Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini


Kuna maelezo mengi uliyotoa ya kinadharia. Balozi wa Usuluhishi alikuwa anamsuluhisha nani huko Kigali? Mapatano yalikuwa yanafanyikia Tanzania iwapo kulikuwa na msuluhishi he/she alitakiwa kuwepo Tanzania wakati vita vinaanza. Kumbuka kuangushwa kwa Marais wawili wakitokea Tanzania ndio ulikuwa mwanzo wa genocide.

Pia Tanzania haikufunga mpaka isipokuwa iliongeza ulinzi mpakani ili Watutsi na Moderate hutu watakaovuka wasifuatwe kuuliwa. Yoyote aliyevuka daraja alipokelewa na kuhifadhiwa. Nchi ingefunga mipaka wale wanyarwanda wasingepona wangeishia mtoni wote.

Yale magenge yalikuwa yanaongozwa na viongozi sio laymen. Na wala si convoy ya Tanzania pekee ambayo haikushambuliwa hata za mataifa mengine pia. Genocide ilikuwa systematic na sio random. Haikuparamia tu watu na magenge yalikuwa yanaact on orders sio kujiongoza tu kama wendawazimu.

Kuhusu wauaji kujaribu kuvamia Ubalozi na kisha kuacha inatakiwa uelewe kitu kimoja. Si Ubalozi wa Tanzania pekee ambao Watutsi walikimbilia, Watutsi walikwenda mahala popote ambapo walihisi palikuwa salama na sehemu pekee ambazo Wauwaji waliogopa kwenda zilikuwa sehemu zenye wageni (si Watanzania pekee). Na walifanya hivyo kuavoid international provocation ambayo ingepelekea nchi nyingine zinunue ugomvi iwapo raia wao wangedhuliwa.

Swala la msingi ukitaka kuelewa survival ilikuwaje jiulize trucks za Tanzania na madereva walirudije?
 
Watu kama nyinyi ni vigumu kuelewa huyo alikuwa barozi wa kimikakati kutokana na hali ya mambo Rwanda kwenye hiyo miaka na jukumu la tz kuwa mpatanishi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu usiishie tu kusema alikuwa ni balozi wa kimkakati na badala yake eleza kama alikuwa balozi wa kimkakati basi asingeweza kuwa na ofisi pale Kigali, ofisi yake isingeweza kuwa na staff wengine akiwemo msimuliaji, asingeweza ku accomodate watu ubalozini kwake kama alivyofanya kwa wale waliokimbilia pale au kuwaondoa watu waliokuwa ubalozini na kuondoka nao kuelekea mpakani kama ilivyosimuliwa?

Kwenye nyaraka hapo juu imeonyesha kwamba alikuwa ni balozi na wewe unadai alikuwa balozi wa mkakati, na kuna mchangiaji mmoja amedai huyo mama aliteuliwa na Mzee Mwinyi kwenda kuwa balozi na baadae kabla ya genocide akaondolewa, wewe unadai hakuwa balozi ila alikuwa ni balozi wa kimkakati. Sasa kwa vile sisi wote tunaokoteza okoteza tu vipande ya habari ili kujiridhisha basi na wewe njoo na ushahidi wako usio na shaka kwamba huyo mama hakuwa balozi bali alikuwa ni balozi wa kimkakati kama unavyolazimisha aitwe.
 
Duh! Tz noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi darasa la saba umefika kweli !!? Maana inaonyesha ujui hata kazi za balozi na vipi anahusika kwenye usuluhishi pale nchi yake inapo husika kwenye usuluhishi
Moja ya kazi yake nikuangalia kile kinacho endelea kwenye nchi yenye mzozo na kuleta taharifa sahihi kwa tume ya usuluhishi,sina muda wa kupoteza kwa kuelimisha mbumbumbu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuwa balozi ila alikuwa balozi wa kimkakati ndiyo kusema nini !!!! ??
Mfano msemo huu ..... "Uchumi na uchumi wa kimkakati "kisha useme uchumi wa kimkakati siyo uchumi ? Sasa balozi wa kimkakati ni balozi kamili kama mabalozi wengine ila yeye huwa na kazi special zaidi ni kama unaposikia special force au askari na askari komando ..wote ni askari ila komando ni special

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lenu amjui neno mkakati mnali underestimat balozi wa kimkakati ni balozi kama wengine ila yeye anafanya kazi special zaidi ya wengine huyu wa kimikakati anakuwa more special kutokana na kusudi la kimikakati ndiyo maana ulikikia alikuwa hadi na radio call pia anaweza kuwa na ulinzi hata wa makomando na siraha za vita na vifaa vya kivita kutokana na uitaji wa kimikakati kwaiyo kudhani balozi wa kimikakati atakiwi kuwa na ofsi ya ubalozi sijui mnatowa wapi hiyo kitu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilishasema mwanzoni website ina walakini. Wengine wamo, wengine hawamo, wengine waliwakilisha nchi mbalimbali na haioneshi, ila aliyeandika ndio kaandika alivyotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya mkuu. Nikubaliane na wewe kwamba huyo balozi hakuwa Dorah Mbezi. Tupe jina la huyo balozi wako wa kimikakati ili tusonge mbele. Maana hata haueleweki uko upande gani.
 
Wewe jamaa ni mpuuzi lakini unajiona unajua. Hujui kilitokea nini Rwanda unaleta theory zako.

Jifunze kwanza timing of events za Rwanda ndio ulete upupu hapa. Msuluhishi na mpatanishi wakati vita inaanza alikuwa Tanzania. Vita vilianzishwa na waliobaki immediately baada ya kupata taarifa za kikichojiri kwenye usuluhishi. Hata Marais wa Rwanda na Burundi na delegetions zao hawakukanyaga ardhi ya Rwanda vita ilipoanza. Balozi wako alirudi vipi immediately?

Nimeuliza pia swali jepesi, trucks zilirudi vipi? Ukipata jibu husika linganisha na visa vya hii story.
Kukusaidia tu official records zinaonesha evacuation ya wanadiplomasia na watumishi wa mataifa mbalimbali waliondoshwa na kulindwa na Wafaransa.
 
Mwenyewe huyuu kutoka Rwandaa
Ndugu andika kwa kiswahili basiiii
 
Defender wale walikua masoja wetu mzigoni, na base yao mpakani. Huku ndani Rwanda walikua wanaingia sana ila ni kuchungulia tu raia wao wako salama then wanarudi kule.
Hamna kuingilia vita ilikua ya kikabila.
Na vikabila vyenyewe viwili so waache wachapane.
Ila pale unaposogeza mambo hayo pale mpakani,
then na wao ndo wanawatekenya kidogo ili mmalizane huko huko.
Lakini asikwambie mtu watusi wengi sanaa na wahutu pia raia waliokolewa bila pingamizi na mpaka kesho wanaiheshimu sana nchi yetu.
Ilikua ukifika mpakani silaha zako tupa huko,jisalimishe huku karibu,unatibiwa unapewa camp ya kukaa, couporn ya msosi na nguo.
Wale waliouliwa na jamaa wa difenda ni hutu militia,
hawakukubali kuona tutsi wanavuka salama wakataka kuvuka daraja pale na silaha wawafanyizie ndio wakachezea za uso na zile njemba saba.
Mleta mada kaeleza vizuri huko kati jinsi vumbi lilivyotimka pale darajani na zile njemba saba zikapotea zikarudi salimini pale pale mpakani na vumbi kibao.
Ina maana mziki ulipoanza wale militia walizama machakani huko ndio mashujaa wetu wakaona hatuwaachi.
Kumbuka kuna lile vagi jamaa katweleza waliloleta pale ubalozini.
Kwa hiyo pale mpakani walikipata wanachotafuta.
 
Tatizo ni lugha mkuu
 
Kaka mkubwa, naomba nikuulize jambo, kwani unataka atokee wapi ili ukubali kwamba ndio yeye ? Au unaposema hatokei, hatokei wapi ?

Maana nimeona kuna mdau ameleta maelezo ya Kinyarwanda hapa yakimtaja nz kuna mdau ametuwekea kwa Kiswahili. Hivi kaka kuna ushahidi mkubwa kuliko mtu au watu kujishuhudilia wenyewe ? Jibu hakuna ushahidi kuzidi huo, namaanisha wenyewe Wanyarwanda katika maandiko yao wamemtaja.
 
Unaona akili yako ilivyo mbovu usuluhishi aufanyi na MTU mmoja tu ila anaweza akachaguliwa mmoja kuwa kichwa cha suluu huyo barozi alikuwa ni sehemu ya timu ya suluu acha ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaona akili yako ilivyo mbovu usuluhishi aufanyi na MTU mmoja tu ila anaweza akachaguliwa mmoja kuwa kichwa cha suluu huyo barozi alikuwa ni sehemu ya timu ya suluu acha ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Na aliyekuwa kapewa jukumu na OAU la kuwa msuluhishi mkuu kwenye mgogoro huo alikuwa ni rais mstaafu Ally H. Mwinyi ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ndiye rais wa Tanzania.
 
Unaona akili yako ilivyo mbovu usuluhishi aufanyi na MTU mmoja tu ila anaweza akachaguliwa mmoja kuwa kichwa cha suluu huyo barozi alikuwa ni sehemu ya timu ya suluu acha ujinga

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe jamaa kweli ni kiazi. Nimeandika wapi usuluhishi unafanywa na mtu mmoja. Tatizo lako huna unachojua kuhusu kilichotokea Rwanda. Unajificha kwenye kujua majukumu ya Balozi kwa ujumla wake.
 

Bora umemsaidia. Maana alihisi hakuna role tuliyoplay kuokoa raia wetu. Na hatua zisingechukuliwa asingevuka mtu pale darajani. Ni parefu na pembamba, militia wangekaa upande wa pili hakuna mtu angevuka pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…