Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

@LadyRed bwana, hili Jambo naona huwa unalizungumzia sana. Linakuumiza kwani? Ni kweli kuwa zipo jamii zilikuwa na privilege nyakati za mkoloni, ilà trust me nao walijiongeza sana tu, na wanazidi kujiongeza to-date. Zipo jamii hapa bongo hadi leo hii pamoja na fursa kuwa kwa kila mtu lakini bado they lag behind, hatuwezi kufanana na kuna watu naturally wapo gifted katika utafutaji na kusaidiana. Kuna sehemu leo hii ukienda vijijini japo ni afrika lakini hutaamini kuona palivyo, na kuna mahali ukienda unaweza kuishia kutoa machozi, ndani ya hii bongo.

So pamoja na privilege kuwepo kwa wote, kuna gifted hands, kuna watu wanabebana sanaaa, na wapo ambao hata dada mtu anaona wivu kwa mdogo mtu kuwin maisha.

Ya huko Rwanda siyajui sana, unaweza kuwa sahihi kwa analysis uliyofanya, ila kwa bongo mmmh.
Mkuu huwa napenda kulisemea kwani huwa nawashangaa watu wanaojiona keki wana kipi cha ziada
Ni kama maoni tu kwani lisipodhibitiwa lina nia ya kutugawa tu na si kutuunganisha...lina nia ovu...
Afterall ukishakua exposed na maisha unaelewa binadamu wote ni wale wale ni suala la watu wapewe exposure na nafasi to prove themselves....

mkoloni ndo kaleta maendeleo ya 'aina' flani ya 'kileo' africa
Hivyo waafrika wenyewe kwa wenyewe kujiona kuna classes ni uzwazwa...wa hali ya juu ...hakuna cha naturally gifted wala nini...wamevumbua nini kipya??..hapo ndo utaona ni advantage ya rule ya mkoloni ndo iliwaweka baadhi ya watu mbele kabla ya wengine sio kwamba wale wengine ni vilaza hamnaa ni fursa tuuu...ndo mana sikuhizi kabila zote wasomi na wafanya biashara wapo...it was just a matter of fursa!!

Kwa uelewa wangu mzungu hio ilikua ni strategy ya kutawala...divide and rule...watu anawavuruga weee huku ye anaendelea kupeta

ss shida ni pale alipoondoka
Ilipasea viongozi waweke sawa hio hali
Tanzania Nyerere alifanikiwa
Bila kuwadhibiti baadhi ya watu wangekua na nchi yao huku wakijiona wao ni elites...unadhani nini kingetokea iwapo ktk hio nchi wamemix na kabila ambalo sio elites kama wao?..by default wenye elimu ndo viongozi... hence kujiona keki ndo kunazaliwa hapo...wale waloachwa nyuma kidogo mfano wale 'wachunga ng'ombe' unadhani wangefanyaje kama sio kuwachabanga elites mapanga tu???!!!

nawasifu viongozi watanzania hasa nyerere ali'contain ukabila udini nk
Ndo mana hadi leo dini za kristo na islamzinapokezana vijiti urais hivyo kila mtu anajiskia anawakilishwa

likewise nyadhifa mbalimbali makabila yooote yapo kwa uchache tu
Magu Kanda ya Ziwa
Samia Zanzibar
Majaliwa kanda ya kusini
Baraza limemix watu kibao
Hivyo hakuna kabila linalojiskia wao wameachwa nyuma..likewise dini wanamix madhehebu yote

Shida Rwanda wachache tutsi bado serikali wanataka wengi wawe wao unafikiri wahutu wanafanyeje?....yanatokea yaliyotokeaa ndugu msomajii

Watu wakishakua exposed wanabadilika
 
Mkuu mbona kama unajichanganya kumbuka Rwanda civil war na Rwanda genocide ni vitu viwili tofauti.

Rwanda civil war ndiyo hiyo kuanzia 1990 na ndio maana kulikuwa na mazungumzo ya kutafuta amani ila Rwanda genocide ilikuja baadae baada ya Rais Habyarimana kuuawa.
Mkuu ambacho unatakiwa ufahamu genocide imeanza miaka ya 80 kipindi cha cockroach movement ambapo watutsi walikua wanafanya guerilla warfare kwenye mipaka ya Rwanda so kisasi wanafanyiwa watutsi walio wachache.

