Mkendo
JF-Expert Member
- Oct 14, 2013
- 3,137
- 2,233
Ndiyo Mkuu
Ndiyo Mkuu,Mwenyezi Mungu awarehemu wapumzike kwa Amani ..Ameen.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndiyo Mkuu,Mwenyezi Mungu awarehemu wapumzike kwa Amani ..Ameen.
Powa tu mbona nawao waliwakata mapanga wenzao.ila Vita ya makabila isikieni tu.hii stori imenihuzunisha sana.hasa pale balozi alipowaambia Kama una passport panda gari Kama huna litakalokukuta tusilauminae. So sad [emoji24][emoji24][emoji24]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji1787][emoji1787] we mdingi inaonesha enzi zako ulikuwa machachari sana kama DOMO hivi[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Pua mkuu!Kuna mahali umesema hukujua mtutsi na Muhutu wanawatofautishaje
Hujaeleza uligundua wanawatofautishaje
Mimi pia hunichanganya naomba unijuze
Sent using Jamii Forums mobile app
Bikira Maria aliwatokea watu kuwaonya kuhusu kimbari?Lakini ajabu dunia ilifahamu ikapuuza. Bikira Maria hadi alitokea kuonya kinachokuja lakini wale mabinti waliotokewa walipuuzwa! Ila yale mauaji ya Rwanda sijui nini kiliikumba dunia!
Sent using Jamii Forums mobile app
Powa tu mbona nawao waliwakata mapanga wenzao.ila Vita ya makabila isikieni tu.hii stori imenihuzunisha sana.hasa pale balozi alipowaambia Kama una passport panda gari Kama huna litakalokukuta tusilauminae. So sad [emoji24][emoji24][emoji24]
Naona ni Comment yako ya pili na zaidi unamhusisha magufuli na huko, una shida gani mkuu.Mkuu yule jamaa unayemsifia wajua kuwa ametoka huko? Watch out your mouth bro.
Sent using Jamii Forums mobile app
Inaendelea .............Habari zenu wakubwa kwa wadogo.
Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.
Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.
Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.
basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..
Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.
Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.
Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.
Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.
Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.
Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.
Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .
Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.
Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .
Itaendelea...........
Muendelezo bonyea link hizi.
Sehemu ya nne
Sehemu ya tano
Sehemu ya sita
Sehemu ya saba
Sent using Jamii Forums mobile app
Una shida gani mkuuImekreki baada ya wewe kuleta hii storry? I can smell something fish.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sijamaanisha tofauti na maoni yako.unavyosema ndio hivyo hivyo.Mkuu "Mbari" ni neno la kiswahili lenye maana ya Koo "clan" "ethnicity" kitu ambacho wengi awakijuhi ni kwamba yae mauaji ya Rwanda yalikuwa baina ya koo mbili za watusi na wahutu (sio kabila) kwan uko watsi na wahutu wote wanaongea kinywarwanda na tamaduni ni sawa awa tofauti zao ni morphology yaan mwonekano....sifa ya ziada awa watusi inasadikika wana asili ya Ethiopia ndo maana ni wazuri kulinganisha na wahutu, mauaji yale kuna wakt mtu ilibidi uokolewe na nan anakujua au "kipande" id na wala sioo mwonekano wako kwan walishaingiliana so kupoteza identity...
I stnd to be corrected
Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania tulichukua hatua gani mauaji wakati mauaji yanatokea ni swali gumu fikirishi sana
Sent using Jamii Forums mobile app
Type error.Unapatikana nchi gani mkuu kwa sasa...maana unaposema leo mchana utaendeleza hii story ni kama vile hapo ulipo sasa hivi ni majira ya asubuh.
Ile defender ya watu 7 kumbukaYani nasoma hadi mwili unasisimka...but naona umejitahidi sana kuna codes( classified info) nyingi kwenye hii hadithi...funguka tu ni zaidi ya miaka ishirini sasa.
Lile wingu lilisababisbwa na nini?ama ndege iliyotunguliwa ilikua karibu na eneo la ubalozini?
Huyu mshua humo ubalozini hakuwa hata mhasibu..alikuwa field nyingine tofauti na accountsNapata wasiwasi kuna baadhi ya mission balozi alikuwa akizichezesha ndio maana kuna vitu umevifungafunga anyway nahisi kuna mkono wa tanzania ulihusika katika kifo cha huyo Rais...
Embu ngoja tuone muendelezo utakuaje...
Sent using Jamii Forums mobile app