Sinywi pombe Sinywi soda! Ninywe nini nikiwa bar

Sinywi pombe Sinywi soda! Ninywe nini nikiwa bar

Tafuta hii, kuna wakti nilikuwa naziona kwenye baadhi ya bar
1721144324594.png
 
Agiza Baltika. Ni bia ya kirusi yenye Zero alm.

Wakuu Nimeamua kuacha pombe kutokana na matatizo ya kiafya.
Lakini soda pia niliQuite tangu 2020.

Sasa napata changamoto nikienda Bar unakuta siwezi kukaa na kampani ya washikaji maana wenzio wanakunywa we unatoa macho.

Hivi ndo nilikuwa natumia lakini naona siyo kabisa

1. Maji
Aisee haya huwezi kunywa saa moja

2.Grand malta
-Hii inanikera inaleta nzi, mapovu kibao

3.Maji na Energy
Nzuri sana unakuwa na kavibe lakini shida haya maenegy kunywa energy mbili si kiaafya siyo poa naona nakunywa sana…

Hebu nipeni vinywaji vinavyoburudisha bila ya kileo
Kunywa mineral water ni nzuri sana kwa tumbo lako. Kwa jina tulozea hapa kwetu tunaiita club soda
 
Back
Top Bottom