Sio kwa ubaya lakini wenzetu waislamu mnakera na adhana ya asubuhi

Sio kwa ubaya lakini wenzetu waislamu mnakera na adhana ya asubuhi

Nikiwa muislamu mwenye akili timamu na mawazo huru naweza sema kuna baadhi ya watoa adhana hawako sahihi kabisa

Adhana kama adhana ikitolewa kwa mara moja wala haina shida kabisa lkn shida inakuja kwa watoa adhana kuongea sana na kusahau kuna watu wengine wasio waislamu wamepumzika,,kitendo cha kila mda kusema saa ngapi kinaboa sana,,ukweli usiopingika wanao swali hata adhana moja tu inawatosha kabisa

Kuna ambao wanatoa nasaha basi bora iwe maneno machache lkn wengine wanaongea sana,,hivi kuna lipi jema unalofanya wakati jirani yako anahudhunika au kukosa raha kwa ibada yako wewe?

Tuache mihemko ya dini hapa,,kuna mahala waislamu inabidi tubadilike tufahamu kwamba kila kitu kinapendeza kikifanywa kwa kiasi,,,hata kama wengine wasio waislamu wanapiga makelele lakini haihalalishi nasi tupige kama wao

Tumesisitizwa sana kuwajali majirani,kuwajali ni pamoja na kutowakera mpaka wakatuona ni kero kwao

Narudia tena adhana ni ibada kubwa sana na itaendelea kuwepo mpaka mwisho wa dunia lakini tupunguze maongezi alfajir wakati wengine wamelala na kupumzika
Aisee hili limenikuta juzi kati hapo Dar ambapo nililala lodge moja ipo jirani na Kimara Bucha kwa siku tatu. Kuna msikiti mmoja unapiga kelele sijawahi kuona. Jamaa anaanza na adhana saa 11 asubuhi na mahubiri kwa kiarabu. Anachoongea hata hakieleweki, yaani kelele mpaka nilihama ule mtaa.
 
Kwa asubuhi adhana inatosha haifai kuweka mahubiri au sala kwenye spika na kubughudhi wengine, maana kuna wagonjwa na kadhalika
Kiustaarabu watafutwe wazee waislamu wa eneo husika ili waongee na uongozi wa msikiti hilo lirekebishwe akienda mtu wa dini nyingine inaweza kuleta hali ya sintofahamu
 
Ndio maana kigezo changu cha kwanza ninapo tafuta makazi huwa ni lazima nijiepushe kuwa karibu na msikiti, kanisa, bar, kiwanda, shule, na taasisi yoyote yenye asili ya kelele na watu wengi. Napenda kuishi eneo tulivu lisilo na bughdha ya aina yoyote labda itokee dharura mara moja moja.
 
Mimi sitakereka kama tu ni kumtukuza Mungu. Ni jambo jema, kuliko kelele zingine. Tuache watu wamtukuze Mungu.
 
Mimi sitakereka kama tu ni kumtukuza Mungu. Ni jambo jema, kuliko kelele zingine. Tuache watu wamtukuze Mungu.
Ni sawa kumtukuza mungu ila kiuhalisia adhana inatosha, ila mahubiri kwenye spika alfajiri hiyo siyo sawa, mimi naamka kusali alfajiri ila kama mtu mwingine kapumzika kwa sababu moja au nyingine sitakiwi kumbughuzi
 
Au ile wakisema kitanda chako ndiyo kaburi lako 😅😅😅😅. Yes nimekuelewa mahubiri ya sauti kwa dini zote. Yanawakera wengine. Labda warekebishe hilo, ibaki kengele ya kuita waumini Kanisani, Adhana ya kuamsha waumini waende Msikitini inatosha. Nakubaliana nawewe Mkuu incharge
 
Exactly maana mtu huna hili wala lile unasikia kitanda chako ndio kaburi unaachaje kuweweseka asubuhi subuhi😆😆😆
 
Inategemea na msongo wa mawazo wa mtu. Mbona wengine wapo jirani na misikiti na hizo adhana haziwaamshi?
Japo kiuhalisia,ile ya alfajiri ilitakiwa iondolewe,maana kama makanisa yanatakiwa soundproof,na misikiti inahusika
 
Wakati huo majini na yenyewe ndio yanakurupuka kuwahi salah fajr
 
Au ile wakisema kitanda chako ndiyo kaburi lako 😅😅😅😅. Yes nimekuelewa mahubiri ya sauti kwa dini zote. Yanawakera wengine. Labda warekebishe hilo, ibaki kengele ya kuita waumini Kanisani, Adhana ya kuamsha waumini waende Msikitini inatosha. Nakubaliana nawewe Mkuu incharge
Kengele ya nn mtu hajuiii kama anatakiwa aende kanisani
 
Mi hata kuwasikiaga siwasikii nnavyolala kama pono
Na niko karibu na misikiti mi2 wa sunni na shia
 
Back
Top Bottom