tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,016
- 1,946
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
OP ni nani? Mara nyingi huwa natumia browser kuLog in JF, na Mara chache sana natumia App uko nakuta ID zina hiyo OPUkitaka kujua story yako Inafatiliwa kwa makini angalia Views achana na comments za kukatisha tamaa.
Shida JF baadhi ya watu wanajifanya wajuaji sana kumbe vichwa vya panzi.
Mtu hajui hata maana ya stashahada, mtu anakurupuka bila kusoma kwa makini eti 1994 haikua hivo wakati OP kaanzia kuelezea 1989, Inasikitisha.
Nasubiri muendelezo Bossless
Basi tunasubiri story yako mkuu ikiisha hii asante sana kumbe na wewe ulikuwa huko
mkuu kama unajua kuhusu usalama wa taifa utajua kuwa si kilA kitu unachokiona ni disclosed...
so hyo ni moja kat ya majib haswa unayopaswa kuyajua..
Mkuu hector samahani, unaweza elezea kdgo ugomvi wa mzee wa msoga, Kikwete na Kagame?? Shida ilkua ni nin??Alishaandaliwa muda kuchukua madaraka toka Kigali, na wakati Baba yake anauawa hakuwepo DRC. 10 days baada ya baba yake kufariki alitua Kinshasa na ndege toka Kigali Rwanda na kukabidhiwa nchi. Rwanda ina mikono mrefu sana katika siasa za Congo
Asante mkuu michango yenu ni muhimu sana angalau mmetufumbua macho vita hasa ni nini kwa raia. Ni kitu cha kutisha sana na tujiepushe mayo kwa kweli.Sikumbuki Kama alisema hivyo katika simulizi yake Ila ninachojua mimi ambacho ni FACT ni kwamba maelfu na maelfu ya wakimbizi wahutu kwa watutsi walivuka border ya Rusumo toka rwanda na kupokelewa Tanzania kati ya Apr mpaka July 1994, ambapo zilianzishwa kambi za wakimbizi chini ya Uangalizi wa UNHCR, kulikua na kambi za wakimbizi Benako, Kyerwa Karagwe, Ngara pamoja na Rulenge.
Pia ikumbukwe kwamba hakuna border ya nchi kavu kati ya Rwanda na Tanzania zaid ya Daraja la Rusumo, kwingine kote tanzania na rwanda inatenganishwa na maji ya mto kagera. Border ni moja tu pale Rusumo darajani.
Sipingani na simulizi ya mtoa mada. Ni kweli anayosema yalitokea. Na anatoa anaglizo ili tuwe makini yasije yakajirudia tena either rwanda au nchi yoyote ile ya jirani. Siko hapa kupingana nae ila kusupport alichosimulia ila pale nilipoona kuna utofauti ndipo nilipohighlight. Tofauti ni ndogo sana ambazo pia anaweza zitolea maelezo zikaeleweka otherwise kila kitu kiko sawa. Historia na vizazi vijavyo vitatuhukumu tusipoweka haya mambo sawa.
Mkuu hector samahani, unaweza elezea kdgo ugomvi wa mzee wa msoga, Kikwete na Kagame?? Shida ilkua ni nin??
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo mwishoni unamaanisha mkuu wetu yupi akiondoka?
Iko hivi...Congo War 1 ilikua kati ya mwaka 1996-1997. Kuna makundi manne( Mobutu Sseseko, Laurent Kabila, Paul Kagame, Yoweri Musseveni) yaliyopigana vita hii na kila kundi lilikua na interest zake tofauti.
Vita hii ilitokea DRC kipindi hicho ikiitwa Zaire ilianzia pronvince za kaskazini mashariki Nord na Soud Kivu, ikaelekea Kisangani mpaka DRC magharibi then Kinshasha ilipoisha na kuondolewa madarakani kwa Rais wa kipind hicho Mobutu Seseko, nchi ikatwaliwa na Laurent Kabila aliyebadili jina la nchi kutoka Zaire na kuwa Democratic Republic of Congo.
