Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Kaka mkubwa, naomba nikuulize jambo, kwani unataka atokee wapi ili ukubali kwamba ndio yeye ? Au unaposema hatokei, hatokei wapi ?

Maana nimeona kuna mdau ameleta maelezo ya Kinyarwanda hapa yakimtaja nz kuna mdau ametuwekea kwa Kiswahili. Hivi kaka kuna ushahidi mkubwa kuliko mtu au watu kujishuhudilia wenyewe ? Jibu hakuna ushahidi kuzidi huo, namaanisha wenyewe Wanyarwanda katika maandiko yao wamemtaja.
You have nailed it. Huyu jamaa anataka ushahidi utoke mbinguni ndo aamini...hata ushahidi ukitoka anakotaka utoke bado atasema haujatoka anakotaka utoke.
 
You have nailed it. Huyu jamaa anataka ushahidi utoke mbinguni ndo aamini...hata ushahidi ukitoka anakotaka utoke bado atasema haujatoka anakotaka utoke.
Nilishauliza huko nyuma kuna mabalozi wa aina mbili huyo mama yupo kundi gani?

1. Ambassador ‘extraordinary and plenipotentiary’ hawa ndio wale kilasiku tunaona wanaapishwa na kupangiwa nchi za kwenda.

2. Ambassador ‘Charge D’affaires’ hawa wanateuliwa temporarily kutoka wizarani kuwakilisha taifa lao pale ambapo serikari yao inahitaji ushiriki kamili kwenye maswala ya nchi nyingine ambayo hawana ubalozi (kama vile Tanzania ilivyokuwa sehemu ya kutatua mgogoro Rwanda).

Sasa kwakuwa atukuwa na ubalozi Rwanda kabla ya 2000 liko wazi huyo mama alikuwa ni balozi wa aina gani.
 
Huyo wa pili bila shaka ni kama huyu au sio kiongozi
[emoji116][emoji116]
Chargé d'Affaires Inmi Patterson | U.S. Embassy in Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm ni nani mpaka nipinge maneno yako?
Nilishauliza huko nyuma kuna mabalozi wa aina mbili huyo mama yupo kundi gani?

1. Ambassador ‘extraordinary and plenipotentiary’ hawa ndio wale kilasiku tunaona wanaapishwa na kupangiwa nchi za kwenda.

2. Ambassador ‘Charge D’affaires’ hawa wanateuliwa temporarily kutoka wizarani kuwakilisha taifa lao pale ambapo serikari yao inahitaji ushiriki kamili kwenye maswala ya nchi nyingine ambayo hawana ubalozi (kama vile Tanzania ilivyokuwa sehemu ya kutatua mgogoro Rwanda).

Sasa kwakuwa atukuwa na ubalozi Rwanda kabla ya 2000 liko wazi huyo mama alikuwa ni balozi wa aina gani.
 
Wewe jamaa kweli ni kiazi. Nimeandika wapi usuluhishi unafanywa na mtu mmoja. Tatizo lako huna unachojua kuhusu kilichotokea Rwanda. Unajificha kwenye kujua majukumu ya Balozi kwa ujumla wake.
Si wewe umesema kama huyo balozi alikuwa usuluhishi kwanini alikuwa Rwanda badala ya Tanzania ...au umesahau

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1387360

Hiko ndicho kinachotokea kwenye hiyo website ya serikari wewe weka jina la balozi wanakuletea na vituo vyake vyote vya kazi.

Mbago alikuwa Russia tu ajafanya kazi sehemu nyingine; unless as a special envoy baadae kama huyo mama inavyoonekana na sidhani kama wamejumuisha hao.
Ali Hassan Mwinyi yumo? Pia alikuwa balozi. Website ina walakini hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji857][emoji857][emoji857] Bado naiona pesa kwenye hii thread.. Mkuu Mungu akijalia uzima .. Na mipango ikampendeza, na mwisho kama wewe hautojali siku moja nitakutafuta.. Unless uwe haupo interested.. Tu make hii kitu iende Amazon.. Naamini kabisa pesa ipo hapa.. Trust me or not [emoji857][emoji857][emoji857]

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu walishaandika long ago mzee kaka... Even more than this.
Tafuta hiki kitabu.

Shake Hands with the Devil... By LT. GENERAL DALLAIRE ROMEO..

true storyyy... Hii ya mzee inasubiri
 
Ni hivi...Laurent Desiré Kabila Sr alikua ni loverboy au tuseme player kwani alikua na wake official 13 na watoto zaidi ya 25.. alikua na wanawake kila kona ya nchi hizi za africa mashariki na kati..Kama muasi wa serikali halali ya Mobutu aliishi maisha ya kujificha katika misitu ya Congo, muda mwingine alikua Uganda, ku kipind alikua Tanzania Lake Tanganyika na kwingineko hii yote ni kuukwepa mkono wa chuma wa dikteta Mobutu Sseseko..maisha yake yalikua ya ki guerrilla warfare akistage attacks toka msituni huku akiomba msaada toka nchi jiran za Tanzania, Uganda rwanda na Burundi. Kwa hiyo katika harakati hizi alikua akizaa hovyo na wanawake kila anapokwenda.

Idadi halisi ya watoto wake haijulikani na idadi halisi ya wake zake haijulikani pia. Na hadi anakua Rais wa DRC 1998-2001 hakua na mke mmoja rasmi. Hakuwah kuwa na first lady wala hakuwajali kabisa watoto wake. Inasemekana Joseph Kabila ni mtoto wake aliyempata alipokuwa Tanzania wengine wanasema ni mtoto wa rafiki yake wa Kitutsi aliyezaliwa south Kivu Congo mashariki.

Baba yake halisi Kabila, mzee Kanambe alikua rafiki wa Kabila na walikuwa pamoja kama waasi wa AFDL dhidi ya serikali ya Mobutu. Alipofariki vitani Kabila anamchukua Joseph Kabila ( Jina lake halisi Hipolite Kanambe) na kumlea kama mwanae. Asili ya Joseph kabila ni debatable ila kwa mwonekano wake wa uso na pua ana asili ya Kitutsi na hafanani kabisa na Laurent Kabila.

Tunachojua for fact ni kwamba Joseph Kabila Jr kakulia Tanzania, Kasoma Shule ya Msingi Msasani Dar es salaam, sekondari kasoma hapa hapa Tanzania, chuo kikuu kasoma Makerere Uganda na katika kutafuta maisha amewah kuwa dereva taxi Dar es salaam, baadae akaelekea Rwanda na Congo kuungana na majeshi ya baba yake ya AFDL pamoja na RPF akiwa kama commander of the 'kadogos'( child soldiers) mpaka alipokuja kurithi mikoba ya baba yake mwaka 2001 kama rais wa DRC akiwa na umri mdogo tu wa miaka 29.

Pichani chini ni Baba yake mzazi Joseph Kabila, Adrien Kanambe, wa mwisho Kulia akiwa na Laurent Kabila katikati wa tatu toka kulia, hapa walikua msituni Congo mashariki wakiongoza vikosi vya waasi dhidi ya serikali ya Mobutu Sseseko.
View attachment 1384412
View attachment 1384468View attachment 1384470View attachment 1384473
Dahh... Story ndani ya story... Mkuu embu tafuta muda iweke vizuri hii..
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.

Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Muendelezo bonyea link hizi.

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano

Sehemu ya sita
Sehemu ya saba

Sehemu ya nane
Sehemu ya tisa

Sehemu ya kumi
Sehemu ya kumi na moja

Sent using Jamii Forums mobile app
HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
  • kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
  • mengineyo .

Stay turn............................

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
- kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
- mengineyo .

Stay turn............................

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu badala ya kuongea haya si ungetipa Hata mwendelezo. Naomba type mwendelezo sasa hivi ili tuendelee kujifunza. Umetuweka weeee tukajua Hata wikiendi utakuja kutufariji. Tupe faraja wenzio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu kama nyinyi ni vigumu kuelewa huyo alikuwa barozi wa kimikakati kutokana na hali ya mambo Rwanda kwenye hiyo miaka na jukumu la tz kuwa mpatanishi

Sent using Jamii Forums mobile app
00⁰⁰⁰
HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
- kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
- mengineyo .

Stay turn............................

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mzee baba Bossless take your time ukiwa umetulia endelea wacha kwanza sisi tuendelee kubishana ila kifupi tumeshalipata jina la yule balozi wetu nadhan kwa sasa yupo Tabora Mungu ni mwema aendelee kumpigania
 
Hali kumbe ilikuwa mbaya kuliko tunavyoambiwa, huu ni ushuhuda wa mtu mmoja tu tena akiwa safarini kuokoa maisha yake. Pata picha nchi nzima ya Rwanda hali ilikuwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu walishaandika long ago mzee kaka... Even more than this.
Tafuta hiki kitabu.

Shake Hands with the Devil... By LT. GENERAL DALLAIRE ROMEO..

true storyyy... Hii ya mzee inasubiri
Kitambo kidogo kuna shuhuda wa vita hii alikuwa anasimulia kule Clouds, anasema yeye alikuwa dereva wa semi na hiyo vita ilimkuta akiwa ndani ya Rwanda. Alielezea mambo mengi sana ya kutisha aliyoyashududia wakati wa kadhia hiyo.

Nakumbuka kuna kisa alisimulia wakati akiwa kwenye harakati za kukimbia jamaa walikuwa wanapiga sana risasi kwenye gari yake. Jamaa anasema yeye hakusimama aliendelea kupiga mashine pasipo kutazama nyuma huku jamaa wanaendelea kupiga risasi nyingi hasa za kwenye matairi nazani walitaka asimame wapore mzigo aliokuwa kabeba.

Jamaa hakusimama anasema kilichompa jeuri ya kutokusimama hiyo gari yake ilikuwa ya kisasa kabisa isiyopenyesha hata chembe ya risasi (bullet proof) na ilikuwa na uwezo wa kujijaza upepo wa matairi yenyewe huku ikiwa stable na kwenye mwendo mkali. Kwaiyo jamaa walivokuwa wanapiga risasi za matairi wakifikiri tairi zitapasuka na gari kusimama au jamaa atayumba na kuingiza gari mtaroni, jamaa anakuambia gari ilikuwa inatingishika tu huku tairi zinajijaza juukwajuu na mileage zinaendea kusoma kama kawaida, gari ya mzungu hii (shikamoo mzungu).

Kwenye ishu ingine anasema akiwa katikati ya mapori huko anachapa mwendo alishtuka kwa mshangao mkubwa kuwaona masista (ndio masista hawahawa wa kanisani) walikuwa wanakimbia vita nao. Hawa masista waliibuka kutoka vichakani wakiwa katika hali mbaya sana na anasema kulikuwa na kila dalili walikuwa tayari wameshafanyiwa ndivo sivyo, jamaa akawasaidia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HABARI ZA MASIKU WANDUGU ,NATUMAINI HAMJAMBO NA MNAENDELEA VYEMA NA MAJUKUMU YENU YA KILA ,BILA SHAKA NIMEPITIA COMMENTS ZENU NA KUFURAHISHWA NA JINSI MNAVYOJARIBU KUUTAFUTA UKWELI WA JAMBO, WACHACHE WANAAMINI NI STORI YA KUTUNGA ILA NIWADHIBITISHIE HII NI KWELI KABISA BILA KUTIA SHAKA ,WENGINE MMEKUWA MKINILAUMU KWA KUACHA BAADHI YA MAMBO HII NAIFANYA KWA MAKSUDI KABISA ILI NDUGU MSOMAJI UPATE KILE KILICHOKUSIDIWA LAKINI KWA MSOMAJI MAKINI UNAWEZA UKAWA UNAPATA MAJIBU KUTOKA HUMO HUMO KAMA UTAAMUA KUTULIZA AKILI NA KUUNGANISHA MATUKIO NA SIMILIZI ZINGINE ZENYE MFANANO NA HII.

NIPENDE TENA KUSEMA KUWA NA WAPANDA SANAA NA SINTOWAANGUSHA ILA NIWAOMBE MPAKA SIMU YANGU ITAKAPOKUWA TAYARI MUNGU AKIPENDA NAWEZE KWENDA KU HUKUA KWA FUNDI KESHO J3 ,SIMU YANGU NI TECNO P7 MIN TABLET SASA SCREEN T.YAKE INASUMBUA ILA ISHALLAH KESHO IKIWA TAYARI NAENDELEA NA STORY HII SASA PART 2. BILA CHENGA.

-Maisha baada ya kutua Tanzania
_kuacha kazi rasmi
- kujiingiza katika biashara vyuma chakavu nchini zambia/tanzania. Sambamba na kufungwa jera miaka3 ndola-zambia.
- mengineyo .

Stay turn............................

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kama vipi tutembeze bakuli ili upate simu mpya kabisa maana wewe ni mpambanaji uliewakabiri kiakili kikundi cha Interahamwe pindi mlivyotoka disco na yule mama mdogo wetu wa kitutsi

Hivi huyo mpenzie hakuwa mhutu kweli? Maana kulingana na simulizi yake baada ya watutsi kuchukua nchi na kuanzisha mahakama zao huyo binti na familia yake walilazimika kuhama makazi yao kwa kuhofia kufanyiziwa na watutsi ambao sasa ndiyo walikuwa wenye kula mema ya nchi. Labda kama sikuelewa vizuri.
 
Back
Top Bottom