Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

PK alichukia nchi kwa nguvu na sio kura
Samahani wakuu naomba mnijuze hapa
Katika mauaji ya Rwanda inaonekana waliolengwa na kuuliwa zaidi ni watutsi yaani ni kama watutsi walikua wapokea kipigo tu mwanzo mwisho

Sasa ikawaje tena baada ya hapo Rais wa rwanda akawa Mtutsi

Inamaana wahutu pamoja na kujipigania na kuua wahutsi bado hawakuweza kusimamisha kiongozi wa kihutu

Naona KG ndo mbabe sasa, Kwahiyo hutu walistruggle for nothing

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa maoni yangu
Siasa haina nguvu hasa kwa watanzania
Ni kitu u can change ama kuhama
Yani hamna wafia siasa au chama
Mange alijaribu hii siasa na alifeli
Watanzania were not up to it

Tofauti na powerful forces za ukabila
Kabila ni lako tu u have no choice umezaliwa hapo by default
Ukabila is the strongest force ikifuatiwa na dini mana watu hujitoa mhanga kabisaa kisa imani
then siasa ya mwisho kabisa
Kweli siasa haina nguvu hapa kwa watanzania ni ya kimasilahi hawana (philosophy) itikadi, lakini pia makabila pia hayana nguvu kuna watanzania wengi hata wanaogopa kuongea lugha za kikabila yao kwa sababu ya 'inferioty complex' wengi wanajificha kwenye kiswahili hata wakiwa nyumbani

kwahiyo nivingumu watanzania kupigana kwa hayo mambo mawili tu......jambo linalo weza kuleta hisia za watu kwa kiwango cha kuuwana ni Dini, Waislama hawana mzaha na Dini yao na pia it's second to none, wako tayari kuyilinda dini yao hata kama ni kupoteza utaifa au asiri yao hili lilidhihirika pale Rwanda wakati wa Rc walikimbilia misikitini kuliko makanisani hamna Muislamu wanaweza kuua muislam mwenzie kwa sabb ya kua mtusi au muhtu Waislamu wana umoja katika hilo wanasemaga 'Muislamu ndugu ye Muislamu' ....... kuanzia 1992 Dini ya Kiislamu ina heshimika sana Rwanda nawanyarwanda wameslimu wengi wameona Uislamu ni 'pragamatic religion'.

Kitu kama hicho kutokea hapa nchini labda kipitie kwenye Imani za Dini serikali iwe makini ifanye 'fair play' sio kupendelea dhehebu moja nakuache mengine inaweza ikashutua mihemuko na hisia za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu nilijifunza vitani ,wakati vita inapiganwa si ajabu kuna watu wengine wanapigana hiyo vita hiyo hiyo lakini hawaonekani inakuwa ni siri ya nchi na nchi,yani inakuwa kwa mfano kama ugomvi wa mtaani mnachokozana mkianza kupigana wakati mnandelea kupigana na mchokozi wako jamaa zake au watu wengine kwa maslahi yao binafsi wanakuwa wanakusachi kiaina au wanakuwa wanapenyeza ngumi mbili tatu kwako kumsaidia jamaa yao au kukusaidia wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama naiona Tz katika hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu ingekuwa mamtoni Mzee wetu Bossless saivi angekuwa anapiga pesa ndefu sana kupitia vitabu. Najua kuna vitabu vingi sana vimeandikwa na wahanga wa haya mauaji vingi vinauzwa online.

Mzee wetu Bossless angepata mwandishi mzuri mchokonozi wa kukamua kumbukumbu za mzee wetu huyu bila shaka ingetoka bonge la stori iliyonyooka vema.

Binafsi sijawahi kuzichoka stori za haya mauaji japo ni mambo ya kusikitisha sana lakini ukisikia au kusoma unapata hamu ya kusikia au kusoma tena na tena nazan ni ile hali ya kushangaa mambo ya ajabu yanayoweza kufanywa na kiumbe alizaliwa kutoka kwa mwanamke.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea ..............

Sasa nimelazimika kuandika hii mapema Sanaa asubuhi ili kumpa mwenyewe simu yake andelee na mambo yake .(simu ya wife)

Sasa tuendelee tukafika province ya GITARAMA tukashudia Jambo la ajabu Sanaa yani kumepowaa watu wachache Sanaa wanatembea mtaani Ila maduka yako wazi biashara inaendelea tu Kama hakuna kitu kinachoendelea Rwanda nikashangaa Sanaa huwezi amini ilibidi tusimame hapo kwanza kwa muda magari yote yakasimima tukawa tunashuka tumepumzika wengine wanaenda dukani lakini hakuna anaerudi na kitu ikawa ni Yale Yale nipe kitu nikupe kitu ,yani una hela nyingi za manyarwansa unaenda dukani mwenye duka anakwambia Kama unataka labda soda nipe Hilo jacket lako aise ikawa pale watu wanauza majaketi na masweta njaaa............ni hatariii.

Unajua ule mji wa GITARAMA Kuna baridi hatari naifananisha na baridi ya njombe na tunduma mwezi wa sita .yani unavaa jacket ili baridi isiingie kwenye mifupa lakini bado inakuchapa tu Kama kawaida ,watu wakawa wanabadilishana na saa za mikononi kwa biskuti daa njaaa....

Gari zikawashwa tukaanza Sasa safari ya kuelekea province nyingine(nimeisahau jina) tukawa tunaendelea tu na safari Kama kilomita 150 tunamaliza Sasa ndo live tunayakuta majeshi ya hayajulikani Ila baadae niliambiwa ni ni batalio ya PK yanii wapo full vijana wembamba warefu wa kitusi ,Ila nchi ya Rwanda niyakipumbavu Sanaa,Sasa katika kuchunguza kwangu nikagundua Kuna baadhi yao wanahaiba ya kihutu kabisa Sasa nikawa najiuliza hii Vita gani? Mbona sielewi ni yakikabila au ya kimaslahi nikawa nikaaachana na Hilo wazo wakatusimamisha lakini kiistarabu Kama traffic hawa wa kwetu wanavyosimamisha magari ya tukasimama .

Sasa ikawa wanaongea na balozi wetu Ila baadae ilikuja julikana kuwa walikuwa wanadai kipande kilichobaki Cha kuingia mpakani Kati ya Burundi na rwanda Kuna mtanange unaendelea( Wanaume wanachapana risasi ikumbukwe mpaka mda huo Kuna miji ambayo tayari ikishakuwa chini udhibiti wa majeshi ya kagame akitafuta mbinu za kuingia Kigali ) tukashauriwa tusubiri kwanza hali itakapokuwa imetulia Hali tutaendelea na safari

Tukatulia hapo inaelekea saa kumi na mbili ya jioni muda ukawadia tukaruhusiwa Sasa Cha ajabu wale wanajeshi wote walikuwepo wakapanda kwenye yale maroli tukawa tunaelekea njia moja kila roli na wanajeshi Kama nane hivi au kumi nyuma ya bodi safarii ikaanza wazee wapo tayari tayari kwa Hali ile nikasema Sasa hapa tunaingia vitani rasmi safarii ikawa inasonga ,Kuna kitu nilijifunza vitani Mara nyingi vitani wanajeshi wanaongea kwa ishara na Kama wakiamua kuongea Basi huongea kwa sauti ya chini Sanaa.

Sasa tukawa Kama tumeshatembea Kama kilomita 30 hivi Sasa tukaanza kusikia risasi zinarushwa hovyo hovyo kutokea maeneo ya polini wale wanajeshi wakastukia kiongozi wao nikasikia anatoa sauti flani hivi ya kutaka Kama kujibu mashamulizi hivi wale wanajeshi nao wakawa wanarusha risasi hivyo hivyo msituni yani AK 47 zinanguruma kwenye masikio yetu live huku magari yanaendelea tu kutembea Ila kwa mwendo mkali Sanaa jamaa wakawa wanajibu Kuna askali alikuwa amesimama upande wangu alikuwa ana RPG na bunduki akawa anaweka vizuri rocket Ili alivurumishe kwenye vile vichaka akinipa Ak47 halafu ananionyesha niendelee kufyatua risasi kwa mbali kupitia tundu la bodi ya gari (yani nilivyoishika ile chuma Kama dakika mbili tu nikajikuta yani nimepata ujasiri mkubwa bila kutarajia hapo ndo nilisema mwanzo nami nikawa nimepigana angalau Vita kidogo yule mwanajeshi akavurumisha lile li rocket Polini mle ndo risasi zikawa zimepoa safari ikawa inaendelea kwa kasi .

Tukaenda tukafika mbele kidogo Kuna Kijiji kimoja wakashuka wakabaki wanajeshi wachache tu tukaendelea na safari hapo wakatwambia kazi imeisha Sasa tunaweza kwenda Hadi boda tukawa nao wale wachache Hadi boda tukafika Kama saa mbili usiku hivi.

Sasa angalia chakushangaza tukalikuta lile defenda jeupe na wanajeshi wale njemba Saba walioshuka ubalozini siku ile yani wamechafuka vibaya sanaa yani vumbi Hadi kwenye kope wamevaa combati hizi hizi za jeshi letu lakini hazina majina yao wala begi ya bendera ya Tanzania wakasalimiana na wale tuliowa wachukua njiani hapo Sasa nikajiongeza nikajua Hawa wazee ,tofauti na pale ubalozi hawakutaka kuongea na mtu pale wakawa wanasaidia watu kushuka halafu wanatupa na pole kabisa huku wanatabasamu ,majitu yameshiba