Kwa kifupi ni kwamba wakati vita hii inaanza Mobutu ndiye alikuwa rais halali wa DRC na Laurent Kabila Sr ndiye alikuwa muasi akipigana kutoka msituni mashariki ya Kongo. Kabila alipata msaada wa kijeshi kutoka kwa majeshi ya Rwanda na Uganda chini ya Kagame na Mseveni. Lengo la Kagame si kwamba alikua sympathizer wa movement au uasi wa Kabila bali lengo lake lilikua ni kuwamalizia mbali wahutu na interahamwe wote waliokimbilia Congo baada ya genocide ya 1994 na pia aliona fursa kwenye madini adhimu ya Congo.
Museveni ye hakua interested na wahutu bali ye pia aliona fursa kwenye madini. Sasa basi majeshi ya Rwanda chini ya Gen James Kabaerebe, uganda pamoja na vikosi vidogo vya waasi wa congo wakiongozwa na Laurent Kabila walivamia Congo mwaka 1996 na kuanza kuuwa interahamwe , kushambulia majeshi halali ya Congo ya Mobutu, wakasonga mbele Toka Goma, kwenda Kisangani, kindu, kinanga mpaka walipofanikiwa kuuzingira mji mkuu wa DRC Kinshasha na kumuondoa madarakani Mobutu Seseko, na kufanikiwa kumuweka kibaraka wao Laurent Kabila kama rais mpya wa DRC. Kabila aliwatunuku vyeo jeshi maafisa waandamizi wa majeshi ya Rwanda ilhali hawakua raia wa Congo.
Ambapo Gen wa kitutsi James Kabarebe aliyeongoza vikosi upande wa Rwanda akipewa cheo cha mkuu wa majeshi CDF. Kilichofuata hapo ni historia ilikua ni kuchota madini tu na kuuwa wahutu/interahamwe wote waliokua wakionekana kama threat kwa serikali ya Rwanda chini ya Kagame. Na pia ndipo kipindi hiki wakasimikwa waasi wa Kitutsi mashariki ya DRC wanaoisumbua serikali ya DRC mpaka leo hii.
Madini yalichotwa na wahutu waliuuwawa mpaka sense ilipomuingia Laurent Kabila ambapo katika kujaribu kutokomeza hali hii akamfukuza na kumvua vyeo vyote CDF wake wankinyarwanda Gen Kabarebe mwaka 1997.
Hali hii ilimchukiza Kagame na swahiba wake Museveni ndipo mikakati ikaanza ya kumng'oa madarakani Laurent Kabila iliyopelekea vita iliyokuja kupewa jina ya Congo War 2.
Ni historia ndefu ila kwa kifupi tu ni kwamba zilitafutwa mbinu nyingi za kivita na za kiinteligensia za kumuondoa Kabila Sr mpaka walipofanikiwa kwa msaada wa CIA ambapo mwaka 2001 Laurent Kabila akiwa ofiain kwake Ikulu Kinshasa alipigwa Risasi na Bodyguard wake karibu, na Bodyguard wake pia akapigwa risasi na mpambe wa Rais (ADC) Eddy Kapend, naye pia kabla ya kuwekwa nguvun katika ile taharuki akapigwa risasi na mlinz mwingine aliyetokomea kusikojulikana. Mpaka leo mauaji ya Rais Kabila Sr yanabaki kuwa ni mystery maana walioshuriki katika kufyatua risasi nao pia waliuawa kama cover up.
Baada ya kufanikiwa katika mauaji haya, Joseph Kabila ambaye ni mtoto wa kambo wa Kabila( si mtoto wake by birth) mwenye asili ya kitutsi akakabidhiwa madaraka ya DRC kama Rais. Joseph kabila ni mtusti, mzaliwa wa Rwanda na ni mpwa wa Gen Kabarebe. Alilelewa na Kabila Sr toka akiwa mdogo baada ya baba yake ambaye alikua member wa jeshi la waasi wa Kabila mashariki ya Kongo alipofariki katika umri mdogo, Laurent Kabila Sr akamchukua Joseph na kumlea kama mwanaye, ila Joseph Kabila si mtoto wa kuzaliwa na Laurent Kabila .
Toka mwaka 2001 baada ya Rais Joseph Kabila Jr kuchukua madaraka rasmi kama Rais, plunder na looting ya madini kutoka DRC na kusafirishwa kinyemela kwenye mataifa ya magharibi kupitia Rwanda Kigali inaendelea na itaendelea mpaka kesho as long as Kagame yuko madarakani.
Pichani chini ni Joseph Kabila akiwa na Uncle ake Gen James Kabarebe (ambae amehudumu kama CDF na minister of defence katika serikali ya Kagame kwa miaka mingi toka 2000 mpaka 2018).
Huyo mrefu katikati mwenye sare ya Jeshi ndo Gen Kabarebe na kulia kwake ni Joseph Kabila , hapo walikua Kigali 1998.
View attachment 1384017
I concur.. Ila one thing is certain mtoa mada amewahi kuishi Rwanda maana kwa jins anavyotofautisha haiba, tabia na tofauti kati ya wahutu na watutsi ni pasi na shaka kwamba amewah kuishi Rwanda. Anatoa vivid naration ya yaliyojiri na yeye akiwa part ya yaliyotokea since 1989 mpaka 1994 ambayo siwezi pinga most of the details zinareflect kiukweli yaliyotokea ambayo ni good thing kushare na kutoa mwangaza kwa waliokuwa hawafaham yaliyojiri pia kutoa precaution kuhusu madhara ya ukabila na utengano wa kikanda hasa Tanzania inapoelekea katika uchaguzi mkuu 2020... Kiukweli ukabila ni mbaya sana na athari kubwa sana panapoibuka Civil/tribal wars. History ni mwalimu mzur kuhusu madhara yake tunapoangazia vita mbalimbali za kikabila zilizowah tokea duniani
Lakin pia niseme kuna discrepancies nyingi katika story yake, siondoi credibility ya maudhui ya story hii ila niseme tu;
1. Hakuna province mbili katika nchi ya Rwanda zinazotenganishwa na zaid ya km 150 kama anavyosimulia mtoa mada kwamba wakati wana evacuate toka kigali baada ya vita kuanza kuna kipind walisafiri km 150 toka province moja mpaka nyingine, hii si kweli. Rwanda ni nchi ndogo sana hakua mkoa unaotenganishwa na mkoa mwingine kwa zaidi ya km 150
2. Anasema walitoka province ya butare then wakaenda province ya Gitarama siku iliyofuata then wakafika border ya burundi the next day. Si kweli maana ukitoka Kigali unaenda province ya Gitarama then ndo unaenda Butare(Huye) na si vice versa ndo unafika Border ya Rwanda na burundi. Kwa route hii kutoka kigali mpaka border ya burundi ni only 154km.
3. Kama waliondoka Kigali kwenda border ya Burundi kuna short route ya kupitia Kinazi then Nyamata mpaka Border ya Burundi. Njia hii ni rougly 36km kutoka Kigali unakua umefika border ya Burundi. Ndo njia ya haraka zaidi, Why hawakupita njia hii sijui.
4. Furthermore kutoka kigali kuja Tanzania directly ilikua rahisi zaidi kupitia border ya Rusumo. Ambapo route hii ya kutoka Kigali mpaka rusumo ni umbali wa 156km tu.
Why walienda bujumbura kwanza ndo waje Tanzania mtoa mada anaweza fafanua zaidi.
5. Pia kwa nini aliacha a very lucrative, noble diplomatic job na kuturn into bussiness bila kufukuzwa kazi na kuturn into bussiness za chuma chakavu Zambia itabaki kuwa mystery kwangu. Uache kazi inayolipa vizur na yenye future na heshima ubalozini uende uza vyuma chakavu zambia inatatanisha. Maybe anaweza fafanua zaidi.
6. Evacuation ya Kutoka Kigali kwenda mipaka yote iwe Uganda, Tz, Burundi au ata Goma DRC kwa gari haipaswi kuchukua more than 1 day maana kigali ni katikati kabisa ya nchi. Na umbali wa kutoka kigali kwenda mipaka yote ya Ug,Tz, DRC, Burundi haizidi km 170. Ambayo kama ni kwa hapa Tanzania ni umbali wa kutoka Dar city centre mpaka Morogoro na morogoro hufiki, Rwanda ni nchi ndogo sana.
Yapo mengi ila kwa sasa ni hayo tu.
