Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Sintosahau nilichokishuhudia kwa macho yangu nchini Rwanda wakati wa vita vya kikabila 1994 hadi naingia kaburini

Powa tu mbona nawao waliwakata mapanga wenzao.ila Vita ya makabila isikieni tu.hii stori imenihuzunisha sana.hasa pale balozi alipowaambia Kama una passport panda gari Kama huna litakalokukuta tusilauminae. So sad [emoji24][emoji24][emoji24]


Hii inamana kwa wale wazee wakuchanana makaratasi baada ya kuingia nchi za watu eti ili wasirudishwe kikinuka wenyeji wanajuana Kaz kwako uliechana Mana ukienda ubalozin ndo Kama hvyo wanakupokea Sasa unarudije kwenu? Ndo mziki hapo mfano China, south Africa na huko Rwanda Kama ulizamia au ulichana huwez Rudi.

Bongoland n kuxuri Sana Basi tuu watu wamepazoea ndo Mana wanaona kwingine kuxur
 
Powa tu mbona nawao waliwakata mapanga wenzao.ila Vita ya makabila isikieni tu.hii stori imenihuzunisha sana.hasa pale balozi alipowaambia Kama una passport panda gari Kama huna litakalokukuta tusilauminae. So sad [emoji24][emoji24][emoji24]

Hidden information ni kwamba kwa sasa wahutu wanaendesha harakati zakurudisha utawala mikononi mwao na wamejichimbia hko misitu ya DRC wakipanga jinsi ya kumuondoa Kagame. Kingne wadadisi wa mambo husema wahutu ndani ya Rwanda hawamkubali PK nae analijua hilo na hutumia mkono wa chuma kuwadhibiti...ndo maana utasikia watu kupotea na kuuliwa. Ila kuna mauaji mengi sana ya siri hko.
 
Habari zenu wakubwa kwa wadogo.

Kwanza napenda kutoa pole na shughuli za kutwa kwa wale wahangaikaji wote kama mimi ambao kila siku lazima tutoke ili tuweze kujipatia riziki halali kila siku iendayo kwa mungu. Tuseme wote asante mungu.

Nisiwachoshe niende moja kwa moja kwenye mada,mdaa huu wakati naandika huu ushuhuda wangu binafsi ambayo nimeishuhudia kwa macho yangu mawili nchini rwanda wakati wa vita ya kikabila ,wenyewe hupenda kuiita mauji ya halaiki.

Stori inaanza wakati ndo nimemaliza masomo yangu ya uhasibu ngazi ya stashahada mwaka 1989 (sintotaja chuo hicho) nikajaribu kuomba kazi wizara ya mambo ya njee mungu si Athumani nikapata kazi ubalozi lakini nikapaangiwa kituo changu cha kazi kigali-Rwanda, kama sijasahau ubalozi Tanzania ulikuwa maeneo yanaitwa KICHUKIRO ,kwa sasa sijui kama bado upo palepale au vipi sina uhakika.

basi mwezi wa sita baada ya kukamilisha taratibu zote nikaanza safari ya kwenda Rwanda kituo changu cha kazi kipya,ajira mpya na mara ya kwanza kusafiri nje ya Tanzania... Safari ikaanza kwenda kuanza maisha mapya nchi ya watu ,mbali na ndugu jamaa na marafiki nikiwa sijui chochote kuhusu nchi hiyo..

Angalizo. naomba tuvulimiliane ni long stori kidogo na yanaweza jitokeza makosa ya kiundishi na kifasihi.... Ntaelezea mambo mengi sana ya kutisha ambayo niliyashuhudia kwa macho yangu mwenyewe ambayo hadi leo nimejitahidi kuyasahau lakini imeshindika kabisa.

Safari inaanza pale Mnazi moja nakumbuka enzi zile kulikuwa hakuna mambo ya Booking. unawahi alfajiri na mapema unatafuta basi lako unapanda tu unasubiri safari ianze.

Basi nikiwa na mabegi yangu na shilingi za kitanzania 60 elfu(nilipewa kwa ajili safari na kujikimu na passport ) tu ,naianza safari ya kwenda Kahama, safari ikaanza midaa ya kama saa moja kamili asubuhi (jina la basi lile nimelisahau ila nakumbuka lilikuwa rayland) kipindi hicho barabara ni vumbi tupu changarawe la vumbi hadi linaingia kupitia madirishani, baada ya safari ya uchovu mwingi hatimae saa nane usiku tunaingia singida stand. Mimi mgeni sijui niende uelekeo gani ikumbukwe miaka ile nyumba za wageni zilikuwa za kuhesabu basi ikabidi tushuke pale stand tukawa tunakula mikate na chai na wengine chai na kahawa.