Sasa Kuna Jambo pembezo ya mpaka likawa linawashangaza watu ,kwenye ukingo wa Barbara wa daraja watu wakawa wanakimbilia pale kwa wingi kuangalia majini usiku wa mbalamwezi huo( kwa taarifa tu Mpaka wa Burundi na rwanda unatenganishwa na mto au niseme maporomoko Kama Yale ya rusumo sijui jina lake) namimi nikawa nimesogea pale lahaulaaa maiti zinatoka upande wa Burundi wa mto zinaingia upande wa Rwanda wakiwa wamechomwa na miti tumboni nasehemu za sili nikasema hii ni Sasa na burundi kimechafuka au ? Sasa nikawa najiuliza tunaenda wapi tunaluka majivu tunakanyaga Moto .
.
Ukisikia kukataa tamaa ya kuishi ndo ikawa Sasa nimekata tamaa nilijua tukifika Burundi ndo ntakuwa sasa nimepona Sasa nao wamaenza kuchinjana Tena ....watu wa boda usiku huo wakaruhusu magari tu kuvuka upande wa pili wakasema watu Hadi kesho tukalala chini pale boda.....maishaaa

Itaendelea..............


(Narudisha simu kwa wife nikipata muda Tena ntamuomba niendelee sijaenda kwa fundi Leo mvua inanyesha, halafu watu wengi wanajua naishi Dar, japo nimezaliwa Ilala nimekulia Magomeni mapipa mtaa wa kizingo nyumba namba Siri yangu Ila kwa Sasa Mimi naishi Morogoro -wilaya mpya ya Mlimba .tarafa,kata,Kijiji Siri yangu najishughurisha na kilimo Cha mpunga na biashara ya mchele) jumapili njema .

Sent using Jamii Forums mobile app
Nasisimka.. Pole Sana Mkuu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kama kuna kitu umenote! Wala haikuwa katika kumshambulia, comment yangu imekaa kimasihara zaidi!!

Mnapokuwa sehemu moja, iwe shule, chuo,kijiweni hata ofisini kuna masihara huwa yanaendelea hata kama rika tofaut.

Kuna sehem nimemquote nikionesha kabisa heye ni baba kwangu! Na sijaona mahala kaandika kwa kuchukua nadhani aliielewa comment yangu! Mie sio mtu wa kihivyo, sio mkosefu wa adabu kwa watu, mfano mdogo humu jf sikumbuki kama nishawahi mkosea mtu adabu mzee!

Ila asante kwa ukumbusho.
Kijana mdogo lakini una busara sana,,,,safi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Da Huyo mama balozi nimemkubali anastahili heshima zake,Mungu amlinde huko alipo.

Sijui na mabalozi wetu hawa kina Pindi Chana wana ujasiri huo kweli au ndio ufia chama tu

Nimekaa nafikiria mtu anamshushia kaka yake upanga shingoni nashindwa kupata picha kabisa,au mtu unamuua na kumchoma sehemu za siri na kuwaunganisha kama panzi daa! sijui hio roho inakuwa imetoka wapi?

Mleta mada vipi kuhusu hao watoto aliowapigania balozi una taarifa nao? na vipi kuhusu Demu wako yule Mnyarwnda?





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa mbona unnaielewesha kwa hasira mkuu. Kwahiyo sasahivi Kuna usawa sasa kelele za nini tena?
Jmn mbona huelewi
Ushaambiwa hamna usawa

Ni kama vile hapa bongo baadhi ya watu walipeana kazi kwa vimemo akishakujua jina tu anajua kabila gani hivyo anaamua akupe au asikupe
Kulikua na usawa hapo?.
Ama viongozi wengi wakitokea sehemu fulani unafikiri nini kinafuata iwapo hawana hekima?.si ni kupeleka maendeleo kwao na kusahau umoja wa nchi!!!
Wale waliosahaulika unafikiri wanajiskiaje na kodi zao ndo zinaimarisha upande mwingine?.!!

Sasa hivi ndo mifumo imeimarika fursa zinaenda kwa wengi zaidi nchi nzima..haikua hivi
 
Point of correction. Kiingereza Cha kimbari ni "massacre''. Mauaji ya kimbari = Massacre killings. Yaani mauji ya watu wengi ambayo NI endelevu au kwa muda mfupi.
" Mauaji ya kimbari = Massacre killings. Yaani"

Mkuu tafadhari mind your translation hamna kiingereza kama hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia Kanisa hasa Katoliki lilitumika sana kutekeleza mauji haya. Watu waliokwenda kupata hifadhi makanisani walijikuta wakiuliwa baada ya kuuzwa kwa interahamwe na viongozi wa Kanisa
Ilikuwa situation ambayo huwezi kufanya uchaguzi kama unataka kuendelea kuishi.unaambiwa kabisa utoe orodha ya waumini wako kati ya hutu or tutsi..wakifika unawapa majina wanachakuwa tutsi wanawaua.sasa kama hutaki unakufa wewe.ealisulutishwa hawakuwa na namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom