Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

UNAMIR ni rubbish ipo Siku ntaleta stori ya mambo yao waliyokuwa wanayafanya Rwanda nyuma ya pazia ndo maana baadhi ya mabalozi wakawa hata hawawaiti kuomba msaada. Nilitaka nimwage kila kitu hapa watu wakaanza oohh story ndefu sanaa sijui unatuchosha nimeamua kuacha baadhi ya mambo.

Sent using Jamii Forums mobile app

wanaolalamika mkasa mrefu nani kawalazimisha kusoma au kuifatilia, wewe tiririka kama ulivyokusudia wengi watasoma.

kila mtu ana maoni yake hata ukipost neno "nawapenda wote huku ndani" still kunaraia watakashifu tu nashauri na kukutia moyoi, kama umekusudia kusimulia mkasa huu basi endeleea.
 
Hawawezi kutoa nyaraka hata moja coz kuna watuhumiwa bado wapio ICC na bado kesi zao hazijaisha.na nimefuatilia kwa karibu sanaa lakini Hamna kitu
Hofu yako tu mkuu, Washington DC wanakawaida ya kudisclose classified issues kila baada ya miaka 20 kwasababu they got no impact to the public zaidi ya kuwajuza nini hasa kilitokea au kufanyika na serikali ilichukua hatua gani. Hata kama hatua walizozichukua zilipelekea mauwaji huwa wako waziwazi na wanaiomba msamaa jamii.
So wewe ongea as long unachotaka kusema labda wao walishazitoa hizo nyaraka zamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante ,ila kama nilivyosema mwanzo najitahidi kukumbuka .kichwa kimechoka uzee babaa nisamehe.simu yenyewe natumia ya tigo tujiftishe.
Bossless stori yako ni nzuri sana, na uzuri wake ni first hand hata haina marejeo ya vitabu kama zile za TheBold ila unaleta kidogo kidogo mnooo kiasi kwamba wa Tz sasa umeanza kuwakera wanastahamili tuu kwasababu wanapenda kijisomea stori na hapa ndipo unapogundua kuwa si kweli kuwa WaTz hawana tabia ya kujisomea ila hawapendi kusoma stori zilizopoa sanaaa na zenye mazingira ya kubuni sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante ,ila kama nilivyosema mwanzo najitahidi kukumbuka .kichwa kimechoka uzee babaa nisamehe.simu yenyewe natumia ya tigo tujiftishe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee Baba unaweza kutueleza kwanini katika safari ile ya kurudi toka Dsm Rais Juvenile Habyalimana wa Rwanda na Cprian Ntadyamila wa Burundi walipandishwa ndege moja!
 
Ushauri wa bure usiweke mambo yasiyo na msingi ili stori iwe fupi na ivutie wasomaji wengi.

Kwa mfano nikachukua basi kwenda Nyamirambo haina haja kuadisia basi ya rangi gani nauli sijui sh ngap huko ni kupoteza muda tu.

Weka vile vitu muhimu sana na ambavyo vilikupa changamoto na hutosahau

Sent using Jamii Forums mobile app
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
“kama hizi zote hazina haja”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Baba unaweza kutueleza kwanini katika safari ile ya kurudi toka Dsm Rais Juvenile Habyalimana wa Rwanda na Cprian Ntadyamila wa Burundi walipandishwa ndege moja!
Huyo wa Burundi aliitwa Cyprien Ntaryamira. Nae alikuwa na ndege yake lakini aliamua kupanda ndege ya jirani yake kwa vile ile ya Habyarimana ambayo alikuwa kapewa na serikali ya Ufaransa ilikuwa ni ya kisasa na yenye kasi zaidi kuliko ya kwake. Pia walikuwa na mambo yao ya kuteta wao kama marais na baadhi ya wasaidizi wao.

Chini ni picha ya makazi ya rais Habyarimana ambapo nyuma ya nyumba hiyo ndipo ndege iliyowachukua marais hao ilipoangukia baada ya kuwa imeshambuliwa. Mahesabu yalipigwa kiasi kwamba ndege ilipotwangwa makombora ikiwa angani ilikuja kuangukia ndani kabisa ya makazi ya rais maeneo ya Kanombe umbali mfupi kutoka ulipo uwanja wa ndege wa Kigali. Picha nyingine ni mbaki ya ndege hiyo iliyotunguliwa ambayo hadi leo yapo kwenye makazi hayo japo uwa hawaruhusu watu kuyapiga picha labda upige kiwiziwizi.

Mara kadhaa nimefika kwenye eneo hilo ambalo kwa sasa ni kwa ajili ya makumbusho. Hata hivyo uwa nashindwa kuamini kuwa pale kweli palikuwa ni makazi ya rais labda pengine kutokana na umasikini wa nchi hiyo kwa miaka hiyo. Mfano ukuta wenyewe unaozunguka makazi hayo ni wa matofali ya kuchoma tena ya kawaida tu na pia jengo lenyewe kama linavyoonekana pichani ni la kawaida tu japo ndani kulikuwa na ulinzi na tahadhari za kutosha za kiusalama plus ushirikina wa hali ya juu.
 

Attachments

  • images (16).jpeg
    images (16).jpeg
    45.4 KB · Views: 69
  • images (17).jpeg
    images (17).jpeg
    38 KB · Views: 69
Wee jamaa ni POPOMA, yani sijui wazazi wako walilipia ada ya nini?? Halafu utakuta et na ww una mpenzi!!!!!

Wapi amesema kipindi hicho alikuwa amesoma chuo kikuu?? Wapi amesema alisoma Rwanda???

Kichwani mwako umebeba makamasi tu

Kizibo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]....! Jf kiboko I see “Halafu utakuta et na ww una mpenzi!!!!”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIP MCH.MTIKILA alinipa mwanga kidogo!!Mauaji yaliratibiwa ikulu ya Dar!Wakapiga ndege wawili kwa jiwe moja!!!JK nyerere alifanikiwa kupachika vijana wake uganda,Rwanda,Burundi na DRC!!!Hadi sasa Watutsi wamejipenyeza Tz!wapo wa kutosha kwenye system!!!
Inawezekana kabisa mkuu maana haiwezekani JWTZ walitumwa kwenda kuisaidia Frelimo halafu Hapo Rwanda wasitumwe halafu mpaka ukafungwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaendelea...................... 49k viewers si mchezo.

Haya sasa tusonge mbele tarehe, saa, sekunde za malaika mtoa roho zikawadia 6/04/1994. Saa tisa usiku tukaashuhudia kitu kama kimondo kikishuka ardhini ila kikapotelea vichakani kwa mbali nje ya mji. kutokana na kishindo chake pale ubalozini kila mtu aliamka lakini hakuna aliejua hasa ni nini, tukachukulia kawaida tukajua ni yale yale kila siku si tumeshaanza kuzoea watu wakaendelea kuchapa usingizi nawanaume wakaendelea kulinda getini.
Asubuhi mapema tukashudia hali ya ajabu ambayo sijawahi kuiona katika maisha yangu, yani kukatokea kitu kama wingu hivi yanii mtu akisimama mitaa tano au kumi kutoka ulipo huwezi mtambua vizuri hadi awe karibu sanaa. Wenye redio wakafungulia redio zao kusikiliza , ikumbukwe kuwa kipindi chote wapiga mayowe wa propaganda redioni walikuwa hawaongee ulikuwa unapigwa tu muziki wa chama ila alfajiri ikasikika wimbo wa taifa ndo unapigwa watu wakabaki wanashangaa halafu unakuwa unajirudia .dalili ya kitu kibaya ikaanza kuhisiwa kigali yote kimyaa.....

Tukawa sasa tunaingia tarehe yenyewe 7/04/1994 harufu ya damu ikawa inasikika kigali nzima, makelele ya maumivu ya watu yakawa yanasikika kwa mbali kutoka hapo ubalozini ,balozi ndo akawa ametoka kututangazia kuwa sasa hali si nzuri rais habyarimana ameuawa ile kusema tu vile watu wote akili zilituruka wengine wakawa kama wanataka kukimbia hovyo wanaume ikabidi wafanye kazi ya ziada kwani kitendo cha kutoka nje ya ubalozi kingeleta maafa makubwa sanaa. Ila wote pale picha iliyotujia kichwani ni kwamba sasa tunakufa hakuna tena msalie mtume.

Swali likaja nani kamuua rais? Hakuna mwenye jibu. Aise kuna wimbo moja hivi ukiimbwa unakuwa kama vile unaomboleza unafanafana na ile ya Kimasai ukawekwa kwenye radio ukawa unapigwa huku unamtaja rais kuwa ameuliwa na Ng'otanyi(waasi wa kitusi) aisee vita ikawa imeanza rasmi hata balozi sasa akawa hatoki tena tukakaa wote mle ndani hakuna kutoka kufuata chakula wala nini.

Siku ya kwanza mitaa kelele kila upande, sasa interahamwe wakaanza kuvamia hadi balozi za jirani ambao walikuwa wameondoka walinzi wao wakakimbia watu wakazidi kuuawa. chakula pale kwa ni uji tu hakuna sukari wala nini, unajua kama upo vitani mara nyingi unakuwa husikii hamu ya kula na unajiona uko powa tu kumbe unazidi kuisha ( kama kuna mtu alipigana vita humu ya kagera atadhibitisha hilo) halafu unaweza shanga kumekucha ghafla kiza kimeingia ghafla usiku mnalala usingizi wenye wa mang'amung'amu tu.

Balozi zikawa zinaendelea kuvunjwa siku zinaenda magrounet yanarushwa hovyo hovyo risasi zinalia zikitulia labda nusu saa zinaanza tena,unajua rwanda ni milima sasa unaweza kaa usiku unaona roketi inarushwa kutoka upande moja kwenda upande mwingine vimulimuli tu vya moto hadi kuna kucha kelele na risasi zinaanza tena. Sasa ikawa dhahiri kuwa hakuna namna tumuachie mungu tu.

Lakini wakati huo balozi alikuwa kwenye chumba kimoja kati vile vyumba vya sili nilivyosema hapo awali sijui alikuwa anafanya nini , ikafika ya kumi sasa ikawa hakuna kitu tena njaa tupo katikati ya vita mjini umezungukwa na wanajeshi wanapigana live bila chenga jiona ya siku hiyo ndo wakaja wanajeshi wa rwanda ,na toka siku ile ndo niliwaona live wanajeshi wa rwanda majitu yamepanda sura ngumu macho mekundu wakaja na maroli yale 24 na ile defender nyeupe ila waliokuwa kwenye ile defender hawakushuka tukaitwa uwani ubalozini .balozi akatoa tamko akasema SAFARI YA KUWAONDOA KIGALI WATANZANIA NDO IMEFIKA NA KAMA HUNA PAPER ( PASSPORT ) TAFADHARI USIPANDE KWENYE ROLI UKIPANDA LIKALOKUTOKEA MBELE USILAUMU MTU. hii kauli aliitoa kwa uchungu na kwa msisitizo sanaa huwa siisahau maishani mwangu. .

Hapo sasa ndo ngoma ikawa ngumu kila mtu akamkimbilia balozi kuomba amsaidie mkewe na watoto wake, balozi akagoma kabisa wengine akawa anawajibu kama unampenda mkeo baki nae hapa aisee watu wakawa kama vile wamepagawa maroli yapo nje lakini unashindwa kwenda kulipanda paper huna , sasa kuna kisa kimoja kilichojitokeza sintokuja kukisahau.kuna mama wa kinyarwanda mtusi alikuwa na bwanake mtanzania amezaa nae ila yeye kipindi cha vita alikuwa ameleta mzigo tanzania ,hivyo ikabidi mama ajitoe mhanga akamuita balozi awachukue wale mabinti wake mapacha wawili walikuwa kama na miaka 14 hivi weupe pua za kitusi kabisa balozi akakubali mama akabaki ,sasa tutaona mbele walivyotaka kuleta kizaazaa nusu tuchapwe RPG kwa sababu yao.

Sasa tukawa tumejipakia kwenye roli wengine wasio na vibali wakawa wamebaki pale hapo ubalozini, hapo hakuna kusikitikiana mnapeana mkono wa kwaheri basi safari ikawa imeanza na escot ya wanajeshi wa rwanda ,vizuizi kibao tukifika kwenye vizuizi wanashuka wanaenda wanajeshi wenyewe wanavitoa tunapita ,cha ajabu vizuizi vingine vilikuwa havina hata watu sijui walikuwa wakajificha au vipi.

Sasa wakati vita imepamba moto Tanzania wakawa wamefunga mpaka wake na rwanda Ikatulazimu kupitia boda ya burundi sasa kimbembe ndo kikaanza hapo, kuna wilaya kama tatu inabidi upite ndo ufike boda ya Burundi na rwanda kama sijakosea kwa kutokea kigali lazima upitie province ya butare halafu ya Gitarama ya mwisho nimeisahau kitambo sanaa. Sasa province Butare (wenyewe wanaita) ili ufike lazima uvuke mto fulani mkubwa unaitwa Nyabarongo kuna daraja kubwa hivi linalounganisha kigali na hiyo wilaya hapo sasa ndo niliona mchezo wawale jamaa saba wa defender hapo tunaenda lakini magari yanakanyaga maiti barabarani maiti zimezaga kila kona. Ile tunashuka kilima kidogo inakaribia kuulifikia kama kilomita tatu hivi wale wanajeshi wa rwanda wakageuka na gari lao ghafla wakarudi nyuma moyo ukapiga paaahhh nikahisi kuna kitu si chakawaida unageuzaje gari ghafla unarudi kwanini usituache tuvuke ndo urudi aisee.

Mbele tena kidogo ile defenda ikasimama katika ya barabara hakuna gari kuendelea kupita magali yakawa yamesimama tu ile defenda ikawa inaendelea kusogea mbele sisi tumeambiwa tusimame hapo hapo hadi Difenda itakaporudi kutoruhusu tuendelee tukawa tu pale na madereva kila mtu kwenye Kibini wengine kwenye bodi nyuma kimyaaaaaa...


Kama lisaa hivi tukasikia risasi zinalindima vibaya Sanaaa yani ikawa dhahiri kama mbele yetu kama kilomita moja watu wanapigana lisasi live ila hatuoni tatizo la rwanda mapori na vichaka vingii ila risasi zikawa zinalia kama zipo chumbani nikasema sasa huu ndo mwisho wetu.

Mwisho lisasi zikakoma tumekaa kama nusu saa hivi defenda hairudi na risasi hazisikiki tena Mwisho balozi akaamuru tuendelee na safari bila defenda dahhh ile tunafika darajani maiti kibao zimelala hapo ila hakuna defenda tukawa tunaendelea na safari tu.

Sasa tukawa tunakaribia kuimaliza province ya Butare sasa hapo ndo kulitokea kizaazaa cha wale mabinti aise tulikuta bonge la kizuizi...... Na maenterahamwe mchanganyiko na wanajeshi wa rwanda aise........ Nikasema. Sasa tunakufa.................................

Itaendelea...........................................

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo Gitarama ndo kuna makumbusho makubwa ya hayo mauaji. Butare( Huye) yakifanyika mauaji makubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unitumie hii story yako kwenye PM.

Hawa watoto wa cerelac ni shida.
Kutokana na kashfa na matusi ya baadhi ya memebers humu napenda kusitisha ushuhuda huu, niwaombe radhi tena na samahani sintoweza kuendelea bora nihamishie ushuhuda wangu kwenye another social network lakini sio humu jf. Mtu hajamaliza kuandika unatukanwa, anakashifiwa,sijui huu utamaduni sijui wawapi? Cha ajabu modereta wanakausha tu bila kukemea mwisho jf inaonekana imekuwa kijiwe cha wahuni. Asante sanaa. Naomba nami nibaki kuwa msomaji wa mada za wengine humu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa huyu mleta story anatumia nguvu nying kuliko kuleta mwendelezo wa story Yeye kutwa kujibu story yenyew unaandika kidogo kidogo Sasa s uweke nguvu zako kwenye mwendelezo kuliko kujibu kujibizana
 
Back
Top Bottom