Sio Lazima ufunge ndoa Kanisani au Msikitini. Kwanza huo ni Utumwa

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,153
Reaction score
93,069
SIO LAZIMA UFUNGE NDOA KANISANI AU MSIKITINI. KWANZA HUO NI UTUMWA.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Kitendo cha kuona ni lazima ufunge ndoa Kanisani au msikitini ujue bado kuna mambo huyajui kuhusu kiitwacho dini. Ujue wewe ni Mtumwa unayehitaji ukombozi.

2. Ukiona unamawazo kwamba ndoa takatifu sijui halali ni Ile ya kanisani au msikitini. Ujue wajanja wamefanikiwa kukuweka nyavuni. Kufunga ndoa kanisani au msikitini haiifanyi ndoa hiyo iwe takatifu au halali.

3. Sababu kubwa ya ndoa za msikitini au Kanisani hazipo kwaajili yako bali kwaajili ya Kanisa au msikiti.

4. Unapofunga ndoa msikitini au Kanisani ni mbinu inayotumiwa na dini kukufunga mnyororo wa utumwa na wao kujipa uhakika wa ongezeko la wateja(waumini) ambao ni watoto mtakaowazaa.
Kwani ukifunga ndoa ya kiislam automatically watoto mtakaozaa watakuwa waislam. Halikadhalika katika ukristo.

5. Viongozi wa dini wanapohamasisha ufunge ndoa ya kidini lengo Lao halipo kiroho kwamba sijui utanufaika na Baraka za Mungu. Sio Kweli. Ni wanataka uhakika wa wawaumini.

6. Ndoa inahusu watu wazima wawili, mwanaume na mwanamke waliopendana, wakakubaliana, wakapeana terms ambazo wataziishi. Kisha wakaamua kuishi pamoja na kufanya maisha pamoja.

7. Washiriki wengine ni wazazi wa pande mbili. Hawa wanapewa taarifa tuu kama ishara ya heshima. Nao watatakiwa kuheshimu uchaguzi na maamuzi ya watoto wao. Wazazi hawana mamlaka ya kuamua mahusiano ya watoto wao. Kumaanisha hawana uwezo wa kubariki au kulaani mahusiano ya watoto wao.

8. Hivyo, mahusiano ya ndoa ni ya watu wawili. Wao ndio wana uwezo wa kuyabariki au kuyalaani kwa matendo yao jinsi wanavyohusiana, wanavyojiheshimu, uadilifu wao.

9. Unapooa au kuolewa, hakuna MTU yeyote anayetakiwa kukupangia ndoa na familia yako iweje.

10. Sijui mchungaji kasema hivi. Sijui sheikh kasema hivi. Sheikh akaseme kwa mkewe huko. Mchungaji akasema kwa mkewe huko. Kila nyumba ina taratibu na culture zake.

11. Unayo hiyari na sio lazima kutafuta mshauri au mtu wa karibu kukusaidia katika ushauri wa mambo ya kifamilia. Unaweza kumchagua Mchungaji au Sheikh ndio. Lakini wao ni washauri tuu na ushauri wao hauhusiani na mamlaka yoyote juu yako.

12. Kuishi na mumeo/mkeo bila kufunga ndoa ya kanisani au msikitini ni Maamuzi yako. Ni ndoa halali na nzuri.

13. Unaweza kuwa na mkeo na mumeo ambao hamjafunga ndoa za kidini na mkaishi vizuri na matendo yenu yakabariki maisha yenu. Mkafanikiwa na watoto wakawa na maadili.

14. Maadili ni Jambo muhimu kwenye jamii. Zipo sehemu nyingi za watoto kufunzwa maadili.

15. Lakini Primary school ya maadili ni nyumbani, wewe na mkeo/mumeo ambao hapa kwenye maadili mtashiriki kwa watoto sehemu kubwa Sana mkiwa I) Walimu wa Maadili kwa watoto,
ii) Walimu wa Stadi za maisha kwa watoto kama kazi za mikono, uzalishaji n.k.
iii) Walimu wa Mahusiano na ndoa kwa watoto wenu. Kwani wao watakuwa wanajifunza kupitia kwenu.

Ni makosa watoto wakishakuwa wakubwa ati wanaenda kufunzwa na wazazi wengine ambao hawakuwazaa kuhusu mahusiano ya ndoa na familia.
Mwenye jukumu hilo ni wewe mzazi.

iv) Kuwafunza Imani ya Mungu na sio Dini.
Watoto hawapaswi kujitambulisha kwa dini zilizoundwa kwa malengo ya kibinafsi, kibiashara na kisiasa.

Baba na mama ndio mna jukumu la kuwafundisha watoto Imani ya Mungu(UTU). Na hiyo sio lazima awe mkristo au muislam au dini yoyote.

16. Mtoto afundishwe kuwa sio Lazima awe dini fulani ndio amuabudu Mungu. Nope! Huo ni uongo na ulaghai. Mtoto afundishwe maisha yake yote ya Kila Siku ni ibada. Kadiri aishivyo kwa kutenda mema kwake, kwa watu na viumbe wengine hiyo ni Ibada kwa Mungu aliyemuumba.

17. Mtoto na mtu mzima ana hiyari ya kuchagua Dini ambazo zipo nyingi kama sehemu ya jumuiya za kijamii kwaajili ya kubadilishana mawazo ya kimaadili, na kushiriki kijamii kama ambavyo angeweza kuchagua Club ya mpira.

18. Mtoto lazima ajue Imani zipo mbili tuu. imani ya uovu/Giza, na Imani ya Wema/nuru ambapo kupitia Imani hizo wanadamu wakaunda Dini zao kulingana na tamaduni na nyakati.

Mimi kufikia hapo sina la ziada. Nawatakia sabato Njema.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
18. Mtoto lazima ajue Imani zipo mbili tuu. imani ya uovu/Giza, na Imani ya Wema/nuru ambapo kupitia Imani hizo wanadamu wakaunda Dini zao kulingana na tamaduni na nyakat

100%
 
Na imani ya uovu ni rahisi sana kuitambua, ni kumwonesha CCM ilipo tu
 
CCM KAMA IMEKAA HAPO MIAKA 60 UJUE AKILI KUBWA IMETUMIKA

EBU ANGALIA AKILI ZA WATU WANAOPAMBANA NA CCM ILE KUELEKEA 29/10

Screenshot_20251220-071210.png
 
Uzi wa moto huu
 
Mkubali tu, Waislamu tumewatoa ushamba, na ndoa ya mkeka
Watu hawazidi watano na ndoa inafungwa, kwisha habari yake
 
Utter Rubbish. Kama huna mada kausha tu acha siku ipite.

Hakuna tuzo ya kandika sana, hizi zingine ni pumba tu maana zinaongia ku criticise imani na tamaduni za watu
 
Hakuna tuzo ya kusoma sana hasa kile unachoona ni pumba.

Sio Kila mada ya kusoma au kukomenti hasa unayoona ni pumba au ambayo hauko interested nayo.

Utamaduni wako sio utamaduni wangu.

Utamaduni wangu haukatai criticisms kama wako unakataa pita kimyakimya.
 
Dunia huru hii, kila mtu afunge ndoa pale anapoona nafsi yake inafurahia.

Kuna wale wa kwenda kanisani, msikitini, nyumbani, au popote. As long as you have peace of mind and you're happy, my friend go for it. Maisha yetu ni mafupi sana, kuanza kupangiana namna gani mtu afurahie mda mchache aliopewa hapa duniani ni kumkosea.

Imagine kuna ndoa na sherehe zinacost 100m, pesa nyingi sana hii, na baada ya two weeks watu wamepigana chini, the question is, did it make them happy? If the answer is YES, let them enjoy!!
 
Back
Top Bottom