Basi mimi nikarudi kulala kwenye gari,alfajiri na mapema gari likaanza safari tena nakumbuka tulifika stand kuu Kahama kana saa tatu usiku hivi. yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!

Tumefika Kahama stand tumepokelewa na wapiga debe enzi hizo wao ndo walikuwa kama mawakala wa magari makubwa anakubebea mzigo hadi kwenye gari unalipa nauli yeye anachukua chake mnaachana hapo hapo hapo ni usiku inabidi kupata gari ya kwenda boda ya Rwanda na Tanzania Rusumo hapo unavuka Mpaka, kuna mto mkubwa unaitwa mto Rusumo unapita kwenye daraja la chuma kama lile lile liloejengwa na wanajeshi pale njia panda Kawe unavuka ng'ambo ukagonga passport ,cha kuchekesha pale kulikuwa hakuna magari ya abiria makubwa.

Magari ya abiria kutoka boda hadi kigali mjini yalikuwa hakuna, ilikuwa inakubidi upande roli la mizigo au abiria mjichange kwa makundi mkodi magari madogo kama tax ila mnabananishwa humo hatari na mizigo juu, kutoka boda hadi kigali ilikuwa kama mwendo wa masaa nane hivi kuingia kigali mjini.

Hatimae baada ya kubadilisha fedha zetu kuwa mafaranga tukapata usafiri wa kutufikisha kigali nakumbuka kundi langu kwenye gari tulilokodi nilipanda na wazaire watupu hivyo kelele zilikuwa nyingi hadi tunaingia kigali wanaimba nakuongea sanaa ubishi mwingi mara mpira mara siasa ili mradi makelele tu.

Saa tisa mchana nikawa tumewasili kigali town enzi hizo sijui lolote kuhusu mji huo zaidi ya address na namba za simu ikabidi niangaze angalau kupata simu lakini wapi,aise kinyarwanda sijui na wao kiswahili kigumu kila nae mujliza ila kupata mawasiliano sikupata msaada ikabidi nikasogolea kwenye stand ya mabus madogo nikamuulize konda kuwa nataka kwenda ubalozi wa Tanzania akaishia kucheka tu niligundua hakunielewa lugha .

Nakumbuka nilikaa stand pale hadi saa kumi na mbili bila bila ikabidi niulizie sehemu pakulala hapo nikaeleweka nikaambiwa lazima upande bus nipelekwe sehemu inaitwa NYAMIRAMBO na nikaambiwa pia kuwa kuna waswahili wengi nikapanda bus hadi nyamirambo nikashushwa tu stand konda akanionyesha kuna hoteli moja ilikuwa imeandikwa nakumbuka inaitwa kama sijasahau ilikuwa inaitwa IMHALA ila nyamirambo ilichanganya kigodo naweza fananisha Magomeni enzi zile.


Nikaenda nikalipia chumba nikaomba kuelekezwa eneo la kula nikaelekezwa, nikaenda nikala halafu nikarudi kujilaza nikipanga namna ya kuingia kesho u abalozi wa Tanzania kuanza majukumu mapya .

Itaendelea...........

Muendelezo bonyea link hizi.

Sehemu ya nne
Sehemu ya tano

Sehemu ya sita
Sehemu ya saba





Sent using Jamii Forums mobile app
Inaendelea .............

Tulipoishia Sasa tukawa tumefikia kuimaliza province ya Butare hapo ndio tukakuta kizuizi interahamwe kibao kama Mia mbili hivi na kila mtu na panga wengine wamebeba RPG wengine vibomu vya Mikono halafu pembeni Kuna maiti kibao, Sasa kilichonistua zaidi maeneo yale kulikuwa na maiti mbili za wazungu nahisi atakuwa mke na mume, Sasa nikajiuliza kama hawa wazungu wameuawa sisi ni akina nani tusiuawe. Ikawa Sasa magari yamesimamishwa .

Sasa nikawa nawaza hivi lile defender limeenda wapi na wale jamaa hapa siwangesaidia au katika mapigano Yale pale darajani limeangukia mto Nyabarongo. Sasa hapo ikawa ni kushuka wote hakuna Cha dereva wala utingo unazima gari chini maroli 24 yote watu tukawa chini jamaa wanaimba nyimbo zao za chama mapanga juu yanalia tu nguo zao zimejaa damu nikajisemea sasa tumekwisha ikabidi balozi atoke kwenye gari lake aje nyuma kwenye maroli.

Sasa ikawa tumepangwa kwenye mstari unanyanyua passport yako juu huna unakaa pembeni, Kama unakumbuka kuna watu nilisema wakati tunavuka daraja walikuwa wanapanda maroli ya nyuma nao walikuwa wanakimbia Kigali sasa ikaja kimbembe kumbe hawana karatasi (passport) Ila ni wanyarwanda aise wakawa wanawekwa pembeni tu haijalishi ni mtusi au ni mhutu

Sasa hapo likaja swali wakawa wanaulizwa wale jamaa kwanini mnakimbia wakati nyinyi ni wahutu kwanini msibaki mpambanie nchi yenu wakawa wanajitetea tu aise likatokea jamaa likamkata na panga moja wapo miongoni mwa wale eneo la shingoni damu ikaruka aise mwili wangu haujawahi kufa ganzi Kama siku ile (Kuna kitu nimejifunza na kimekuwa kikijadiriwa Sana humu binadamu anapokaribia kufa huwa hasikii maumivu yeyote huwa anakuwa Kama amepigwa na ganzi Kama tutaendelea kunifuatilia nitaelezea tukio lilonitokea nikiwa nikiwa jela Ndola-Zambia baadae sana, msistuke nimeshafungwa jela miaka mitatu kisa biashara za chuma chakavu) tuendelee...

Sasa Yule mtu aliepigwa panga akawa amedondoka anakoroma Kama mbuzi aise kwa kweli pale akili iliondoka kidogo nikawa kama nimehama ulimwenguni kwa sekunde kadhaa hapo wote passport zipo juu yaani unanyoosha Mikono na passports jamaa linapita linakagua aise ikawa huku Zoezi la kuwasurubu wale wahutu wengine likiendelea Sasa Kuna watu sijui ni ndugu wale nao walikuwa wamedandia roli wakawa chini pamoja nasi yule mkubwa akapewa panga amkate yule mdogo shingoni ikawa jamaa anasita sita wakasema Sasa tunawaua wote si hutaki, pale pale yule mkubwa akampa mpanga yule mdogo halafu alikuwa amevaa Sweta zile zenye kofia akaivua akakunja shingo akamwambia yule mdogo piga shingoni ikawa Kama anasita Ila Kaka mtu akamwambia piga yule dogo akapiga kweli damu ikaruka hadi nilipokuwa nimesimama Hadi matonetone yakawa yamechafua kidogo suruali niliyokuwa nimevaa aise jamaa kadondoka mzima mzima paaaa...

Sasa hapo balozi anaongea na lile jamaa lililoonekana Kama ndio kamanda lao Ila likawa Kama halina time nae vile nikajisemea Leo hatutoki, majamaa yanapanda kwenye maroli yanachukua kila kitu kilichokuwemo mikate, nguo, viredio, majiko na masufuria ya kupikia


Sasa hapo tukawa njia panda. Sasa wakati lile njembaa linakagua aise likafika kwenye gari ya balozi likawaona wale mabinti aise acha liwachomoe unaujua ile gari ya balozi Ilikuwa na tinted hivyo alivyoshuka aliwaacha, watoto wakachomolewa wakavutwa nywele Kama kuku vile unavyomtoa bandani ikawa Sasa mzozo kila interehamwe anataka awavute ikawa mzozo mabinti wale wakawa katika ya msitu wa wauaji

Mwanzoni nilisema Kuna matukio mawili ambayo Aliyafanya balozi Hadi nikamvulia kofia nimetaja la kwanza pale ubalozi, Sasa Hili ni la pili yule mama (balozi) alichomoka pale pale alipokuwa akaingia katikati ya msitu wa wale jamaa akawa anavutana nao yaani anawavuta wale watoto na wale interehamwe wanawavuta wale watoto sasa ikawa vurugu tupu ikabidi wale watoto wawe wamemuinamia balozi tumboni Kama vile kuku anae atamia, uongo mbaya siku ile ndio nilimchukia balozi wangu yani nilimuuona Hana maana kabisa yaani kwa kitendo kile alichokuwa amekifanya nilijua Sasa anaamsha hasira za interahamwe Sasa tunakufa wote. Dhana ya kuogopana ikawa imechukua nafasi tumefikia mwisho wa uharibifu kila mtu anatetea nafsi yake (nikaona Bora angeacha tu wauawe wale mabinti sisi tuendelee na safari yetu mungu anisamehe ila mawazo hayo yalikuwa Bora kuliko kitu chochote kwa wakati ule)

