishaji wanao upande wanaoutegemea ushinde. Ndo maana tunayo matukio kadhaa ya viongozi kulipuliwa angani wakitokea katika hiyo mikutano ua suruhu! Rejea kwa Museveni dhidi ya South Sudan; Abyarimana na mwenzake wakitokea Tz... Hata Nkurunziza amekataa kuhudhuria baadhi ya mikutano kwa hofu ya kukutwa na yalowakuta watangulizi wake.
Jamii huelezwa kile ambacho wakuu wanataka kifahamike, ukweli huwa hauwekwi hadharani.
Sent using
Jamii Forums mobile app