LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 18,037
- 33,681
Ame edit mwanzoni alisema 1994Kasema ni 1989 ndo kaenda Rwanda sio kipibdi cha vita. Hebu mkuu kuwa na subira.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ame edit mwanzoni alisema 1994Kasema ni 1989 ndo kaenda Rwanda sio kipibdi cha vita. Hebu mkuu kuwa na subira.
Sent using Jamii Forums mobile app
Bossless,
We Muongo, ulienda mwezi WA sita hahahaha.
Vita imeanza mwezi WA nne imeisha mwezi WA Saba but wewe ulipata KAZI mwezi WA sita wakati serikali ya Rwanda imevurumishwa na Rpf na kukimbilia Gisenyi Kwa kina Haruna Niyonzima huku mapigano makali yakiendelea.
Anyways wakati unapata hiyo KAZI Rais wa Rwanda alikuwa anaitwa Nani?
Jibu huna Mpira uishie hapa.
" falsus in uno falsus in omnibus" false in one thing false in every thing.
@moderators futeni uzushi huu unachafua hadhi ya jf
Mzee unatudanganya.
Ulikumbana na mawasiliano magumu wakati umesoma chuo kikuu kwa hiyo na kiingereza hawajui hujui?
Kule mwanzo unesema unesoma chuo Kule Kule rwanda halafu wakati unaoata ajira unaenda kuripoti unasema Ni Mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi??
CHAIII HII
Sent using Jamii Forums mobile app
Manina,,,,nimescrow mpaka chini hakuna muendelezo,,,,unadhan watu ni kila mda tunapata mda wa kuingia humu!!?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni fact kabisa kwa kile nilichokishuhudia rwanda ,tatizo watu wanakuja na comments za kukatisha tamaa na matusi naona hata uvuvi kuendelea na hii kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hoteli rwanda ni movie tu ile, tulia ntaelezea mambo ambayo hujawahi kusikia popote pale hii sio hadithi ni ushuhuda wangu mwenyewe .kwa macho yangu mwenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Tag mkuu pleaseHii ni fact kabisa kwa kile nilichokishuhudia rwanda ,tatizo watu wanakuja na comments za kukatisha tamaa na matusi naona hata uvuvi kuendelea na hii kitu.
Sent using Jamii Forums mobile app
huyu LIKUD alilogwa na rafiki yake juma njembaLIKUD,
Mbona inaonekana wewe ndiye una haraka? Wengi tunafahamu kwamba vita imeanza mwezi huo wa nne hadi wa saba tena mwaka 1994.
Yeye ameanza na mwaka aliomaliza masomo ya stashahada mwaka 1989 na kupata kazi kwenye ubalozi huko Rwanda. Bado anaendelea na background hajafikia kipindi vita imeanza.
You are missedNinavyopenda story hapa nimeshawaka... leta vitu Mkuu.
Halafu hii tabia ya watu kuvamia story na kukashifu kuwa ni uongo, ya nini? Kama unaona story ni ya uongo si uachane nayo?
Ustaarabu ni jambo la msingi linalowashinda wengi, hakika.
.. Tunafuatilia mkuuHoteli rwanda ni movie tu ile, tulia ntaelezea mambo ambayo hujawahi kusikia popote pale hii sio hadithi ni ushuhuda wangu mwenyewe .kwa macho yangu mwenyewe.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mjukuu wa Mwl. Kashasha 😂😂😂You are missed
DuhHabari zenu wakubwa kwa wadogo.
Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.
Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.
basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..
Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.
Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.
Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.
Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.
Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .
Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.
Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .
Itaendelea...........
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee unatudanganya.
Ulikumbana na mawasiliano magumu wakati umesoma chuo kikuu kwa hiyo na kiingereza hawajui hujui?
Kule mwanzo unesema unesoma chuo Kule Kule rwanda halafu wakati unaoata ajira unaenda kuripoti unasema Ni Mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi??
CHAIII HII
Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahahaha!msiwe na wasi wasi wadau mimi nitaendeleza[emoji23][emoji23]
Sent from my iPhone using JamiiForums