Mama kakomaa aise lile jamaa likawa limefika pale, balozi kishati chake kimechanwa imebaki sidiria tu na alivaa sketi mama kakomaa lile jamaa likatoa sauti kwa kinyarwanda REKAA hiyo sauti huwa siisahau (maanake nafikiri ni achaa) Sasa wakati anasema vile kuna tukio lilienda sambamba na ile sauti nusu tufe aise.

Unajua roketi ya mkono RPG ukiwa umeibeba lazima uelekeze juu Sasa Kuna interahamwe moja sijui Ilikuwa aje, unajua Hawa hawana mafunzo wameokotwa tu mitaani aliishika Kama vile kashika bunduki ya kawaida Sasa wakati wa vuta ni kuvute sijui lilishika kwenye triga chuma ikachomoka ikapita katika ya watu, ikapita katika ya roli na gari ya balozi tukasikia mripuko aise kila mtu pale alichanganyikiwa yanii ni moshi mtupu Sasa ikawa haijulikani imetokea wapi imerushwa au imekuwaje Tena?

Intetahamwe wakasambaa wengine wakawa wanakimbilia mabondeni, kama dakika kumi zikapita tukawa tumepowaa kidogo Ila kelele tupu lile jamaa likamsogelea balozi likamuuliza hao ni akina akasema wanangu unajua balozi alikuwa mweupe na wale watoto walikuwa weupe kwa struggle ile lile jamaa halikutia shaka tena, mwanamke kumpigania mtoto namna ile hata wewe huwezi kataa kuwa sio mwanae Sasa hapo tukawa tumetulia kidogo jamaa wakaturuhusu safari ikaanza hapo watanzania watupu wale wadandiaji wote walishushwa sijui kilichoendelea nyuma Sasa tukawa tunaingia province ya GITARAMA safari anaendelea upo kwenye kibini za maroli lakini unasikia dereva anaingiza gia Kama vile hataki kwackweli kwa lile tukio kila mtu alikataa tamaa kabisa....

Sasa tunaingia mji wa GITARAMA tunashuhudia Jambo ambalo linatuacha wote tumeduwaa na mi Domo wazi....Ila hakuna wakumuuliza mwenzake. ......jambo gani hilo?

Itaendelea......................................



( Ila kisimu Cha wife daa sijakizoea battan zake napata shida kweli kuandika)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu "Mbari" ni neno la kiswahili lenye maana ya Koo "clan" "ethnicity" kitu ambacho wengi awakijuhi ni kwamba yae mauaji ya Rwanda yalikuwa baina ya koo mbili za watusi na wahutu (sio kabila) kwan uko watsi na wahutu wote wanaongea kinywarwanda na tamaduni ni sawa awa tofauti zao ni morphology yaan mwonekano....sifa ya ziada awa watusi inasadikika wana asili ya Ethiopia ndo maana ni wazuri kulinganisha na wahutu, mauaji yale kuna wakt mtu ilibidi uokolewe na nan anakujua au "kipande" id na wala sioo mwonekano wako kwan walishaingiliana so kupoteza identity...

I stnd to be corrected

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijamaanisha tofauti na maoni yako.unavyosema ndio hivyo hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani nasoma hadi mwili unasisimka...but naona umejitahidi sana kuna codes( classified info) nyingi kwenye hii hadithi...funguka tu ni zaidi ya miaka ishirini sasa.
Lile wingu lilisababisbwa na nini?ama ndege iliyotunguliwa ilikua karibu na eneo la ubalozini?
Ile defender ya watu 7 kumbuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Napata wasiwasi kuna baadhi ya mission balozi alikuwa akizichezesha ndio maana kuna vitu umevifungafunga anyway nahisi kuna mkono wa tanzania ulihusika katika kifo cha huyo Rais...

Embu ngoja tuone muendelezo utakuaje...

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mshua humo ubalozini hakuwa hata mhasibu..alikuwa field nyingine tofauti na accounts

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom