komrade
JF-Expert Member
- Sep 26, 2019
- 207
- 262
Wanyarwanda wamesameheana na kusahau. Wewe usiyesahau yanakuhusu nini.
Ni vema ukaishia hapohapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni vema ukaishia hapohapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Angemaliza kwa muda mfupi kama anakazi za kufanya zingine jeSababu za watu kusema vibaya muda mwingine husababishwa na mleta mada Yan unaleta stori Tena wewe ndo shuhuda unaileta nusu, baadae unaanza battle na watu kwenye Uzi huohuo, humu Kuna watu wanaakili Kama maji ya Nazi ukianza kwenda nao sawa lazima utoke nje ya reli.
Pia kingine Inaonekana ulitegemea kupewa pole Mana ulivyorud kwa kunyong'onyea sio Bure.
Pia jifunze kujifunza kilasiku hyo stori yako ungeimaliza kwa muda mfupi ungewexa bada upande wapili ambao wewe ilkua uhujui hvyoungefaidika kujua vingi kupitia stori yako.
1989 inaanza Kaz we n mtu mzima sasa hvyo uvumilivu lazima unao mengi ushaona
Nilivyoamka asubuhi na hang over ya bia ya primus, kichwa kilikuwa kinagonga sana kuangalia saa ni saa nne asubuhi. Nikaoga fasta nikashuka restaurant kupata supu na kutoa lock. mwingine aendelezeNilivyofika hotelini mida si mrefu nikatoka kupata chakula, nikauliza mapokezi ntapata bia? Naam! Wakajibu zipo basi nikaa meza ya juu kabisa nikaanza kula bia.
Kesho nikaamka..mwingine aendeleze
Story tamuDah story ina mvuto, ila ndo hivyo mwendo wa episode kama Drama
Ntalifanyia kazi wazo lako. AsanteKwa umri wako mkuu, hukutakiwa kabisa kupanikishwa na vijana wasiojielewa humu JF na kuamua kuacha story!
Kuna wengine humu tunapenda kujifunza Sana haya Mambo Sasa ukifanya hivyo tunakuwa bored kinoma.
Mwaga story watu tupate kujifunza.
Nikushauri tu Kama ikiwezekana chukua pc uitype hiyo story yako halafu uitupie humu ikiwa nzima then wewe upotee, wa kupanic na watoa povu unawachunia huku wewe unajinywea alikasusu bila wasiwasi. Hupaswi kufanya ligi na usiyemjua.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes fanya mambo mkuu.
Baada ya hapo nikajikuta nimeishiwa faranga ikabidi niende Nyabugogo kubadili hela ya kitanzania huku nikijiuliza kuhusu yule demu wa kinyarwanda aliyenihudumia japo lugha hatukuelewana. Nilifanikiwa kubadili na kuelekezwa ubalozini. Nilivyofika ubalozini nikaona watu wana wasiwasi hawana raha. Nikaona kila mtu akipita reception anakodolea macho picha ya raisi. Mpaka hapo nilijua neno moja la salam (mwalamse)......Nilivyoamka asubuhi na hang over ya bia ya primus, kichwa kilikuwa kinagonga sana kuangalia saa ni saa nne asubuhi. Nikaoga fasta nikashuka restaurant kupata supu na kutoa lock. mwingine aendeleze
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.
Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.
Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.
basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..
Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.
Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.
Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.
Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.
Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .
Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.
Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .
Itaendelea...........
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza napenda kuwashukuru wote mlionipa moyo wa kuendeleza huu ushuhuda wangu asanteni sanaa labda niwaahidi ntaendelea hiki kitu lakini niwaombe radhi kidogo mimi umri umeenda majaribia kuigiza 55 yrs sasa unaona kwa umri huu hata typing tu lazima iwe kidogo kidogo kutokana na utu uzima
Kuna watu wanajua mimi ni under18 , nipende tu kuwaambia msitukane au kushutumu msiyemjua, akatae kukobolewa pale inayobidi au napo sahau jambo lakini kutukanwa si busara hata kidogo.
Kwa machache hayo - mtaelewa maisha ya kazi ubalozini ,maisha ya uraiani,kukimbia vita na kujikuta katika vita bila kutarajia (yani kupigana vita wengine mnaweza msinielewi lakini vita nimepigana kidogo ili kupata njia ya kupita), kurudi tanzania, kuacha kazi, kuhamia Zambia- Ndola na baadae kuanza kujishughulisha na biashara ya vyuma chakavu kutoka kapiiimposhi-zambia kuuza Tunduma na dar.
Stay turn........
Sent using Jamii Forums mobile app
Ishia hapo hapo!baada ya kagame kuna genocide nyingine.huijui rwanda wewe..ngoja kagame afe au apoteze madaraka kwa namna yeyote ile.tutsi watatafutana kwa tochi nakwambia.Wanyarwanda wamesameheana na kusahau. Wewe usiyesahau yanakuhusu nini.
Ni vema ukaishia hapohapo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes fanya mambo mkuu.
Mtoa mada kutoka rusumo hadi Kigali ni km 120 na sisi wenye malori tulikuwa tunatembea massa 6 - 7,na kinachosababisha tutembee kwa muda mrefu ni milima,yaani nimilima mitupu panda shuka kila kwa gari ndogo ukizidi sana itakuwa ni masaa 3 na huo utakuwa mwendo wa konokono wakati madereva was kule wanaendesha kasi sana.
Hivyo rudisha kumbukumbu zako muda ulioutaja kwa gari ndogo sio sahihi.
Ila ni kweli Nyamirambo ndio uswahilini kama ilivyo Buyenzi kule Bujumbura.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani anaendelea ?nistue niunge Juhudi za kumbembeleza!!! Story naitamani hasa!!!
Sent using Jamii Forums mobile app