Ikumbukwe hao RPF pia walifanya genocide kwenye maeneo walioteka kuanzia 1990 yaani iwe cyangugu cjui ruhengeri kote huko walikuwa hawaamini Mhutu ni kuwapiga risasi na panga kwenda mbele kwahiyo genocide imefanyika ndani ya Rwanda civil war. Rejea kisa cha Kibeho walipoua Wahutu zaidi ya elfu 3 kwenye kambi yao ya wakimbizi wa ndani.

Ila ile ya April to June1994 ni kilele tu cha mauaji lakini kuchinjana kwa genocide kulianza hata kabla Habyarimana hajauawa.
 
Sasa mbona unnaielewesha kwa hasira mkuu. Kwahiyo sasahivi Kuna usawa sasa kelele za nini tena?
Nisamehe bure

kwa sasa sina uhakika ila history/time will tell
Bt kwa maoni yangu nahisi 'wahutu' bado hawajiskii vizuri..ss PK atafanyaje kuwaweka sawa sijui...
 
Aiiyaaaah#&$[emoji51][emoji51][emoji51][emoji2962][emoji849][emoji849][emoji849][emoji848]hili jiwe lako ulilorusha gizani mbona kama kuna watu umewalenga??

Unazingua sana Mim limenipata

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijalenga mtu jmn
Jiwe gizani😂😂
Wakoloni walipekeka mishenari sehemu nyingi tu
 
Mkuu ambacho unatakiwa ufahamu genocide imeanza miaka ya 80 kipindi cha cockroach movement ambapo watutsi walikua wanafanya guerilla warfare kwenye mipaka ya Rwanda so kisasi wanafanyiwa watutsi walio wachache.

Ikumbukwe hao RPF pia walifanya genocide kwenye maeneo walioteka kuanzia 1990 yaani iwe cyangugu cjui ruhengeri kote huko walikuwa hawaamini Mhutu ni kuwapiga risasi na panga kwenda mbele kwahiyo genocide imefanyika ndani ya Rwanda civil war. Rejea kisa cha Kibeho walipoua Wahutu zaidi ya elfu 3 kwenye kambi yao ya wakimbizi wa ndani.

Ila ile ya April to June1994 ni kilele tu cha mauaji lakini kuchinjana kwa genocide kulianza hata kabla Habyarimana hajauawa.
Mkuu hivyo visa vilivyotokea wakati wa civil war kwanini uviite genocide ilihali ni majeshi ya pande mbili yaliyokuwa yanapigana?

Ila ukiangalia matukio ya kuanzia April 1994 ni kwamba ni jamii moja ilichochewa na viongozi wao kushambulia jamii nyingine ili kuwamaliza kabisa tofauti na matukio ya kuanzia 1990 ambayo ni majeshi ya pande mbili yalipigana sio raia.
 
Inaendelea ..............

Sasa nimelazimika kuandika hii mapema Sanaa asubuhi ili kumpa mwenyewe simu yake andelee na mambo yake .(simu ya wife)

Sasa tuendelee tukafika province ya GITARAMA tukashudia Jambo la ajabu Sanaa yani kumepowaa watu wachache Sanaa wanatembea mtaani Ila maduka yako wazi biashara inaendelea tu Kama hakuna kitu kinachoendelea Rwanda nikashangaa Sanaa huwezi amini ilibidi tusimame hapo kwanza kwa muda magari yote yakasimima tukawa tunashuka tumepumzika wengine wanaenda dukani lakini hakuna anaerudi na kitu ikawa ni Yale Yale nipe kitu nikupe kitu ,yani una hela nyingi za manyarwansa unaenda dukani mwenye duka anakwambia Kama unataka labda soda nipe Hilo jacket lako aise ikawa pale watu wanauza majaketi na masweta njaaa............ni hatariii.

Unajua ule mji wa GITARAMA Kuna baridi hatari naifananisha na baridi ya njombe na tunduma mwezi wa sita .yani unavaa jacket ili baridi isiingie kwenye mifupa lakini bado inakuchapa tu Kama kawaida ,watu wakawa wanabadilishana na saa za mikononi kwa biskuti daa njaaa....

Gari zikawashwa tukaanza Sasa safari ya kuelekea province nyingine(nimeisahau jina) tukawa tunaendelea tu na safari Kama kilomita 150 tunamaliza Sasa ndo live tunayakuta majeshi ya hayajulikani Ila baadae niliambiwa ni ni batalio ya PK yanii wapo full vijana wembamba warefu wa kitusi ,Ila nchi ya Rwanda niyakipumbavu Sanaa,Sasa katika kuchunguza kwangu nikagundua Kuna baadhi yao wanahaiba ya kihutu kabisa Sasa nikawa najiuliza hii Vita gani? Mbona sielewi ni yakikabila au ya kimaslahi nikawa nikaaachana na Hilo wazo wakatusimamisha lakini kiistarabu Kama traffic hawa wa kwetu wanavyosimamisha magari ya tukasimama .

Sasa ikawa wanaongea na balozi wetu Ila baadae ilikuja julikana kuwa walikuwa wanadai kipande kilichobaki Cha kuingia mpakani Kati ya Burundi na rwanda Kuna mtanange unaendelea( Wanaume wanachapana risasi ikumbukwe mpaka mda huo Kuna miji ambayo tayari ikishakuwa chini udhibiti wa majeshi ya kagame akitafuta mbinu za kuingia Kigali ) tukashauriwa tusubiri kwanza hali itakapokuwa imetulia Hali tutaendelea na safari

Tukatulia hapo inaelekea saa kumi na mbili ya jioni muda ukawadia tukaruhusiwa Sasa Cha ajabu wale wanajeshi wote walikuwepo wakapanda kwenye yale maroli tukawa tunaelekea njia moja kila roli na wanajeshi Kama nane hivi au kumi nyuma ya bodi safarii ikaanza wazee wapo tayari tayari kwa Hali ile nikasema Sasa hapa tunaingia vitani rasmi safarii ikawa inasonga ,Kuna kitu nilijifunza vitani Mara nyingi vitani wanajeshi wanaongea kwa ishara na Kama wakiamua kuongea Basi huongea kwa sauti ya chini Sanaa.

Sasa tukawa Kama tumeshatembea Kama kilomita 30 hivi Sasa tukaanza kusikia risasi zinarushwa hovyo hovyo kutokea maeneo ya polini wale wanajeshi wakastukia kiongozi wao nikasikia anatoa sauti flani hivi ya kutaka Kama kujibu mashamulizi hivi wale wanajeshi nao wakawa wanarusha risasi hivyo hivyo msituni yani AK 47 zinanguruma kwenye masikio yetu live huku magari yanaendelea tu kutembea Ila kwa mwendo mkali Sanaa jamaa wakawa wanajibu Kuna askali alikuwa amesimama upande wangu alikuwa ana RPG na bunduki akawa anaweka vizuri rocket Ili alivurumishe kwenye vile vichaka akinipa Ak47 halafu ananionyesha niendelee kufyatua risasi kwa mbali kupitia tundu la bodi ya gari (yani nilivyoishika ile chuma Kama dakika mbili tu nikajikuta yani nimepata ujasiri mkubwa bila kutarajia hapo ndo nilisema mwanzo nami nikawa nimepigana angalau Vita kidogo yule mwanajeshi akavurumisha lile li rocket Polini mle ndo risasi zikawa zimepoa safari ikawa inaendelea kwa kasi .

Tukaenda tukafika mbele kidogo Kuna Kijiji kimoja wakashuka wakabaki wanajeshi wachache tu tukaendelea na safari hapo wakatwambia kazi imeisha Sasa tunaweza kwenda Hadi boda tukawa nao wale wachache Hadi boda tukafika Kama saa mbili usiku hivi.

Sasa angalia chakushangaza tukalikuta lile defenda jeupe na wanajeshi wale njemba Saba walioshuka ubalozini siku ile yani wamechafuka vibaya sanaa yani vumbi Hadi kwenye kope wamevaa combati hizi hizi za jeshi letu lakini hazina majina yao wala begi ya bendera ya Tanzania wakasalimiana na wale tuliowa wachukua njiani hapo Sasa nikajiongeza nikajua Hawa wazee ,tofauti na pale ubalozi hawakutaka kuongea na mtu pale wakawa wanasaidia watu kushuka halafu wanatupa na pole kabisa huku wanatabasamu ,majitu yameshiba

Sasa Kuna Jambo pembezo ya mpaka likawa linawashangaza watu ,kwenye ukingo wa Barbara wa daraja watu wakawa wanakimbilia pale kwa wingi kuangalia majini usiku wa mbalamwezi huo( kwa taarifa tu Mpaka wa Burundi na rwanda unatenganishwa na mto au niseme maporomoko Kama Yale ya rusumo sijui jina lake) namimi nikawa nimesogea pale lahaulaaa maiti zinatoka upande wa Burundi wa mto zinaingia upande wa Rwanda wakiwa wamechomwa na miti tumboni nasehemu za sili nikasema hii ni Sasa na burundi kimechafuka au ? Sasa nikawa najiuliza tunaenda wapi tunaluka majivu tunakanyaga Moto .
.
Ukisikia kukataa tamaa ya kuishi ndo ikawa Sasa nimekata tamaa nilijua tukifika Burundi ndo ntakuwa sasa nimepona Sasa nao wamaenza kuchinjana Tena ....watu wa boda usiku huo wakaruhusu magari tu kuvuka upande wa pili wakasema watu Hadi kesho tukalala chini pale boda.....maishaaa

Itaendelea..............


(Narudisha simu kwa wife nikipata muda Tena ntamuomba niendelee sijaenda kwa fundi Leo mvua inanyesha, halafu watu wengi wanajua naishi Dar, japo nimezaliwa Ilala nimekulia Magomeni mapipa mtaa wa kizingo nyumba namba Siri yangu Ila kwa Sasa Mimi naishi Morogoro -wilaya mpya ya Mlimba .tarafa,kata,Kijiji Siri yangu najishughurisha na kilimo Cha mpunga na biashara ya mchele) jumapili njema .

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwako pia comrade!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
@LadyRed bwana, hili Jambo naona huwa unalizungumzia sana. Linakuumiza kwani? Ni kweli kuwa zipo jamii zilikuwa na privilege nyakati za mkoloni, ilà trust me nao walijiongeza sana tu, na wanazidi kujiongeza to-date. Zipo jamii hapa bongo hadi leo hii pamoja na fursa kuwa kwa kila mtu lakini bado they lag behind, hatuwezi kufanana na kuna watu naturally wapo gifted katika utafutaji na kusaidiana. Kuna sehemu leo hii ukienda vijijini japo ni afrika lakini hutaamini kuona palivyo, na kuna mahali ukienda unaweza kuishia kutoa machozi, ndani ya hii bongo.

So pamoja na privilege kuwepo kwa wote, kuna gifted hands, kuna watu wanabebana sanaaa, na wapo ambao hata dada mtu anaona wivu kwa mdogo mtu kuwin maisha.

Ya huko Rwanda siyajui sana, unaweza kuwa sahihi kwa analysis uliyofanya, ila kwa bongo mmmh.
"Kujiongeza" kubebana " mimi nimechukua haya maneno mawili tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mnasema wanaongea lugha moja tena? Mnanichanganya
Kwa jinsi nilivyosoma na kufuatilia hayo yalikuwa mapigano ya koo na koo, maana kwenye tamaduni zote wako sawa.

Kinachokuja kuwatofautisha ni muonekano wa koo la Kitusi na Koo la Kihutu.
 
Mkuu yale hayakuwa mauaji dhidi ya watutsi tu bali ilikuwa ni VITA yaani wakati wahutu wanachinja watutsi na hao Watutsi wanachinja wahutu kutumia vikundi vyao vya waasi mfano INTEREHAMWE/FDLR,APERHUTU kwa Wahutu na be it UPRONA/RPF kwa watutsi na ndio maana kule Uganda kwenye mitaala ya shule haiitwi Rwanda genocide kule tulisoma inaitwa Rwanda civil war yaani VITA sio Mauaji!!

Ila yaonekana kagame alikua kajipanga zaidi hivyo baada ya kushinda vita naye akalipiza kisasi akawachinja hao wahutu wakakimbilia DRC ambapo aliwafuata na kuwateketeza na tokea hapo nguvu ikahama kutoka kwa Wahutu ikaja kwa watutsi na imekua hivyo mpaka leo.

Wahutu sio kwamba wali-fight for nothing" ila walishashinda vita tokea 1959 na wakajikomboa kutoka mikono ya watutsi so walienjoy uhuru wao mpaka 1990 ambapo uvamizi wa Watutsi ulianza. Hivyo ile vita ilikua ni ya kujilinda zaidi dhidi ya uvamizi wa watutsi na sio kuvamia watutsi kama unavyodhani. Yaani kama watutsi wasingetishia kuvamia Rwanda kulikua hakuna haja ya wao kuwaua maana madaraka yalikua kwa wahutu.

Hope umepata picha mkuu
Origin ya hao wavamizi wa Kitutsi ni wapi Mkuu? Kama ni hvyo ni lazima Wahutu watapambania nchi yao tena, na suala la vita nyingine kutokea ni LA MUDA TU.
 
K

Kwa mantiki hiyo mkuu, naamini kwa namna moja au nyingine wahutu watakua wanajipanga kulipiza ili washike hatamu wawachomoe Watusi.

Swali in je wanatumia mbinu gani kujipanga? Tuliona Kagame alitumia RPF akitokea msituni.
Mkuu kagame hakujipanga "msituni" bali alikua na back up ya serikali za kitutsi za Uganda na Burundi ambao pia baada ya kushika hatamu walimsaidia kuwateketeza wahutu waliokimbilia huko DRC.

Wahutu changamoto ni kwamba hawapo organized wala kimkakati kila mtu anapambana kivyake sasa ambacho wanaweza ni kutumia back up ya serikali za kihutu mfano Nkuruzinza na walitakiwa wahakikishe DRC anashinda mtu ambaye hayuko puppet wa Kagame!! Wamechelewa sana.

Maana kagame wakimvamia tu Museveni na Magu watamsaidia so watafeli!! Hapo bado DRC itawafukuza..... Ila kagame na watutsi walikua makini kabla ya uvamizi wanahakikisha serikali za jirani zipo mfukoni.

Hata alopovamia wahutu DRC alihakikisha ameshaongea na kaunda wa Zambia na Dos santos wa Angola kuwa wasiingilie vita. Sasa wahutu hawana ushawishi huo kwenye serikali zetu hivyo vita itakua ngumu sana

Fursa yao pekee ni kuhakikisha Nkuruzinza hatolewi kwa gharama yoyote lasihivyo ndio utakua mwisho wa ndoto zao kurudi Rwanda.
 
Nina rafiki wa kitutsi,siku anamuona jamaa yetu flan mrundi(hutu),akatokea kumchukia ghafla bila hata ya kusema neno lolote,kichonishangaza zaidi na Yule hutu akawa hamsemi vizuri Yule tutsi.kumbuka hawajasemeshana toka wanakutana.sijui wanatambuana vipi?na hakuna aliyewatambulisha,just kuangaliana tu na chuki juu.rwanda imetulia kwa muda tu.
 
Nahisi ndo mana walika wakiuana muda wowote na popote mana unamtambua kwa kumtizama tu

Hawa Wahutu hawana tofauti na sisi kabisa ila hawa Watutsi wanaonekana kabisa kama ni watu fulani wageni hivi,na kama ni mchanganyiko wa asili mbili fofauti.

Ila vita vya hivi kihistoria huwa haviishi, zaidi huwa vinapoa kisha vinaendelea.
 
Origin ya hao wavamizi wa Kitutsi ni wapi Mkuu? Kama ni hvyo ni lazima Wahutu watapambania nchi yao tena, na suala la vita nyingine kutokea ni LA MUDA TU.
Kwa mujibu wa historia kidogo nliyosoma
Wahutu ndo original people of Rwanda...ndo wengi
Ila
Tutsi ni wahamiaji wakitokea Ethiopia somalia nk
Ndo mana wanafanana nao kimuonekano

nafikiri namna pekee ya kuwapoza hutu ni kuwanyanyua wawe kama tutsi na ikibidi rais ajae awe wa kwao
Ss sijui atakua na hasira bado ama atadhamiria kujenga nchi
Ila yaelekea bado kuna 'tension'
 
Origin ya hao wavamizi wa Kitutsi ni wapi Mkuu? Kama ni hvyo ni lazima Wahutu watapambania nchi yao tena, na suala la vita nyingine kutokea ni LA MUDA TU.
Mkuu wote ni kabila moja sema tu wanatofautiana tuseme Koo yaani za wahutu ni kama wabantu zaidi wa magharibi ya Afrika ila watutsi kama koo za Watu wa Ethiopia/Eritrea huko.

So wakoloni wakawagawa..... Ni sawa na leo mkoloni awagawe wachagga kwa kigezo cha weupe na weusi!! Kuwa wachagga weupe awaite watutsi na weusi awaite wahutu ilihali kabila lilelile tu!!

Na hili sio Rwanda tu limetokea Burundi na DRC pia hizi jamii haziwezi kaa pamoja ni kuchinjana kila siku mpaka leo huko Kivu.

Vita yes ni suala la muda tu ila kagame kajipanga sana mkuu ana support ya serikali zote zinazomzunguka hivyo chance yao labda wasubiri siku amefariki ghafla!! Wapate support ya wahutu wa ndani ambao ni 90% ukijumlisha na wahutu waliopo DRC zaidi ya million 2, jumlisha na wahutu wa Burundi aiseee hao watutsi mbona wanateketezwa ndani ya siku moja tu (Mungu aepushe)

Ila ni suala la muda tu
 
Back
Top Bottom