Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
- kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
- mengineyo .


Stay turn............................


Sent using Jamii Forums mobile app

Pamoja sana mkuu Bossless
 
Balozi afanyi kazi kama official undercover agent ata kama anashiriki kwenye covert mission zingine za nchi yake.

Ndio maana anatambulishwa rasmi kama kuna majukumu mengine ya siri ni yeye, washirika wake walio undercover na serikari iliyomtuma.

Ubalozi wenyewe wa Rwanda nchini Tanzania umefunguliwa kwa mara ya kwanza 2009 na Tanzania sidhani kama kulikuwa na ubalozi Rwanda prior to 2000’s tangia uhuru wake (those understandings are open for correction if others know otherwise)
Kitendawili kimeshateguka chief, balozi alikuwepo na alisimamia mchongo mzima wa negotiations.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi huyo mpenzie hakuwa mhutu kweli? Maana kulingana na simulizi yake baada ya watutsi kuchukua nchi na kuanzisha mahakama zao huyo binti na familia yake walilazimika kuhama makazi yao kwa kuhofia kufanyiziwa na watutsi ambao sasa ndiyo walikuwa wenye kula mema ya nchi. Labda kama sikuelewa vizuri.
kama nimemuelewa amesema kwenye ile mahakma watu wengine walikuwa wanatajana tu kwa kisasi, mtu anaweza taja hata mtutsi mwenzie kwamba aliwasaidia hao ntarahamwe na ukitajwa haijalishi wewe ni mtutsi au hutu ni hukumu tu na hakuna wa kufatillia kama ni kweli au unasingiziwa
 
Kuna maelezo mengi uliyotoa ya kinadharia. Balozi wa Usuluhishi alikuwa anamsuluhisha nani huko Kigali? Mapatano yalikuwa yanafanyikia Tanzania iwapo kulikuwa na msuluhishi he/she alitakiwa kuwepo Tanzania wakati vita vinaanza. Kumbuka kuangushwa kwa Marais wawili wakitokea Tanzania ndio ulikuwa mwanzo wa genocide.

Pia Tanzania haikufunga mpaka isipokuwa iliongeza ulinzi mpakani ili Watutsi na Moderate hutu watakaovuka wasifuatwe kuuliwa. Yoyote aliyevuka daraja alipokelewa na kuhifadhiwa. Nchi ingefunga mipaka wale wanyarwanda wasingepona wangeishia mtoni wote.

Yale magenge yalikuwa yanaongozwa na viongozi sio laymen. Na wala si convoy ya Tanzania pekee ambayo haikushambuliwa hata za mataifa mengine pia. Genocide ilikuwa systematic na sio random. Haikuparamia tu watu na magenge yalikuwa yanaact on orders sio kujiongoza tu kama wendawazimu.

Kuhusu wauaji kujaribu kuvamia Ubalozi na kisha kuacha inatakiwa uelewe kitu kimoja. Si Ubalozi wa Tanzania pekee ambao Watutsi walikimbilia, Watutsi walikwenda mahala popote ambapo walihisi palikuwa salama na sehemu pekee ambazo Wauwaji waliogopa kwenda zilikuwa sehemu zenye wageni (si Watanzania pekee). Na walifanya hivyo kuavoid international provocation ambayo ingepelekea nchi nyingine zinunue ugomvi iwapo raia wao wangedhuliwa.

Swala la msingi ukitaka kuelewa survival ilikuwaje jiulize trucks za Tanzania na madereva walirudije?
Nakumbuka msimuliaji alisema vita ya kuuana kwa hayo makabila ilikua ya siri kwa siku 70 na baada kifo cha maraisi ndio dunia ikashtuka na hapo pia wahutu wakapata hofu baada ya kiongozi wao kufa kuuana kukapungua, kwa hiyo mauaji yalikolea kabla raisi hajauwawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom