MR KUO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 2,678
- 3,818
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inaendeleaaa...........Habari zenu wakubwa kwa wadogo.
Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.
Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.
basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..
Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.
Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.
Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.
Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.
Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .
Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.
Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .
Itaendelea...........
Sent using Jamii Forums mobile app
Wasikukatishe tamaa, huyu hakumbuki na Burundi ilikuwa bugarama unashuka mpaka masaa matatu na ni km32 tu ila hauwezi kutembea mt300 lazima ukutane na barriers. Yote hii ni sababu ya waasi kulipua madaraja na kuvamia watuUnaongelea Rwanda ya mwaka gani? Tuanzie hapo? Halafu ntakujibu wakati unatoka Boda kwa miaka hiyo ya 1989 kulikuwa kuna vizuizi zaidi ya 50 kila kilometer 10 ...mnakuta barrier mnasachiwa kuanzia mabegi hadi buti ya gari. Kwa kukumbusha kipindi hicho ndo vuguvugu LA uvamizi lilikuwa limeanza kukawa kuna mashambulizi madogo madogo yapa na pale kutoka kwa waasi. Ntakupa mfano mdogo kama wewe. Ni msafiri kweli hebu niambie kutoka kasubalesa to Lubumbashi kuna berrier ngapi? Unajua kwanini? Waasi baba serikali haimini MTU tena ndivyo Rwanda ilivyokuwa miaka hiyo sasa unahisi utafika kwa hayo Masaa yako matatu?
Sent using Jamii Forums mobile app
Hii simulizi ni nzuri ila itaisha mvua za masika mwakaniInaendeleaaa...........
Nilipoishia nikiwa IMhala hoteli najiandaa sasa namna ya kuwahi kuamka mapema kuwahi kituoni kwangu kuripoti asubuhi. Mapema tu nikaamua nikajianda safi kabisa nikaanza safari ya kuelekea kituoni kwangu, nikashudia kitu cha ajabu ambacho sikukizoea .Dar ukiamka saa kumi na moja alfajiri kwa miaka hiyo hata kwa sasa ukifika stand utakaa tu kidogo hadi saa kumi na mbili au nani nusu hivi unaweza kuwa umepata usafiri na kuondoka iwe kwa texi au daladala wanyarwanda swala la kuamka mapema hilo kwao hapana labda sijui kama wamebadilika kipindi hiki, basii mtu mzima nikawa stand barabarani nasubiri daladala huwezi amini hadi saa moja moja kamili asubuhi hakuna cha daladala wala nini nikamuuliza jirani yangu pale stand hii ukoje akaniambia mabasi yanaanza kufika saa mbili kamili au na nusu nikamuomba anionyeshe texi nipande akaniambia hakuna stand ya texi Unachotakiwa kufanya unasimama barabarani unapungua gari lolote dogo mkono itakayosimama basi hiyo ndo taxi mnaelewana bei anakupeleka, mimi nikafanya hivyo kweli nikawa nimepata usafiri tukaelewana (sikukumbuki tulikabiliana bei gani ila alipeleka hadi ubalozini getini) nilishuka nikajitambulisha kwa mlinzi akiniruhusu kuingia ndani nikaingia hadi mapokezi nikatoa barua yangu ya ajira nikapokelewa safii kabisa na watumishi wenzangu sasa hapo nikawa majihisi nipo nyumba tunaongea lugha moja tunaelewana safii mzee nikapumzishwa sebule ndogo kumsubiri balozi afike nijitambulishe ili sasa taratibu zingine zifuatwe.
Muda si mrefu balozi akafika alikuwa mwanamama mweupe kama mpemba mama mtu mzima( naomba nisilitaje jina lake) akanikaribisha tukaongea maeneo ya hapa na pale ikawa baadae akaaga nikabaki na wasaidizi wake sasa ndo nikawa nimeingia mzigoni rasmi nikiwa na mabegi yangu yote( ikumbukwe kule hotelini niliaga kuwa sirudi hivyo niliondoka na kila siku changu hadi ubalozi).
Iko hivi ubalozi wowote lazima uwe na baadhi ya vyumba vya siri na wazi hivyo vya siri( naomba nisivizungumzie na kazi yake ni nini kwa kuwa sio lengo) basi katika vile vyumba viwili nikakabidhiwa chumba kimoja kwa ajili ya kupumzika mimi na mizigo yangu nikawa naishi pale ubalozini kwa muda kama week mbili hivi nalala naamka nafanya shughuli ndogondogo za ofisi mda wa kazi ukiisha watumishi wenzangu wananitembezA mjini ,taratibu nikaanza kuzoea mjii mawazo ya kupanga uswahili yakaanza kuingia akilini mwangu ,baada ya muda nikaomba kuhamia mtaani nikakubaliwa bila shaka ( hili niliweka sawa kwanza madhumuni ya vyumba vy pale ubalozini sio kufanya kuwa makazi ya kudumu unakaa kwa muda unajipanga kidogo then unaanza kuishi mtaani) .
Basi mzee mzima nikapa nyumba yangu pale Gikondo karibu na bandari kavu huwa wanakuita MAGERWAA kama sijakosea speeling basi nikawa nimepata nyumba nakuanza maisha nikiwa single kabisa sina hata mtoto wa kusingiziwa nje maisha ya kaanza hapo ( RWANDA hadi sasa hakunaga mambo ya kupanga chumba kimoja kule ukipanga unatakiwa upange nyumba nzima ) maisha yakawa yanaendelea ni kazini nyumbani taratibu vijana wakaanza kunizoea majirani wote wakaanza kunizoea pia sasa sikujua walikuwa wanavutiwa na nini kwangu ila baadae niligundua kuwa walikuwa wananipenda kwasababu naongea kiswahili hivyo nikiwa naongea wanafurahi japo sikuwa na uhakika kama wananielewa au vipi? Akafikia hata wakifanya sherehe zao majirani lazima wamletee barua ya mwaliko mimi nikihudhuria wanafurahi sanaa walikuwa wananiita mswahili. Neno la kwanza kujifunza la kinyarwanda ilikuwa salama AMAKURU yani habari yako.
Maisha yakaendelea pale kazini, ikawa ni mwendo wa kazi kwenda mbele hadi kufikia mwaka 1990 hapo yani nikawa na miezi sita na siku kadhaa kigali miezi yote hiyo nilikuwa sijatoka nje ya mji wa kibali.
Niseme mwaka huo ndo nilianza kupata ufahamu juu ya maisha halisi ya Wanyarwanda mtaani kwangu ikawa nikialikwa kwenye sherehe nakuta watu wale wale (naomba nieleweke hapo kwa mfano unaishi mtaa moja kuna kaya nyingi tu lakini ule mtaa ukawa kama kuna mgawanyiko flani hivi yani ukiitwaa kwa mzee john unamkuta mzee Amosi yupo hivyo kwa mzee Amosi unakuta mzee john yupo halafu mtaani kuna watu wengine hawashirikishwi kabisa japo wapo mtaani hapo.) hii ikawa unanitatiza ikabidi nianze kufanya utafiti wangu kwa siri ikiwemo kuwauliza watumishi wenzangu pale ubalozini.
Pale ubalozi kulikuwa na dereva ambao alikuwa anasaidia anahudumu pale ubalozini,siku moja nikamuuliza kuhusu hilo jambo alichonijibu ni kuwa hicho kinachotokea na ndo maisha halisi ya Wanyarwanda yani Watusi na Wahutu hawafungamani katika mambo mbalimbali akasema kuwa kuna hali ya ubaguzi wa hali ya juu hasa Wahutu kuwabagua Watusi ambao ni wachache sanaa na hilo ndo nilipokuwa nilishuhudia kwa takribani kipindi cha mwanzoni ila nikawa siajelewa mtusi yupo na mhutu yupo na unamtambuaje mtusi na mhutu unamtambua aje ukawa mtihani sasa kwangu.
Baada ya kulielewa hilo sawasawa ndo ikawa sababu ya mimi kukacha tena kwenda kwenye sherehe za majirani kwani nilihisi kinachotengezwa hapo si jambo jema ikafikia mahala jirani akiniiona nimesimama na jirani mwingine ana nuna au ananipita bila hata kutusalimia ikawa inanishangaza kwakweli CHUKI YA UKABILA NI MBAYAA SANAA.usiombe.
Maisha yakaendelea kama kawaida ila nikaona Nihamie mtaa mwingine kuwakomoa wale majirani, nikawa nimehama pale nikahamia mtaa mwingine nikajitahidi nisiwe na mazoea kama ya awali nikawa ni kazi ,nyumba ,matembezi mjini kurudi nyumbani na kulala.
Hatimae mwaka ukapita ukaingia mwaka wa pili ya ni 1992 hapo ndipo kuna kipindi rwanda kukawa na mambo ya ajabu sanaa yani mnaweza mkawa mmelala wanakuja watu wana silaha, mapanga na mashoka usiku wanawamsha wote mnawekwa kwenye foleni unasikia huyu ni ing'otanyi ukiambiwa hivyo ujue jamaa watakuchukua wanaondoka na wewe ndo kwa heri na ukujifanya kubisha pale pale unageuzwa asusa yani unakataa katwa mapanga watu wanakuona ,ila niligundua waliokuwa wanafanyiwa hivyo wengi wao waikuwaWatusi wakawa wanadai kuwa huwa wanatoroka kwenda kupata mafunzo ya kijeshi polini na wanarudi kimya kimya uraiani kuchora ramani ya uvamizi kuisaidia kikundi cha waasi wa RPF.kwa miaka hiyo uvamizi wa RPF maeneo ya mipakani ulikuwa wa mara kwa mara hadi kufikia jeshi la rwanda kuhamia mipakani kulinda ila mashambulizi hayakukomaa japo majeshi ya serikali yalikuwa tunajitahidi kuzima uasi
Sasa turudi kwa wale watu wanaokuja usiku na bunduki na magruneti na mapanga kusaka watu wanaowaita ing'otanyi ,badaae nikagundua kuwa wale jamaa wanaitwa interahamwe yani kwa kiswahili wavamizi wa pamoja hapa naomba niongelee jambo moja muhimu sanaa kwa faida ya wasomaji, dalili ya kwanza kabisa ya uvunjifu wa amani au vurugu za kikabila au vita ni pale utakapo ona vikundi vya kisiasa, au vya kidini vinakuwa na walinzi au vikundi vya ulinzi halafu wanamilishwa bunduki halafu mkuu wa jeshi la polisi au majeshi anakaa kimyaa hakemei wala kutoa katazo lolote ukiona hivyo Unachotakiwa kufanya uza mali zako zote hamia nchi unapoona wewe ni salama kwako mapema sanaa.
Kilichotokea interahamwe walikuwa kwa mfano kama green gard wa Ccm au red bregard wa chadema , mara ghafla wakawa wanaonekana mtaani wamevaa nguo za chama chao cha MRND wakiwa na silaha kabisa za kivita wanatembea mtaani wanaimba nyimbo za kujipamba chama chao na rais wao hii maanake nini ukiona hivi juu chama tawala hakina imani tena na jeshi hivyo wakaona bora silaha zinaoagizwa na serikali wapewe makada wa chama wajilinde wenyewe, makada wakawapa interahamwe, interahamwe wakawa wNaogopeka kuliko hata polisi au jeshi wakiingia dukani kwako wakichukua mkate au siagi haruhusiwi kuhoji, kuhoji tu umekula kwako utachakazwa kwa kipigo vibaya sanaa sasa ikawa ukiwa na kesi hata kama aliekuonea ni interahamwe ukipeleke kesi polisi hakuna kitakachoemdelea ,kama umemkariri nenda kwa bosi wake huwa anakuwa Kada wa chama mfano mabalozi unamuelezea pale kwa kutia huruma ndani ya dakika sufuri anaitisha gwaride kama huyo aliokuonea ni wa eneo hilo ukimtambua anamcharaza vibaya fimbo mbele za watu ata kama kakupora kitu lazima arudishe hapo hapo ikawa inankishangaza sanaa binafsi nikiwa eneo la nyehere-gikondo kuna moja alinipora saa nikaenda kwa kada akaitwa akanirudishia tena bila ubishi kama kauza au katupa analipa pesa atakayoitaja kada (balozi) haijalishi hicho alichokupola kina dhamana gani.
Leo nimejitahidi kuandika ndefu nitaendelea kesho nimechoka sanaa........itaendelea.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa mkuu...leo imekuwa ndefu.tukutane keshoInaendeleaaa...........

Hii simulizi ni nzuri ila itaisha mvua za masika mwakani
Kasema Keshoo
Hii haiishi leo. Ni kama Isidingo.
Jisome ulichoandika..kaa kimya utashtukiwa bure... Hahaha hicho sio kiswahil cha mtz. Just saying...Mzee unatudanganya.
Ulikumbana na mawasiliano magumu wakati umesoma chuo kikuu kwa hiyo na kiingereza hawajui hujui?
Kule mwanzo unesema unesoma chuo Kule Kule rwanda halafu wakati unaoata ajira unaenda kuripoti unasema Ni Mara yako ya kwanza kwenda nje ya nchi??
CHAIII HII
Sent using Jamii Forums mobile app
Jf kuna watu mafedhuli sijapata kuona! Maana watu wanaendelea kutukana tu hata hawazingatii umri wa mleta uzi.Wengi wao humu huyu mleta uzi ni sawa na baba yao.Huu uzi umejaa kutukanana kwingi sana. Aliyekosea kaomba radhi lakini watu hawasomi coments, ni kutukana tu.
Zaidi ya hilo, ameshaomba radhi mara kibao na kuna jamaa mwingine hapo juu alisema mshkaji amema liza chuo kikuu rwanda, baada ya kuona kakosea ameomba radhi ila kuna watu hawaelewi somo.Jf kuna watu mafedhuli sijapata kuona! Maana watu wanaendelea kutukana tu hata hawazingatii umri wa mleta uzi.Wengi wao humu huyu mleta uzi ni sawa na baba yao.
Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaaahngoja niendelee mkuu
baada ya kula tunda la masikhara kwa yule mtoto wa kitusi, dakika mbili nikamuona jamaa flani mweusi tiii, akija mbele yangu akiwa na gadhabu nzito, macho yake yalikua mekundu ya kuogofya mithili ya mfyatua mafataki kule geita gold mine, umbo lake ni jitu la miraba minne,upande wa kulia kama upande wa kushoto , alikua na mkono mzito kama yale machuma ya kunyanyua mizigo pale bandarini. katika hali ya taharuki huku nikiendelea kumshangaa huyo njemba aliekuwa anakuja mbele yangu ghafla nikashtuka mtu ananishika bega langu la kushotoiiiiiiiii
ghafla katika hali ya taharuki nikahisi kama nimemwagiwa maji usoni.
lahaula kumbe hilikua ni ndoto maza alinimwagia maji kuniamsha niwai shule.
mwisho wa story ukurasa umefungwa twendeni sasa tukajenge nchi.