Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

CCM tuwaangalie jamani UVCCM ni hatari sana, hawa CCM tuwaondoe mapema ili tujenge utamaduni wa kuachiana uongozi. Kama mwanasiasa anapowakosoa tu wanaamua kumuua vipi huko mbele.
Mikutano ya wapinzani inazuiwa (Heche) na polisi ya wao inaruhusiwa kufanya fujo mbele ya mkutano wa mpinzani sawa je kwao itakuwaje?
Tunakoelekea sipajui. Intarahamwe wa bongo ngoja waanze kupewa vyombo vya ncha kali tuone


Sent using Jamii Forums mobile app
na CCM ndo watakao iangamiza nchi kwa kuleta machafuko, angalia kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa walichokifanya, kama siyo uungwana wa kijinga wa watanzania wa kukubali kudhulumiwa haki zao hiyo tu ilikuwa ni tiketi ya kuipeleka nchi kwenye machafuko.

Msimuliaji wa kisa hiki kuna jambo moja la maana sana kalielezea kuwa ukiona vyama vya siasa vimeanzisha vikundi vyao vya ulinzi ujue kuwa imani kwa jeshi la polisi imekwisha na kinachofuata hapo ni nchi kuingia kwenye machafuko.

Nterahamwe kikosi kikuu cha mauaji kilikuwa ni kikundi cha ulinzi kilichoanzishwa na chama tawala na ndicho kilichoendesha mauaji ya hatari sana nchini Rwanda ambayo kwa kiasi fulani na mimi niliyashuhudia kwa kuwa nilikuwa karibu na maeneo hayo ndo maana sina swali lolote kwa msimuliaji wa kisa kwa kuwa na mimi niliguswa.

Ukiachilia mauaji ya kuuawa kamanda Mawazo, kwa macho yangu nimeshuhudia wagombea 2 wa upinzani wanapigwa mapanga mbele yangu na vijana wa kikundi cha ulinzi cha CCM katika uchaguzi wa serekali za mitaa wa mwaka 2014 kwa kuwa tu CCM walitaka wapite bila kupingwa.

Hata hivi vikundi vya ulinzi ndani ya vyama waanzilishi walikuwa ni CCM.
 
Kuna nyuzi huwa zinasababisha tufahamu kiwango cha IQ za watu flani flani Muraa
Asante Mkuu! Hiyo ni kwa mujibu wa sheria za kidiplomasia...

...hivi unaielewa vita mkuu!! Kuna kombola linaloweza kukwepa balozi kwa kuwa sheria zinailinda balozi! Unamkubuka aliyeponyokwa na roketi ya begani wakati watz wamezungukwa na interahamwe!! Kama jengo la ubalozi lingekuwa karibu, sheria zingesaidia nini!!

Fita ni fita muraa!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatambuaje kuwa huyu kabila hii huyu kabila hii?
Wana muonekano tofauti sana

Unaweza watambua kwa muonekano tu
93E16B81-7242-4237-ADCC-B6C58C657EE1.jpeg

9B49A753-412D-42C6-86C6-BD52F34441B7.jpeg

9A437BBE-302F-4A40-B844-6C10906A4478.jpeg
 
Sijui kama kuna kitu umenote! Wala haikuwa katika kumshambulia, comment yangu imekaa kimasihara zaidi!!

Mnapokuwa sehemu moja, iwe shule, chuo,kijiweni hata ofisini kuna masihara huwa yanaendelea hata kama rika tofaut.

Kuna sehem nimemquote nikionesha kabisa heye ni baba kwangu! Na sijaona mahala kaandika kwa kuchukua nadhani aliielewa comment yangu! Mie sio mtu wa kihivyo, sio mkosefu wa adabu kwa watu, mfano mdogo humu jf sikumbuki kama nishawahi mkosea mtu adabu mzee!

Ila asante kwa ukumbusho.
pamoja sana chief
 
Mbona mnasema wanaongea lugha moja tena? Mnanichanganya
 
Haya jazia jaziaa nyama hizo.eti mbona mnasema wanaongea lugha moja sasa inakuaje tena wanapigana?
Sadly this is not ur home utupangie tufanye nini ooopss...kikubwa tufate sheria za JF

hujaona wadau walokua rwanda pia miaka hio wamejazia nyama tumeelewa zaidi
 
RIP MCH.MTIKILA alinipa mwanga kidogo!!Mauaji yaliratibiwa ikulu ya Dar!Wakapiga ndege wawili kwa jiwe moja!!!JK nyerere alifanikiwa kupachika vijana wake uganda,Rwanda,Burundi na DRC!!!Hadi sasa Watutsi wamejipenyeza Tz!wapo wa kutosha kwenye system!!!
Kama jk alipenyeza watu wake hizo nchi imekuwaje sasa iko v. versa kwamba watoto wa rwanda ndo wako kwenye tz system?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo balozi alikuwa akiitwa nani??
Inaendelea .............

Tulipoishia Sasa tukawa tumefikia kuimaliza province ya Butare hapo ndio tukakuta kizuizi interahamwe kibao kama Mia mbili hivi na kila mtu na panga wengine wamebeba RPG wengine vibomu vya Mikono halafu pembeni Kuna maiti kibao, Sasa kilichonistua zaidi maeneo yale kulikuwa na maiti mbili za wazungu nahisi atakuwa mke na mume, Sasa nikajiuliza kama hawa wazungu wameuawa sisi ni akina nani tusiuawe. Ikawa Sasa magari yamesimamishwa .

Sasa nikawa nawaza hivi lile defender limeenda wapi na wale jamaa hapa siwangesaidia au katika mapigano Yale pale darajani limeangukia mto Nyabarongo. Sasa hapo ikawa ni kushuka wote hakuna Cha dereva wala utingo unazima gari chini maroli 24 yote watu tukawa chini jamaa wanaimba nyimbo zao za chama mapanga juu yanalia tu nguo zao zimejaa damu nikajisemea sasa tumekwisha ikabidi balozi atoke kwenye gari lake aje nyuma kwenye maroli.

Sasa ikawa tumepangwa kwenye mstari unanyanyua passport yako juu huna unakaa pembeni, Kama unakumbuka kuna watu nilisema wakati tunavuka daraja walikuwa wanapanda maroli ya nyuma nao walikuwa wanakimbia Kigali sasa ikaja kimbembe kumbe hawana karatasi (passport) Ila ni wanyarwanda aise wakawa wanawekwa pembeni tu haijalishi ni mtusi au ni mhutu

Sasa hapo likaja swali wakawa wanaulizwa wale jamaa kwanini mnakimbia wakati nyinyi ni wahutu kwanini msibaki mpambanie nchi yenu wakawa wanajitetea tu aise likatokea jamaa likamkata na panga moja wapo miongoni mwa wale eneo la shingoni damu ikaruka aise mwili wangu haujawahi kufa ganzi Kama siku ile (Kuna kitu nimejifunza na kimekuwa kikijadiriwa Sana humu binadamu anapokaribia kufa huwa hasikii maumivu yeyote huwa anakuwa Kama amepigwa na ganzi Kama tutaendelea kunifuatilia nitaelezea tukio lilonitokea nikiwa nikiwa jela Ndola-Zambia baadae sana, msistuke nimeshafungwa jela miaka mitatu kisa biashara za chuma chakavu) tuendelee...

Sasa Yule mtu aliepigwa panga akawa amedondoka anakoroma Kama mbuzi aise kwa kweli pale akili iliondoka kidogo nikawa kama nimehama ulimwenguni kwa sekunde kadhaa hapo wote passport zipo juu yaani unanyoosha Mikono na passports jamaa linapita linakagua aise ikawa huku Zoezi la kuwasurubu wale wahutu wengine likiendelea Sasa Kuna watu sijui ni ndugu wale nao walikuwa wamedandia roli wakawa chini pamoja nasi yule mkubwa akapewa panga amkate yule mdogo shingoni ikawa jamaa anasita sita wakasema Sasa tunawaua wote si hutaki, pale pale yule mkubwa akampa mpanga yule mdogo halafu alikuwa amevaa Sweta zile zenye kofia akaivua akakunja shingo akamwambia yule mdogo piga shingoni ikawa Kama anasita Ila Kaka mtu akamwambia piga yule dogo akapiga kweli damu ikaruka hadi nilipokuwa nimesimama Hadi matonetone yakawa yamechafua kidogo suruali niliyokuwa nimevaa aise jamaa kadondoka mzima mzima paaaa...

Sasa hapo balozi anaongea na lile jamaa lililoonekana Kama ndio kamanda lao Ila likawa Kama halina time nae vile nikajisemea Leo hatutoki, majamaa yanapanda kwenye maroli yanachukua kila kitu kilichokuwemo mikate, nguo, viredio, majiko na masufuria ya kupikia


Sasa hapo tukawa njia panda. Sasa wakati lile njembaa linakagua aise likafika kwenye gari ya balozi likawaona wale mabinti aise acha liwachomoe unaujua ile gari ya balozi Ilikuwa na tinted hivyo alivyoshuka aliwaacha, watoto wakachomolewa wakavutwa nywele Kama kuku vile unavyomtoa bandani ikawa Sasa mzozo kila interehamwe anataka awavute ikawa mzozo mabinti wale wakawa katika ya msitu wa wauaji

Mwanzoni nilisema Kuna matukio mawili ambayo Aliyafanya balozi Hadi nikamvulia kofia nimetaja la kwanza pale ubalozi, Sasa Hili ni la pili yule mama (balozi) alichomoka pale pale alipokuwa akaingia katikati ya msitu wa wale jamaa akawa anavutana nao yaani anawavuta wale watoto na wale interehamwe wanawavuta wale watoto sasa ikawa vurugu tupu ikabidi wale watoto wawe wamemuinamia balozi tumboni Kama vile kuku anae atamia, uongo mbaya siku ile ndio nilimchukia balozi wangu yani nilimuuona Hana maana kabisa yaani kwa kitendo kile alichokuwa amekifanya nilijua Sasa anaamsha hasira za interahamwe Sasa tunakufa wote. Dhana ya kuogopana ikawa imechukua nafasi tumefikia mwisho wa uharibifu kila mtu anatetea nafsi yake (nikaona Bora angeacha tu wauawe wale mabinti sisi tuendelee na safari yetu mungu anisamehe ila mawazo hayo yalikuwa Bora kuliko kitu chochote kwa wakati ule)

Mama kakomaa aise lile jamaa likawa limefika pale, balozi kishati chake kimechanwa imebaki sidiria tu na alivaa sketi mama kakomaa lile jamaa likatoa sauti kwa kinyarwanda REKAA hiyo sauti huwa siisahau (maanake nafikiri ni achaa) Sasa wakati anasema vile kuna tukio lilienda sambamba na ile sauti nusu tufe aise.

Unajua roketi ya mkono RPG ukiwa umeibeba lazima uelekeze juu Sasa Kuna interahamwe moja sijui Ilikuwa aje, unajua Hawa hawana mafunzo wameokotwa tu mitaani aliishika Kama vile kashika bunduki ya kawaida Sasa wakati wa vuta ni kuvute sijui lilishika kwenye triga chuma ikachomoka ikapita katika ya watu, ikapita katika ya roli na gari ya balozi tukasikia mripuko aise kila mtu pale alichanganyikiwa yanii ni moshi mtupu Sasa ikawa haijulikani imetokea wapi imerushwa au imekuwaje Tena?

Intetahamwe wakasambaa wengine wakawa wanakimbilia mabondeni, kama dakika kumi zikapita tukawa tumepowaa kidogo Ila kelele tupu lile jamaa likamsogelea balozi likamuuliza hao ni akina akasema wanangu unajua balozi alikuwa mweupe na wale watoto walikuwa weupe kwa struggle ile lile jamaa halikutia shaka tena, mwanamke kumpigania mtoto namna ile hata wewe huwezi kataa kuwa sio mwanae Sasa hapo tukawa tumetulia kidogo jamaa wakaturuhusu safari ikaanza hapo watanzania watupu wale wadandiaji wote walishushwa sijui kilichoendelea nyuma Sasa tukawa tunaingia province ya GITARAMA safari anaendelea upo kwenye kibini za maroli lakini unasikia dereva anaingiza gia Kama vile hataki kwackweli kwa lile tukio kila mtu alikataa tamaa kabisa....

Sasa tunaingia mji wa GITARAMA tunashuhudia Jambo ambalo linatuacha wote tumeduwaa na mi Domo wazi....Ila hakuna wakumuuliza mwenzake. ......jambo gani hilo?

Itaendelea......................................



( Ila kisimu Cha wife daa sijakizoea battan zake napata shida kweli kuandika)

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya jazia jaziaa nyama hizo.eti mbona mnasema wanaongea lugha moja sasa inakuaje tena wanapigana?
Chanzo cha kupigana ni kabila moja/tutsi minority kujiona bora kuliko wengine/hutu majority kwa zaidi ya miaka 200

Ilianzia kwa 'divide and rule' ya mkoloni
Hata alivyoondoka wakaendelea kujiona wao ndo watu wengine ni sub class

Nmeeleza kifupi hapo nyuma uliponishushua
Zaidi soma google yako bayana
 
Mkuu ungekua mtanzania unaefuatilia mambo ya nchi hii ungeshaelewa
Nina uhakika na nilichoandika
Ila kwa kua huu uzi si wa TZ ni wa Rwanda tuendelee na hio mada
Afterall...TZ kwa sasa ni ngumu kuigawa walishadhibitiwa watu wa aina hiyo
Hao watusi wa bongo naamini huko mbeleni watawaibua wahutu wao wenyewe.

Hii arrogance ya kujifaragua kuwa wao ndo 1st class citizens ikipata watu wa kutia kiberiti hisia za upande wa pili,kwisha habari.
 
Endelea kueelezea sasa nimekuruhusu.
Chanzo cha kupigana ni kabila moja/tutsi minority kujiona bora kuliko wengine/hutu majority kwa zaidi ya miaka 200

Ilianzia kwa 'divide and rule' ya mkoloni
Hata alivyoondoka wakaendelea kujiona wao ndo watu wengine ni sub class

Nmeeleza kifupi hapo nyuma uliponishushua
Zaidi soma google yako bayana
 
Back
Top Bottom