Wewe ni mvivu wa kusoma jamaa kaelezea vizuri kabisa jifunze kusoma vitu kwa umakinI concur.. Ila one thing is certain mtoa mada amewahi kuishi Rwanda maana kwa jins anavyotofautisha haiba, tabia na tofauti kati ya wahutu na watutsi ni pasi na shaka kwamba amewah kuishi Rwanda. Anatoa vivid naration ya yaliyojiri na yeye akiwa part ya yaliyotokea since 1989 mpaka 1994 ambayo siwezi pinga most of the details zinareflect kiukweli yaliyotokea ambayo ni good thing kushare na kutoa mwangaza kwa waliokuwa hawafaham yaliyojiri pia kutoa precaution kuhusu madhara ya ukabila na utengano wa kikanda hasa Tanzania inapoelekea katika uchaguzi mkuu 2020... Kiukweli ukabila ni mbaya sana na athari kubwa sana panapoibuka Civil/tribal wars. History ni mwalimu mzur kuhusu madhara yake tunapoangazia vita mbalimbali za kikabila zilizowah tokea duniani
Lakin pia niseme kuna discrepancies nyingi katika story yake, siondoi credibility ya maudhui ya story hii ila niseme tu;
1. Hakuna province mbili katika nchi ya Rwanda zinazotenganishwa na zaid ya km 150 kama anavyosimulia mtoa mada kwamba wakati wana evacuate toka kigali baada ya vita kuanza kuna kipind walisafiri km 150 toka province moja mpaka nyingine, hii si kweli. Rwanda ni nchi ndogo sana hakua mkoa unaotenganishwa na mkoa mwingine kwa zaidi ya km 150
2. Anasema walitoka province ya butare then wakaenda province ya Gitarama siku iliyofuata then wakafika border ya burundi the next day. Si kweli maana ukitoka Kigali unaenda province ya Gitarama then ndo unaenda Butare(Huye) na si vice versa ndo unafika Border ya Rwanda na burundi. Kwa route hii kutoka kigali mpaka border ya burundi ni only 154km.
3. Kama waliondoka Kigali kwenda border ya Burundi kuna short route ya kupitia Kinazi then Nyamata mpaka Border ya Burundi. Njia hii ni rougly 36km kutoka Kigali unakua umefika border ya Burundi. Ndo njia ya haraka zaidi, Why hawakupita njia hii sijui.
4. Furthermore kutoka kigali kuja Tanzania directly ilikua rahisi zaidi kupitia border ya Rusumo. Ambapo route hii ya kutoka Kigali mpaka rusumo ni umbali wa 156km tu.
Why walienda bujumbura kwanza ndo waje Tanzania mtoa mada anaweza fafanua zaidi.
5. Pia kwa nini aliacha a very lucrative, noble diplomatic job na kuturn into bussiness bila kufukuzwa kazi na kuturn into bussiness za chuma chakavu Zambia itabaki kuwa mystery kwangu. Uache kazi inayolipa vizur na yenye future na heshima ubalozini uende uza vyuma chakavu zambia inatatanisha. Maybe anaweza fafanua zaidi.
6. Evacuation ya Kutoka Kigali kwenda mipaka yote iwe Uganda, Tz, Burundi au ata Goma DRC kwa gari haipaswi kuchukua more than 1 day maana kigali ni katikati kabisa ya nchi. Na umbali wa kutoka kigali kwenda mipaka yote ya Ug,Tz, DRC, Burundi haizidi km 170. Ambayo kama ni kwa hapa Tanzania ni umbali wa kutoka Dar city centre mpaka Morogoro na morogoro hufiki, Rwanda ni nchi ndogo sana.
Yapo mengi ila kwa sasa ni hayo tu.
Kuweni na subira jameni.
Mwandishi anamalizia kuangalia ile muvi ya HOTEL RWANDA na SOMETIMES IN APRIL kisha aje kuendelea kutusimulia
Bila kusahau hili ndio lilikuwa lengo lake.yani tulitumia kama siku mbili hivi Dar-kahama .leo hii dar - Kahama unatumia siku moja umefika halafu utasikia mtu anasema nchini hii bwana hakuna maendeleo kabisa daa!!!
PK....angewaozesha kwa lazima..wangekuja acha chuki zao...lakini hivi anafanya kuwapaisha zaidi tutsi..kuna siku atajuta!..anapalilia visasi vya milele...
na mbaya zaidi makabila ni mawili tu!
Wakizaliana inabaki ubaguzi tu ila ile chuki ya kuuana inakwisha!
Karume aliona mbali...imebaki...chuki za chini chini tu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly.mkuu kwanza nikushukru kwa uchambuzi, isivyo bahati mambo ya diplomatic ethics yanamlolongo mrefu sanA, kiasi kwamba ukitizama kwa makini Bossless amejarb tu kuelezA yale mambo kwa juujuu sana....
hvyo upo ukwel lakin si ukwel wote ila tukio au matukio ni hAlisi.... wakati mwingin maadili ya kazi yAnazua kusemA kitu maana ukikisemA hicho kitu hAtA kama una id iliyojificha waki track wanajua ni nani kasema.....
b
"Interahamwe" ni neno la kinyarwanda lenye maana ya kupiga pamoja....Maneno Itere+hamwe
ITEREHAMWE INA MAANA GANI?
HAMWE NAHISI INAMAANA YA PAMOJA. JE HII ITERE?
Hii website ina walakini, haikumtaja huyo mama. Kuna utofauti kiasi wa jinsi mleta uzi alivyomuelezea huyo balozi, na shaka yangu ni kuwa pengine wakati wa mauaji, huyo mama alikuwa anakaimu hiyo nafasi, japo yeye kaeleza kuwa tangu 1989 alikuwa ni balozi.Team | United Republic of Tanzania High Commissions, Embassies, Consulates, and Diplomatic Missions
Hiyo website ina orodha ya mabalozi wote tangia uhuru na nchi walizopangiwa. Unaweza search kwa kila nchi pia inakupatia list ya mabalozi waliowahi kuiwakilisha Tanzania hiyo sehemu.
Tatizo ni kwamba huyo balozi hayumo kwenye list, ukipekuwa unaona atukuwa na balozi muda huo Rwanda isipokuwa Burundi na kwenyewe pia akupelekwa mtu baada 1991 mpaka vita ilipoisha.
Ukipekuwa sana domument zingine unakutana na jina la ‘Ami Mpungwe’ kama chief diplomat kutoka wizarani aliekuwa architect wa usuluhishi wa mambo ya Rwanda na ‘Patrick Chokala’ kama msemaji wa serikari hao ndio watanzania wanaotajwa na Dr Salim.
Lakini hakuna mention ya huyu mama balozi, pamoja na uzuri wa story but one significant fact is missing for credibility hapo ndio kwenye utata ili wengine tumeze yote as yet ntachukua 80%; very interesting though.
Hii website ina walakini, haikumtaja huyo mama. Kuna utofauti kiasi wa jinsi mleta uzi alivyomuelezea huyo balozi, na shaka yangu ni kuwa pengine wakati wa mauaji, huyo mama alikuwa anakaimu hiyo nafasi, japo yeye kaeleza kuwa tangu 1989 alikuwa ni balozi.
Kuna balozi ambaye hata kwenye website hakuwekwa jina lake, ni mama na alikuwa kipindi cha 1988/89 mpaka 1993 kama sijakosea.
Hata uki google mazingumzo ya amani ya Rwanda, japo yameandikwa Kinyarwanda/Kifaransa, ila utaona kila ikitajwa Tz na jina la huyo mama linakuwapo. Na alitokea bara sio visiwani.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kifupi hakuna historia ya ubalozi Rwanda kabla 2000’s kwa mujibu wa hiyo website ya serikari.Hii website ina walakini, haikumtaja huyo mama. Kuna utofauti kiasi wa jinsi mleta uzi alivyomuelezea huyo balozi, na shaka yangu ni kuwa pengine wakati wa mauaji, huyo mama alikuwa anakaimu hiyo nafasi, japo yeye kaeleza kuwa tangu 1989 alikuwa ni balozi.
Kuna balozi ambaye hata kwenye website hakuwekwa jina lake, ni mama na alikuwa kipindi cha 1988/89 mpaka 1993 kama sijakosea.
Hata uki google mazingumzo ya amani ya Rwanda, japo yameandikwa Kinyarwanda/Kifaransa, ila utaona kila ikitajwa Tz na jina la huyo mama linakuwapo. Na alitokea bara sio visiwani.
Sent using Jamii Forums mobile app