Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Eti bikira Maria alitokea akaonya shubaaaajit toa upuuzi wako hapa
Hata ukichek baadhi ya movie walizoigiza kuhusu haya mauji
Pia baadhi ya kesi viongozi wengi wa kanisa walichochea haya mauaji, watu wanakimbilia kanisani viongozi wa kanisa wanakwenda kuwastua wauaji wanakuja kufanya yaoo
Hayo ya kutokea bikra Maria ni swagger tuu kutoana mchezoni
Hakuna loloteeee
 
Makabila gani hayo yenye nia ya kuligawa taifa? Yataje kama una uhakika na ulichoandika?
Mkuu ungekua mtanzania unaefuatilia mambo ya nchi hii ungeshaelewa
Nina uhakika na nilichoandika
Ila kwa kua huu uzi si wa TZ ni wa Rwanda tuendelee na hio mada
Afterall...TZ kwa sasa ni ngumu kuigawa walishadhibitiwa watu wa aina hiyo
 
Inaendelea ..............

Sasa nimelazimika kuandika hii mapema Sanaa asubuhi ili kumpa mwenyewe simu yake andelee na mambo yake .(simu ya wife)

Sasa tuendelee tukafika province ya GITARAMA tukashudia Jambo la ajabu Sanaa yani kumepowaa watu wachache Sanaa wanatembea mtaani Ila maduka yako wazi biashara inaendelea tu Kama hakuna kitu kinachoendelea Rwanda nikashangaa Sanaa huwezi amini ilibidi tusimame hapo kwanza kwa muda magari yote yakasimima tukawa tunashuka tumepumzika wengine wanaenda dukani lakini hakuna anaerudi na kitu ikawa ni Yale Yale nipe kitu nikupe kitu ,yani una hela nyingi za manyarwansa unaenda dukani mwenye duka anakwambia Kama unataka labda soda nipe Hilo jacket lako aise ikawa pale watu wanauza majaketi na masweta njaaa............ni hatariii.

Unajua ule mji wa GITARAMA Kuna baridi hatari naifananisha na baridi ya njombe na tunduma mwezi wa sita .yani unavaa jacket ili baridi isiingie kwenye mifupa lakini bado inakuchapa tu Kama kawaida ,watu wakawa wanabadilishana na saa za mikononi kwa biskuti daa njaaa....

Gari zikawashwa tukaanza Sasa safari ya kuelekea province nyingine(nimeisahau jina) tukawa tunaendelea tu na safari Kama kilomita 150 tunamaliza Sasa ndo live tunayakuta majeshi ya hayajulikani Ila baadae niliambiwa ni ni batalio ya PK yanii wapo full vijana wembamba warefu wa kitusi ,Ila nchi ya Rwanda niyakipumbavu Sanaa,Sasa katika kuchunguza kwangu nikagundua Kuna baadhi yao wanahaiba ya kihutu kabisa Sasa nikawa najiuliza hii Vita gani? Mbona sielewi ni yakikabila au ya kimaslahi nikawa nikaaachana na Hilo wazo wakatusimamisha lakini kiistarabu Kama traffic hawa wa kwetu wanavyosimamisha magari ya tukasimama .

Sasa ikawa wanaongea na balozi wetu Ila baadae ilikuja julikana kuwa walikuwa wanadai kipande kilichobaki Cha kuingia mpakani Kati ya Burundi na rwanda Kuna mtanange unaendelea( Wanaume wanachapana risasi ikumbukwe mpaka mda huo Kuna miji ambayo tayari ikishakuwa chini udhibiti wa majeshi ya kagame akitafuta mbinu za kuingia Kigali ) tukashauriwa tusubiri kwanza hali itakapokuwa imetulia Hali tutaendelea na safari

Tukatulia hapo inaelekea saa kumi na mbili ya jioni muda ukawadia tukaruhusiwa Sasa Cha ajabu wale wanajeshi wote walikuwepo wakapanda kwenye yale maroli tukawa tunaelekea njia moja kila roli na wanajeshi Kama nane hivi au kumi nyuma ya bodi safarii ikaanza wazee wapo tayari tayari kwa Hali ile nikasema Sasa hapa tunaingia vitani rasmi safarii ikawa inasonga ,Kuna kitu nilijifunza vitani Mara nyingi vitani wanajeshi wanaongea kwa ishara na Kama wakiamua kuongea Basi huongea kwa sauti ya chini Sanaa.

Sasa tukawa Kama tumeshatembea Kama kilomita 30 hivi Sasa tukaanza kusikia risasi zinarushwa hovyo hovyo kutokea maeneo ya polini wale wanajeshi wakastukia kiongozi wao nikasikia anatoa sauti flani hivi ya kutaka Kama kujibu mashamulizi hivi wale wanajeshi nao wakawa wanarusha risasi hivyo hivyo msituni yani AK 47 zinanguruma kwenye masikio yetu live huku magari yanaendelea tu kutembea Ila kwa mwendo mkali Sanaa jamaa wakawa wanajibu Kuna askali alikuwa amesimama upande wangu alikuwa ana RPG na bunduki akawa anaweka vizuri rocket Ili alivurumishe kwenye vile vichaka akinipa Ak47 halafu ananionyesha niendelee kufyatua risasi kwa mbali kupitia tundu la bodi ya gari (yani nilivyoishika ile chuma Kama dakika mbili tu nikajikuta yani nimepata ujasiri mkubwa bila kutarajia hapo ndo nilisema mwanzo nami nikawa nimepigana angalau Vita kidogo yule mwanajeshi akavurumisha lile li rocket Polini mle ndo risasi zikawa zimepoa safari ikawa inaendelea kwa kasi .

Tukaenda tukafika mbele kidogo Kuna Kijiji kimoja wakashuka wakabaki wanajeshi wachache tu tukaendelea na safari hapo wakatwambia kazi imeisha Sasa tunaweza kwenda Hadi boda tukawa nao wale wachache Hadi boda tukafika Kama saa mbili usiku hivi.

Sasa angalia chakushangaza tukalikuta lile defenda jeupe na wanajeshi wale njemba Saba walioshuka ubalozini siku ile yani wamechafuka vibaya sanaa yani vumbi Hadi kwenye kope wamevaa combati hizi hizi za jeshi letu lakini hazina majina yao wala begi ya bendera ya Tanzania wakasalimiana na wale tuliowa wachukua njiani hapo Sasa nikajiongeza nikajua Hawa wazee ,tofauti na pale ubalozi hawakutaka kuongea na mtu pale wakawa wanasaidia watu kushuka halafu wanatupa na pole kabisa huku wanatabasamu ,majitu yameshiba

Sasa Kuna Jambo pembezo ya mpaka likawa linawashangaza watu ,kwenye ukingo wa Barbara wa daraja watu wakawa wanakimbilia pale kwa wingi kuangalia majini usiku wa mbalamwezi huo( kwa taarifa tu Mpaka wa Burundi na rwanda unatenganishwa na mto au niseme maporomoko Kama Yale ya rusumo sijui jina lake) namimi nikawa nimesogea pale lahaulaaa maiti zinatoka upande wa Burundi wa mto zinaingia upande wa Rwanda wakiwa wamechomwa na miti tumboni nasehemu za sili nikasema hii ni Sasa na burundi kimechafuka au ? Sasa nikawa najiuliza tunaenda wapi tunaluka majivu tunakanyaga Moto .
.
Ukisikia kukataa tamaa ya kuishi ndo ikawa Sasa nimekata tamaa nilijua tukifika Burundi ndo ntakuwa sasa nimepona Sasa nao wamaenza kuchinjana Tena ....watu wa boda usiku huo wakaruhusu magari tu kuvuka upande wa pili wakasema watu Hadi kesho tukalala chini pale boda.....maishaaa

Itaendelea..............


(Narudisha simu kwa wife nikipata muda Tena ntamuomba niendelee sijaenda kwa fundi Leo mvua inanyesha, halafu watu wengi wanajua naishi Dar, japo nimezaliwa Ilala nimekulia Magomeni mapipa mtaa wa kizingo nyumba namba Siri yangu Ila kwa Sasa Mimi naishi Morogoro -wilaya mpya ya Mlimba .tarafa,kata,Kijiji Siri yangu najishughurisha na kilimo Cha mpunga na biashara ya mchele) jumapili njema .

Sent using Jamii Forums mobile app
Babu nahitaji mchele wajukuu zako wale asee nikipata kama kilo 50 sio haba .nisaidie namna yakukupata nioe no tugmfanye biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania siasa ndio jambo la hatari kuliko chochote kwa sasa! Kuna kadi ya ccm mara kadi ya chadema nk. Hizi kadi ni suala la muda tu, zinaweza kutumika kufanya ubaguzi na baadaye kusababisha mauji makubwa kwa watanzania. Wenye mamlaka hawaoni, tusio na mamlaka tunaona lkn hatuna namna ya kufanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa maoni yangu
Siasa haina nguvu hasa kwa watanzania
Ni kitu u can change ama kuhama
Yani hamna wafia siasa au chama
Mange alijaribu hii siasa na alifeli
Watanzania were not up to it

Tofauti na powerful forces za ukabila
Kabila ni lako tu u have no choice umezaliwa hapo by default
Ukabila is the strongest force ikifuatiwa na dini mana watu hujitoa mhanga kabisaa kisa imani
then siasa ya mwisho kabisa
 
Kuwa salama kwa Tanzania sio kwamba inshu za ukabila au udini hazikufanya au hazipo Ila n distance Kati ya hzo pande ndio ilkua inafanya Hilo Jambo lisiwezekane sie tuna eneo kubwa Sana alafu population yetu n ndogo katika eneo tulilonalo Mana Kuna distance Zaid ya 300km kuuacha utamadun mmoja Hadi mwingine.

Hvyo sehemu Kama Burundi, kenya, Rwanda na Uganda walifanikiwa Sana sababu yakuwa na eneo dogo na population kubwa kwenye eneo Moja pia DRC na Sudan.

Hata hapa Tanzania wanatamani Sana tuingie kwenye machafuko ya sisi kwa sisi ili waje kusema wanalinda Aman wajichukulie vyakao

Hawa wanasiasa Tena Hawa maarafu ndio agents wa kutupeleka huko kaa chin uwafuatilie utaona Kuna kitu huyu JPM anajitahidi kufikisha kijiti salama Sana japo JK ilkua imebaki kidogo tuu tuingie humo kumbuka ya green guard, red gurd, cuf sijui iliitwaje Mara panyaroad Mara vikund vya kijingajinga tuu.
JK ana mazuri yake na mabaya yake. JPM pia hivyo hivyo. Kuna kitu kinachotakiwa kufanyika kwenye Taifa hili sio hadi tuuane kama wakenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahani wakuu naomba mnijuze hapa
Katika mauaji ya Rwanda inaonekana waliolengwa na kuuliwa zaidi ni watutsi yaani ni kama watutsi walikua wapokea kipigo tu mwanzo mwisho

Sasa ikawaje tena baada ya hapo Rais wa rwanda akawa Mtutsi

Inamaana wahutu pamoja na kujipigania na kuua wahutsi bado hawakuweza kusimamisha kiongozi wa kihutu

Naona KG ndo mbabe sasa, Kwahiyo hutu walistruggle for nothing

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu yale hayakuwa mauaji dhidi ya watutsi tu bali ilikuwa ni VITA yaani wakati wahutu wanachinja watutsi na hao Watutsi wanachinja wahutu kutumia vikundi vyao vya waasi mfano INTEREHAMWE/FDLR,APERHUTU kwa Wahutu na be it UPRONA/RPF kwa watutsi na ndio maana kule Uganda kwenye mitaala ya shule haiitwi Rwanda genocide kule tulisoma inaitwa Rwanda civil war yaani VITA sio Mauaji!!

Ila yaonekana kagame alikua kajipanga zaidi hivyo baada ya kushinda vita naye akalipiza kisasi akawachinja hao wahutu wakakimbilia DRC ambapo aliwafuata na kuwateketeza na tokea hapo nguvu ikahama kutoka kwa Wahutu ikaja kwa watutsi na imekua hivyo mpaka leo.

Wahutu sio kwamba wali-fight for nothing" ila walishashinda vita tokea 1959 na wakajikomboa kutoka mikono ya watutsi so walienjoy uhuru wao mpaka 1990 ambapo uvamizi wa Watutsi ulianza. Hivyo ile vita ilikua ni ya kujilinda zaidi dhidi ya uvamizi wa watutsi na sio kuvamia watutsi kama unavyodhani. Yaani kama watutsi wasingetishia kuvamia Rwanda kulikua hakuna haja ya wao kuwaua maana madaraka yalikua kwa wahutu.

Hope umepata picha mkuu
 
Amini kwamba.
Kuna raia humu wana roho mbaya, wanamshawishi baba yetu Bossless ahamishe stori kwenye kitabu

wanatamani stori ingekuwa yao wangetuhamisha watsap kwa kiingilio cha elfu 2
Mungu akaliona hilo ndo maana stori kampa mzee wetu

Ajabu watakopi na kuhamishia FB, ista na watsap, watajifanya wao ndio mzee Bossless na watawachangisha wenzao pesa ya kiingilio ili kupata stori


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...................... 49k viewers si mchezo.

Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....

Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.

Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.

Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.

Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.

Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .

Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.

Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.

Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.

Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...


Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.

Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.

Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................

Itaendelea...........................................

Sent using Jamii Forums mobile app
"toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]badala ya kusikitika nmecheka
 
JK ana mazuri yake na mabaya yake. JPM pia hivyo hivyo. Kuna kitu kinachotakiwa kufanyika kwenye Taifa hili sio hadi tuuane kama wakenya

Sent using Jamii Forums mobile app


Baya n baya tuu ndugu hata ulipake rangi gan bado litakugharimu japo mistake alioifanya n kuruhusu kila kitu kiende kwa kila mtu anavyotaka Sasa lazima utengeneze makundi mawili makubwa wenye nguvu na Mali vs wenye nguvu na hawana Mali na Kama unavyojua pesa huwapi kwa wachache Sasa Hawa wengi walishaanza kuingia road mdogo mdogo rejea wanasiasa wa 2012 - 2015, rejea wale madogo Mara daa Mara MWANZA Kule Arusha nako.

Hapo ndo utajua ukiwa rais n mwiko kuruhusu Uhuru wa vitu flan hv Tena kwa nchi Kama Tanzania ilivyo
 
Unarudi kufanya nini?

Anzisha na wewe uzi wako tutakuja kusoma.hii tabia ya kuanzisha stori ndani ya stori ni ya kiboya sana.
Baada ya Berlin Conference 1884 Mjerumani alipewa Rwanda ila baada ta WWI mbelgiji aliichukua territory hio

Ukisoma zaidi Wikipedia kuhusu source/background ya genocide......
The colonists favoured the Tutsi over the Hutu when assigning administrative roles, believing them to be migrants from Ethiopia and racially superior.[30] The Rwandan king welcomed the Germans, using their military strength to widen his rule.[31] Belgian forces took control of Rwanda and Burundi during World War I,[32] and from 1926 began a policy of more direct colonial rule.[33][34] The Belgians modernised the Rwandan economy, but Tutsi supremacy remained, leaving the Hutu disenfranchised.[35] In 1935, Belgium introduced identity cards labelling each individual as either Tutsi, Hutu, Twa or Naturalised. While it had previously been possible for particularly wealthy Hutus to become honorary Tutsis, the identity cards prevented any further movement between the groups.[36]

Js imagine eti ukiwa na hela na we ni mhutu unaweza nunua ID card ya mtutsi ushenzy kabisa na hio ni 1935 miaka 60 kabla ya mauaji

ntarudi....
 
Ndio maana PK anaogopa kuachia ngazi kwani anajua fika kitanuka
Kama una sura ya kitutsi, utakuwa bonge la lady[emoji39], samahani nimeingilia uzi wa majonzi. Ilà kwa kweli hawa watu sidhani kama yameisha, PK akiondoka tu tunaweza kushuhudia mengine. Just imagine in 90 days wamekufa kwa risasi na mapanga watu karibia 1mill, Nani alipandikiza huo uovu, nani alitoa pesa za kufadhili uovu, nani alimwaga silaha? Mtu mke na mume wanachapana mapanga, wakimaliza wanawachapa watoto mapanga WTF kilichoingia kwenye vichwa vyao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachoshangaza kabisa hakuna kabila linaloitwa watusi au kabila linaloitwa wahutu yaani hawa watu wanaongea Lugha Moja ila tofauti yao ni Races tu basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unanichanganya mkuu.inamana gani kusema hakuna kabila ya tusi na hutu? Sasa waliokuwa wanaopigana ni kabila gani vs kabila gani.maana tumesikia ni Vita ya wahutu na watusi.
 
Unatambuaje kuwa huyu kabila hii huyu kabila hii?
Hawa wanyarwanda lazima wakinukishe Tena

Huwa nikitazama rwanda TV na tv 10 naona watangazaji wote watutsi sijawahi ona.mhutu

Just imagine huko serikalini kupoje

Kosa walilofanya wahutu ndio watutsi Sasa wanalifanya



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge la ushauri, huto balozi nimemsaka hata kwa google hakuna info zake.
Amenivutia sana kumfahamu
JF ni taasisi kubwa sana kwa hivi sasa.
Nashauri huyo Balozi leo afahamike jina na Picha yake,apewe heshma kubwa leo kwakuwa ni siku ya wanawake Duniani.Ana kila sababu ya kukumbukwa na kutambulika kwa ushupavu wake.
Mleta habari umenisisimua sana,siwezi kuelezea.Kipindi hicho tulikuwa JKT kwa mujibu wa sheria 841 kj.Tulikuwa tunaambiwa tutapelekwa huko (redio mbao) kutuliza hali ya mambo.So imenikumbusha Mbali sana.
Cc Bossless
Cc Maxence Melo
Cc Asha D Abinallah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom