Sijui ni umaskini? Kutokujali na kupuuzia kwa serikali?? au tu kutokujua hatari waliyokuwemo raia wa Tanzania pale ubalozini, yaani mimi nafikiri ilitakiwa zishuke helicopter za JWTZ pale ziwachukue raia na kurudi. Safari ya uokoaji kwa usafiri wa malori ilikuwa ni ya hatari kubwa sana, maana kuyasoma tu waliyokuwa wanayapitia siku za mwisho za kuokolewa pale najisikia vibaya sana sijielewielewi nafikiria wahanga wale walikuwa na hali gani, ni jehanum ya duniani.