From: BOSSLESS TO BONGOMAN
SASA TUENDELEA NA STORY YETU ILA NAOMBA NIWATAKE RADHI KIDOGO KUTOKANA NA SHUGHURI ZA SHAMBA NILIVYOKUWA NI MEBANWA HAKIKA UKIJUMLISHA NA HAYA MASIKA HATA MUDA WA KUANDIKA MISTARI MIWIRI TU NILIKUWA NI KUDHINDA SHAMBA NA KULALA SHAMBA .
PLUS KUKIMBIZANA NA NDEGE NA KUTEGUA MAJARUBA PALE YANAPOJAA MAJI KUHUSUS SIMU HAIKUPONA VIZURI NIKAAMUA KUNUNUA NYINGINE TU NAWASHUKURU WALE MLIOKUWA NA NIA YA KUNICHANGIA SASA TUENDELEE NA STORY YETU.
Sasa baada ya kuvuka mpaka ndo nikahisi akili yangu ndo imakaa sawa nakumbuka nilisafiri kwa maroli kutoka mpakani hadi kahama tben nikakaa kahama mjini kama siku mbili hivi then nikakwea train kuingia kuja Dar (ikiwa ni mara ya kwanza kupanda train) ugeni wa kupanda train ukanipa somo fulani ila kuna kituko nilikifanya hadi leo huwa sikisahau na nikikumbuka macheka mwenyewe iko hivi nilipokuwa nimekaa nilikaa na jamaa moja hivi yeye alikuwa ametulia tu na konyagi yake mkononi anakunywa taratibu sasa sikumbuki kama tulibadilishana story kwa namna moja ama nyingine ila kwa asilimia kubwa alikuwa anaongea mwenyewe kilevilevi tu.
Tukafika sehemu hivi nakumbuka itakuwa ilikuwa Tabora train ikawa imesimama akina mama wanauza chakula na mambo mengine hivi sasa tukawa tumeagiza vyakula tunakula sasa wakati tunakula yule mlevi akaniuliza ndugu wewe unaelekea wapi nikamjibi naekea Tanzania halafu nikawa namjibi kwa kujiamini kabisa daaahhh ebwanae watu waliokaribu walicheka hatarii nikajistukia nikarekebisha kuwa naelekea Dar ila watu walibaki na kicheko hatariii. Safari ikaendelea
Hatimae tukafika station_ dar es salama nikashuka nikapanda texi hadi magomeni enzi zile kuna majamaa yalikuwa yanauza mitumba pale barabarani mitumba safi kabisa nikanunua tisheti mbili na jeans mbili zikawa ndo nguo zangu za mwanzo toka nirudi ikumbukwe tu kuwA niliach nguo nyingi na baadhi yamabegi yangu yalipoteana kwenye maroli sasa nikawa ndo naekea home .
Nikafika home nikakuta hakuna mtu ila nyumba iko wazi niakaingia nikaenda chumba cha madogo nikabadilisha nguo nikaenda bafuni kuoga nikarudi nikaingia ndani nikalala mpaka saa kumi na mbili jioni ndo nikaamka nikala sasa ndo nikaanza kupokea pole na maswali kibao toka kwa ndugu jamaa na marafiki wengine wakawa kama hawaamini .mzes asikwambie mtu bongo kuna amani sanaaa
Yani anaenda kuitwa jamaa w mtaa wa ng'ambo kuja kuniona tu jamaa wakawa wazidi kujaa tu nyumbani ikabidi mzee awaambie waje kesho waniache kwanza nipumzike maisha yakawa yanaendelea siku ikapita hadi week ikaisha ijumaa tatu mapema nikariport wizara ya mambo ya njee .
Taarifa zetu zilikuwa zimeshawafikia so kufika nikasaini kitabu nikamuona katibu muhtasi akanipa barua sikujua ina nini nikakaa benchi nikawa na isoma nikumbushe ni mwaka huo huo 1994 ilikuwa kama mwezi wa tano mwishoni au katika ya wa sita hivi ,nikawa nasoma nikakuta barua ya likizo ya miezi mitatu na barua ya malipo ya likizo ya mapumziko na laki 130 nikachukua barua yangu nikarudi home.
Ikimbukwe tu kuwa bado tulikuwa kwenye payroll na hela ilikuwa inaingia kila mwezi kama kawaida .sasa mzee mzima nimasema ngoja niangalie salio kipindi hicho mfumo wa kulipa mishahara kupitia akaunti za mabenk ulikuwa hakuna wewe kila mwisho wa mwezi nikupokea tu kwa mahasubu uwe dar au kigali , sijui taasisi kwaa taasisi nyingine.ulikuwa unaweza kumuuliza mhasibu kiasi au balance ua mshara wako bada ya muda akakwambia so mimi nilikuwa na kama nina miezi 2 hivi sijagusa mshahara nikauliza ikaonekana na kama US 600 hivi .
Nikaridi home maisha yakawa yanaendelea natokea home kila siku naenda pale kwa wauza mitumba napiga story jioni narudi nyumbani nakula nalala siku zikaenda likizo ikaisha nikareport wizarani nikakuta barua ya kupangiwa kituo makau kama mhasibu msaidizi ,
Nikumbishe maisha ya kukaa uraiani miezi ile mitatu ndo yslinifany sasa nikakutana na watu wengi walikuw wanafanya biashara tofauti pale kijiweni japo wengi hawakujua taaluma yangu lakini walitokea kunipenda akiweno mzes moja alikuwa wa kichagga alikuwa na anaitwa Mambosasa sina hakika kama ndo lilikusa jina lake halisi ila alikuwa na mabasi ya abiria ya ubungo_kariakoo alikuwa ameyaandika jina hilo Mambosasa na fiat moja hivi kukuu mzes alikuwa anaishi magomeni makanya na alikuwa ana nunua srepa na kuuza so nikawa nimeanza kupata IDEAR ya ile biashara yake.......
Itaendeleea .......POLE NA CORONA
Sent using
Jamii Forums mobile app