Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Baada ya hapo nikajikuta nimeishiwa faranga ikabidi niende Nyabugogo kubadili hela ya kitanzania huku nikijiuliza kuhusu yule demu wa kinyarwanda aliyenihudumia japo lugha hatukuelewana. Nilifanikiwa kubadili na kuelekezwa ubalozini. Nilivyofika ubalozini nikaona watu wana wasiwasi hawana raha. Nikaona kila mtu akipita reception anakodolea macho picha ya raisi. Mpaka hapo nilijua neno moja la salam (mwalamse)......

mwingine aendelee mleta mada atatukuta njiani.
😀 😀 😀 😀 😀
Jf kuna watu wamepinda, eti atawakuta njiani. Na wamembembeleza amekubali, atakuja kuendeleza mlipoishia.
 
Kwanza napenda kuwashukuru wote mlionipa moyo wa kuendeleza huu ushuhuda wangu asanteni sanaa labda niwaahidi ntaendelea hiki kitu lakini niwaombe radhi kidogo mimi umri umeenda majaribia kuigiza 55 yrs sasa unaona kwa umri huu hata typing tu lazima iwe kidogo kidogo kutokana na utu uzima

Kuna watu wanajua mimi ni under18 , nipende tu kuwaambia msitukane au kushutumu msiyemjua, akatae kukobolewa pale inayobidi au napo sahau jambo lakini kutukanwa si busara hata kidogo.

Kwa machache hayo - mtaelewa maisha ya kazi ubalozini ,maisha ya uraiani,kukimbia vita na kujikuta katika vita bila kutarajia (yani kupigana vita wengine mnaweza msinielewi lakini vita nimepigana kidogo ili kupata njia ya kupita), kurudi tanzania, kuacha kazi, kuhamia Zambia- Ndola na baadae kuanza kujishughulisha na biashara ya vyuma chakavu kutoka kapiiimposhi-zambia kuuza Tunduma na dar.

Stay turn........

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwa mitihani uliyopitia najua hauwezi kubabaishwa na kelele za watu wenye kashfa hapa jukwaani, najua yale uliyoyaona maana binafsi nimetembelea sana hizo nchi Rwanda,Burundi na Congo, hakika wewe ni mwanaume unapaswa kupuuzia vitu vidogo kama hivi.

Leta stori mkuu
 
Shida ya watu wengi wanatabia ya kujiona special na wanahitaji kubembelezwa...

Anyways, hongera kwa kubadilika. Upinzani upo sehemu zote na kwa kila kitu na mtu.

Hata ukiwa mwenyewe kuna muda unakuwa unajipinga baadhi ya vitu.

Usiwe na soft heart Mkuu.
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.

Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulitaka uingie ahera!!? Kaburini utalalaa ti
 
Hapa ndio unaposikia binadamu hatuna uvumilivu, kutukanwa kidogo umekata tamaa ya kuendelea... Achana na hao wewe mwaga ushuhuda..

Ukiwa mtu wa kukata tamaa kisa wengine watasema nini au wanasema nini huwezi kufanikiwa.

Mpaka hapo ulipo umekutana na changamoto nyingi na umeshinda sasa inawezekana vipi ukate tamaa kwa maneno ya mwanaJF?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa watu wengine ile tu kushuhudia yale mauaji ya kutisha kwa macho ingetosha kabisa kuwapa ujasiri wa kuhimili vishindo vya dharau, matusi, njaa, kukatishwa tamaa n.k. Mleta mada kwa yale mauaji aliyoshuhudia hakupaswa kuwa mtu wa kukatishwa tamaa kirahisi rahisi. Ila ni maamuzi yake binafsi japo stori ilikuwa nzuri na yenye mwelekeo wa kusisimua sana.
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.

Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Sent using Jamii Forums mobile app
umeandika vizuri hili zoezi lako la kuandika riwaya umepasi.
 
Mtoa mada kutoka rusumo hadi Kigali ni km 120 na sisi wenye malori tulikuwa tunatembea massa 6 - 7,na kinachosababisha tutembee kwa muda mrefu ni milima,yaani nimilima mitupu panda shuka kila kwa gari ndogo ukizidi sana itakuwa ni masaa 3 na huo utakuwa mwendo wa konokono wakati madereva was kule wanaendesha kasi sana.
Hivyo rudisha kumbukumbu zako muda ulioutaja kwa gari ndogo sio sahihi.
Ila ni kweli Nyamirambo ndio uswahilini kama ilivyo Buyenzi kule Bujumbura.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongelea Rwanda ya mwaka gani? Tuanzie hapo? Halafu ntakujibu wakati unatoka Boda kwa miaka hiyo ya 1989 kulikuwa kuna vizuizi zaidi ya 50 kila kilometer 10 ...mnakuta barrier mnasachiwa kuanzia mabegi hadi buti ya gari. Kwa kukumbusha kipindi hicho ndo vuguvugu LA uvamizi lilikuwa limeanza kukawa kuna mashambulizi madogo madogo yapa na pale kutoka kwa waasi. Ntakupa mfano mdogo kama wewe. Ni msafiri kweli hebu niambie kutoka kasubalesa to Lubumbashi kuna berrier ngapi? Unajua kwanini? Waasi baba serikali haimini MTU tena ndivyo Rwanda ilivyokuwa miaka hiyo sasa unahisi utafika kwa hayo Masaa yako matatu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu mzee anatuangusha wazee wa rika lake!..

Hivi miaka 55 ndio sababu ya kumfanya mzee aliyekwepa mishale mingi kuondoshwa kwenye reli ya mada aliyoishuhudia kwa macho yake? tena kataka mwenyewe kutushirikisha bila ya mtu kumlazimisha... 😳 Mimi siamini utetezi wake huu, labda tatizo ni kifaa anachotumia hakina uwezo mkubwa au sio chake.

Naishauri JF au hata ndugu yetu Paschal Mayalla wainunue simulizi hii kisha ichapishwe kama makala hapa JF au majarida mengine... Hii habari ya ITAENDELEA mara sitaki tena kuendeleza simulizi ni utoto ukubwani unaopaswa kuadhibiwa na uongozi wa jukwaa hili.😡
 
Back
Top Bottom