Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

You have nailed it. Huyu jamaa anataka ushahidi utoke mbinguni ndo aamini...hata ushahidi ukitoka anakotaka utoke bado atasema haujatoka anakotaka utoke.
 
You have nailed it. Huyu jamaa anataka ushahidi utoke mbinguni ndo aamini...hata ushahidi ukitoka anakotaka utoke bado atasema haujatoka anakotaka utoke.
Nilishauliza huko nyuma kuna mabalozi wa aina mbili huyo mama yupo kundi gani?

1. Ambassador ‘extraordinary and plenipotentiary’ hawa ndio wale kilasiku tunaona wanaapishwa na kupangiwa nchi za kwenda.

2. Ambassador ‘Charge D’affaires’ hawa wanateuliwa temporarily kutoka wizarani kuwakilisha taifa lao pale ambapo serikari yao inahitaji ushiriki kamili kwenye maswala ya nchi nyingine ambayo hawana ubalozi (kama vile Tanzania ilivyokuwa sehemu ya kutatua mgogoro Rwanda).

Sasa kwakuwa atukuwa na ubalozi Rwanda kabla ya 2000 liko wazi huyo mama alikuwa ni balozi wa aina gani.
 
Huyo wa pili bila shaka ni kama huyu au sio kiongozi
[emoji116][emoji116]
Chargé d'Affaires Inmi Patterson | U.S. Embassy in Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ni nani mpaka nipinge maneno yako?
 
Wewe jamaa kweli ni kiazi. Nimeandika wapi usuluhishi unafanywa na mtu mmoja. Tatizo lako huna unachojua kuhusu kilichotokea Rwanda. Unajificha kwenye kujua majukumu ya Balozi kwa ujumla wake.
Si wewe umesema kama huyo balozi alikuwa usuluhishi kwanini alikuwa Rwanda badala ya Tanzania ...au umesahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ali Hassan Mwinyi yumo? Pia alikuwa balozi. Website ina walakini hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si wewe umesema kama huyo balozi alikuwa usuluhishi kwanini alikuwa Rwanda badala ya Tanzania ...au umesahau

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesema Tanzania ilikuwa msuluhishi. Kwa role nchi iliyoplay Balozi kama mdau muhimu wa Tanzania asingekuwepo Rwanda wakati wa Makubaliano ya Amani ya Arusha
 
Watu walishaandika long ago mzee kaka... Even more than this.
Tafuta hiki kitabu.

Shake Hands with the Devil... By LT. GENERAL DALLAIRE ROMEO..

true storyyy... Hii ya mzee inasubiri
 
Dahh... Story ndani ya story... Mkuu embu tafuta muda iweke vizuri hii..
 
HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
  • kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
  • mengineyo .


Stay turn............................


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu badala ya kuongea haya si ungetipa Hata mwendelezo. Naomba type mwendelezo sasa hivi ili tuendelee kujifunza. Umetuweka weeee tukajua Hata wikiendi utakuja kutufariji. Tupe faraja wenzio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama nyinyi ni vigumu kuelewa huyo alikuwa barozi wa kimikakati kutokana na hali ya mambo Rwanda kwenye hiyo miaka na jukumu la tz kuwa mpatanishi

Sent using Jamii Forums mobile app
00⁰⁰⁰
Sawa mzee baba Bossless take your time ukiwa umetulia endelea wacha kwanza sisi tuendelee kubishana ila kifupi tumeshalipata jina la yule balozi wetu nadhan kwa sasa yupo Tabora Mungu ni mwema aendelee kumpigania
 
Hali kumbe ilikuwa mbaya kuliko tunavyoambiwa, huu ni ushuhuda wa mtu mmoja tu tena akiwa safarini kuokoa maisha yake. Pata picha nchi nzima ya Rwanda hali ilikuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu walishaandika long ago mzee kaka... Even more than this.
Tafuta hiki kitabu.

Shake Hands with the Devil... By LT. GENERAL DALLAIRE ROMEO..

true storyyy... Hii ya mzee inasubiri
Kitambo kidogo kuna shuhuda wa vita hii alikuwa anasimulia kule Clouds, anasema yeye alikuwa dereva wa semi na hiyo vita ilimkuta akiwa ndani ya Rwanda. Alielezea mambo mengi sana ya kutisha aliyoyashududia wakati wa kadhia hiyo.

Nakumbuka kuna kisa alisimulia wakati akiwa kwenye harakati za kukimbia jamaa walikuwa wanapiga sana risasi kwenye gari yake. Jamaa anasema yeye hakusimama aliendelea kupiga mashine pasipo kutazama nyuma huku jamaa wanaendelea kupiga risasi nyingi hasa za kwenye matairi nazani walitaka asimame wapore mzigo aliokuwa kabeba.

Jamaa hakusimama anasema kilichompa jeuri ya kutokusimama hiyo gari yake ilikuwa ya kisasa kabisa isiyopenyesha hata chembe ya risasi (bullet proof) na ilikuwa na uwezo wa kujijaza upepo wa matairi yenyewe huku ikiwa stable na kwenye mwendo mkali. Kwaiyo jamaa walivokuwa wanapiga risasi za matairi wakifikiri tairi zitapasuka na gari kusimama au jamaa atayumba na kuingiza gari mtaroni, jamaa anakuambia gari ilikuwa inatingishika tu huku tairi zinajijaza juukwajuu na mileage zinaendea kusoma kama kawaida, gari ya mzungu hii (shikamoo mzungu).

Kwenye ishu ingine anasema akiwa katikati ya mapori huko anachapa mwendo alishtuka kwa mshangao mkubwa kuwaona masista (ndio masista hawahawa wa kanisani) walikuwa wanakimbia vita nao. Hawa masista waliibuka kutoka vichakani wakiwa katika hali mbaya sana na anasema kulikuwa na kila dalili walikuwa tayari wameshafanyiwa ndivo sivyo, jamaa akawasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama vipi tutembeze bakuli ili upate simu mpya kabisa maana wewe ni mpambanaji uliewakabiri kiakili kikundi cha Interahamwe pindi mlivyotoka disco na yule mama mdogo wetu wa kitutsi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama vipi tutembeze bakuli ili upate simu mpya kabisa maana wewe ni mpambanaji uliewakabiri kiakili kikundi cha Interahamwe pindi mlivyotoka disco na yule mama mdogo wetu wa kitutsi

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi huyo mpenzie hakuwa mhutu kweli? Maana kulingana na simulizi yake baada ya watutsi kuchukua nchi na kuanzisha mahakama zao huyo binti na familia yake walilazimika kuhama makazi yao kwa kuhofia kufanyiziwa na watutsi ambao sasa ndiyo walikuwa wenye kula mema ya nchi. Labda kama sikuelewa vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…