Sio lazima uende CHADEMA ili kuwa mpinzani, jipenyeze kwenye mifumo yao kama Magufuli halafu badili uliyokuwa unaona si sawa

Mfano wa Magufuli sio sahihi hata kidogo. Hakukaa ndani ya CCM na hasa katika ubunge kwa miaka mingi kiasi kile ili apenyeze mabadiliko yoyote ndani ya mfumo. Alikuwa part and parcel ya mfumo wa CCM na alishiriki kupitisha uozo wote uliojiri tangu awe bungeni.

Pili, katika mfumo wa CCM tulio nao, ni Rais wa nchi pekee ndiye mwenye uwezo na/au kauli ya mwisho katika kufanya mabadiliko yoyote ndani ya serikali na nchini kwa ujumla. Wengine wote ni “wasindikizaji”.

Unaposhauri mtu ajiunge na CCM ili kuleta mageuzi akiwa “ndani ya mfumo” basi sisitiza pia ahakikishe anakuwa Rais wa JMT - kama alivyokuwa Magufuli. Nje ya uRais atarajie kuwa chawa wa Rais atakayekuwepo madarakani.

Halafu Magufuli hakuleta mabadiliko yoyote ya msingi katika mfumo. Mfumo wa utawala wa CCM ulibaki vile vile ulivyokuwa kabla na ndio uliomuwezesha SSH kudandia uRais kirahisi kweli kweli (kama kumsukuma mlevi vile!😅).

Alichofanya Magufuli ni “ujasiri na uthubutu” wa kuweka pembeni utwalala wa katiba na sheria na kutanguliza “uzalendo” ili kufanya mambo “makubwa” kwa maendeleo ya taifa. Mambo kama (hususan) miradi mikubwa ya kimkakati, kulinda rasilimali, na kupambana na mabeberu na vibaraka wao nchini. Ndivyo, wafuasi, waumini na wapenzi wa Magufuli wanavyomtambua. Ndiyo legacy yake.

Mleta mada jua kazi ya kuleta mageuzi katika nchi hii si ya kitoto. Kenya wamemwaga damu sana kufika hapo walipo na bado mapambano yanaendelea. Ndivyo ilivyo duniani kote. Hata USA wanapambana hadi leo kuhakikisha utawala wa katiba na sheria unakuwepo nchini. January 6 2021 pale Capitol hill, damu ilimwagika.
 
Chawa wa shetani Magufuli hawajifichi hata wakivaa ngozi ya kondoo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…