Sio lazima useme kwamba ulisota sana kwenye maisha ili kutu-motivate

Sio lazima useme kwamba ulisota sana kwenye maisha ili kutu-motivate

Utajiri unatafutwa sasa inategemea unautafutaje. Uamue kuwa wa mjini au wa shambani. Kutumika au kutumia, ni wewe tu.
 
Hata Mo Dewji anapenda kuonekana amepambana sana. Hakuna MTU asiyependa kuona juhudi zake zinakuwa appreciated.

Mo Dewji ukimwambia Mali zake za urithi hapendi kabisa.

Kina Drake hawakutoka maisha magumu, lakini wanapenda kuonekana hivyo mpaka ana ngoma yake ya "Started from the Bottom, Now We are here"
Inaweza ikawa kweli wanatoka familia za kishua lakini ule ushua hawakutafuta wao wazazi ndo wameutafuta ishu inakuja kwenye kuendeleza huo ushua inabidi utoe appreciation kidogo

Huyo drake mafanikio aliyoyapata ni juhudi zake na sio familia yake na nyimbo za drake ndo zinazoskilizwa na kupendwa na watu so hapo huwezi sema familia imembeba




Kuna watoto wangapi wa kishua wameshindwa kuendeleza mali walizoachiwa na wazazi wao?.. wapo wengi sana mfano ni dogo aliyeuza V8 la marehemu baba yake kwa milioni 20 ili akale bata
 
Matajiri wa bongo ni ukakasi mtupu. Haitoshi kusema wapo walioanzia chini, kufanikiwa kutoka kwenye familia yenye ukwasi si dhambi. Ila kwa Tanzania tukiamuangalia Diamond hata alivyoanza tu muziki nyimbo ya kwanza mpaka aliyotoa wiki mbili zilizopita unaona ni fursa tosha, unaona mafanikio aliyonayo.

"Ukitaka kuwa tajiri fanya peke yako, ila ukitaka mafanikio makubwa fanya na wenzako".
 
Hard work + God or Ndumba = success no free boti
Smart work + few planned simple actions executed consistently everyday without divergence i.e you're objective to your proven planned of actions that in long run will put odds of your success to your favor / repeatable process executed tirelessly = success
Sio hard work Mana baamedi na wafanyakazi wa vibarua viwandani Kama kwa mo na baresa wanafanya kazi kwa bidii wanapumzika nusu saa ya chakula tu Ila sio matajiri.
You've to work smart na sio boast to work hard ,you can leverage on others time,money and nguvu zao sio uje hapa kujitapa kuwa nilikuwa nalala nje kwenye makalvati Mara nashindia mkate mmoja na maji siku nne.


Lazima uwe smart kichwani.
Sikilza mie huwa Naona binadamu hatuna tofauti na wanyama wengine wa porini. Mana wanakulana na ivyo ivyo binadamu tunakulana. Wazungu wametula wametuibia Mali zetu,hata sie serikali Ni kikundi Cha watu wachache mno hawazidi watano Ila wanakula watanzania wote ,
Ni Kama chui anatawala nyumbu na anatumia nyumbu hao hao kuwatawala wengine na kuwala Kama ambavyo Askari anatumiwa kutudhibiti sie ili tuliwe na wachache juu.
 
Kwenye ahadi za mwanaCCM kuna ila inayosema, fitina kwangu mwiko na nitakuwa mkweli daima. Nikiwa kama mwanaCCM mwenye kadi iliyolipiwa ada nakataa kabisa mambo ya kinafiki na kudanganyana.

Miaka ya hivi karibuni kumejitokeza watu wengi sana wahamasishaji wa mafanikio (Motivational Speakers) ambao naona wanachofanya ni jema sana na ni msaada kwa nchi. Ila pia kumejitokeza mambo mengi yenye ukakasi kwenye shughuli za hawa watu.

Wengi wao pia ni jobless wanaoongea kwa kukopi wahamasishaji wa marekani hali ambayo inakosa uhalisia kwa mazingira ya nchi yetu. Hali ya maisha, utamaduni na mfumo wa maisha ya Tanzania una tofauti kubwa na kule USA hivyo mhamasishaji wa USA hawezi kuwa sawa na wa Tanzania.

Sasa shida inakuja mhamasishaji anapokuja na maneno ya kina Kiyosaki, Ben Carson na kuwaambia vijana wa Nanjilinji. Mwisho wa siku inakuwa sio hamasa bali kuwavuruga zaidi vijana.

Kilichonisukuma zaidi hadi kuandika uzi ni hii tabia ya kila Motivational Speaker kudai alipitia maisha magumu sana hadi kufika alipofika.

Tena wanaokera zaidi ni wale ambao kiuhalisia bado wana maisha magumu na kujikweza. Nitatoa mifano michache ya watanzania maarufu ambao motivation zao zimejaa utata na kukosa uhalisia.

1. MAJIZO: Huyu bosi wa EFM huwa anadai alikuwa anakosa hata hela ya kula enzi akiwa DJ ila akapambana na kufungua redio. Nikipiga thamani ya uwekezaji wake pale EFM na muda aliotumia kutoka U-DJ hadi kuwa mmiliki wa redio kubwa nchini hesabu zinakuwa zinakataa. Na kama ingekuwa hivyo basi Aboubakar Sadik aliyekuwa nae Kwafujo DJs angekuwa nae kashafungua redio au kitega uchumi kikubwa.

2. FRED VUNJABEI: Huyu kijana nae analeta ukakasi sana. Anadai ELIMU tu alichopewa na baba yake ambaye pia ni mfanyabishara mwenye mafanikio kwa ngazi ya Iringa. Lakini katika hali ya kushangaza anatuambia kabla ya kuuza nguo alikuwa mwajiriwa kama mhasibu huku akianza biashara za kwenda China wakati akiwa mwajiriwa. Pia anatuambia alishawahi kuwa muuza magari na kusafiri nchi nyingi. Katika hali ya kushangaza zaidi anadai alikuwa na mtaji mdogo sana ikabidi amchangie rafiki yake aanze kwanza biashara ambaye baada ya kufanikiwa ndo akampa Fred 20m. Huyu kijana nae aachane na mambo ya kusema alipambana sana.

3. MABINTI MAARUFU WENGI; Hili group lina watu wengi ndo maana nimeona niwataje kama group. Wengi wao wanashinda hotel za kitalii wakila bata na kuudanganya umma kwamba wamepambana sana kufikia hapo.

Nashauri Motivational Speakers wakaiga mfano wa Sugu, Mzee Mtei, Marehemu Mengi na Ruge ambao stori zao zimejaa uhalisia na kweli wanahamasisha.
Weye nae una uelewa mdogo sana! Hata Prince Hurry kapitia wakati mgumu pale Bakhngham Palace! lkn leo atakwambia yuko vizuri huko Canada!! kwa jinsi ulivyo wewe huy hutamwamini kuwa alikuwa na shida pale!

Baba yangu alikuwa na Ma Bus 200, lkn nilikuwa siana raha nayo!! japo hela ilikuwa si tatizo, kwangu mpaka pale nilipo soma sana ndo ilikuwa raha yangu! kwa hiyo usihukumu watu kwa jinsi ulivyo weye! Rudi drsasni!
 
Hawa matajiri wa bongo kama fred, majizzo na wengine huwa hawanipi hamasa...kuna mkono au msaada wa mtu uliwabeba ndo wakafika hapo si hivhivi.

hasahasa majizzo nasikia ni wale jamaa wapenda rainbow
Majizo nae ni mpenda Upinde? (Rainbow)🤭🥱

kwahyo anapinda au anapindwa?
 
Wazungu wametula wametuibia Mali zetu,
Huu nao ni ujinga wa kiwango cha lami!! well!! hao wazungu wamekula mali gani zenu/zako??...km ni Almas! hamjui thamani ya zenyewe hata cha kuzifanyia ni wao ndo wamewafundisha! km unajua nitajie fasta hapa!

Dhahabu, NUCLEAR, kahawa, Mkonge nk Au....hata wakiwaachia mtazifanyia nini?? OK! Nyerere kawapiga beat wazungu weee!! eti wasije na kweli hawakuja,

Sabuni Bia tu zikawa shida, Migodi ilikaa tu km ma pori, mkafuria Magwanji ya Mwanza leo mnajiona wajanjaaa! mlipo koma kwa kukosa je si mliwaita wenyewe waje kuwasaidia wajamaeni?? au mmeshiba sasa mmesahau??

na siku hizi hawataki kuja kuwekeza kwa sababu mnawaita majina mabaya mara mkoloni, Beberu, gabachori wamerudi! nakwambia mtakoma njaa yake safari hii mtawapigia magoti! si unaona Mlimani city ...wanaondoka??

au huna macho?? ! uone mnavo ringia kufanya shoping pale! sasa itakuwa ni mwendo wa kariakoo tu! endeleeni kuwaita wezi uone km watakaa!! Mtakulana km matahaira!! wataenda zao Nairobiii! na south tu!

hapo hata chungulia tu, noo! uone km utalii haujafa!! ni Mwafrica gani anafanya utalii wa tija mbugani zaidi ya hao unaowananga??...wabongo Mtakufa njaaa!! nyie haya weee!!

Tatizo lenu weusi urafi tu na uchoyo mnataka muwe km wao wkt hamna akili hizo!..tulieni basi hamtaki mnaanza mara hatufungamani, mara kipindi cha mpito! usiwaponze wenziooo!

Si ndo nyie mliupinga ujamaa wa Nyerere nyie ?? mkatamani Ubepari?? Ok! fanyeni wenyewe huo Ubapari sasa!...hamuwezi ndo km hivi....kushikana wenyewe kwa wenyewe uchawi!

bado kuuana tu sasa ndo mnasubiri, south, DRC wameshaanza! sasa mtu na akili zangu kweli nikae na watu km nyie wa nini??? bora kusepa zangu Ulaya tu!
 
Weye nae una uelewa mdogo sana! Hata Prince Hurry kapitia wakati mgumu pale Bakhngham Palace! lkn leo atakwambia yuko vizuri huko Canada!! kwa jinsi ulivyo wewe huy hutamwamini kuwa alikuwa na shida pale!

Baba yangu alikuwa na Ma Bus 200, lkn nilikuwa siana raha nayo!! japo hela ilikuwa si tatizo, kwangu mpaka pale nilipo soma sana ndo ilikuwa raha yangu! kwa hiyo usihukumu watu kwa jinsi ulivyo weye! Rudi drsasni!
Hatuongelei furaha unayomaanisha wewe. Tubaongelea msoto kuhusu kupata pesa. Elewa mada.
 
Hatuongelei furaha unayomaanisha wewe. Tubaongelea msoto kuhusu kupata pesa. Elewa mada.
Drs la saba C'' !! Narudia tena kwa faida ya watu wote km weye! Msoto wangu na Madaraka Nyerere! kuhusu kupata Pesa, ni tofauti sana na Msoto wako wewe Mwanakijiji wa Wilolesi ya Iringa vijijini kuhusu kupata pesa!!

kunilinganisha smaki/& Madaraka Nyerere! na wewe kuhusu pesa ni Makosa makubwa ya uelewa! ndo maana nikasema kwa msisitizo urudi drsani ukasome zaidi ili ufunguke kimaisha, na

bado nasisitiza utimize hayo km unajipenda lkn! .....na siku isiyo kuwa na tarehe utaja nishukuru! ....lkn inaonyesha Bado ni mzito kuelewa........lkn ndo mlivyo slow learner! na sie wataalam hatuchoki kuwakumbusha!
 
Drs la saba C'' !! Narudia tena kwa faida ya watu wote km weye! Msoto wangu na Madaraka Nyerere! kuhusu kupata Pesa, ni tofauti sana na Msoto wako wewe Mwanakijiji wa Wilolesi ya Iringa vijijini kuhusu kupata pesa!!

kunilinganisha smaki/& Madaraka Nyerere! na wewe kuhusu pesa ni Makosa makubwa ya uelewa! ndo maana nikasema kwa msisitizo urudi drsani ukasome zaidi ili ufunguke kimaisha, na

bado nasisitiza utimize hayo km unajipenda lkn! .....na siku isiyo kuwa na tarehe utaja nishukuru! ....lkn inaonyesha Bado ni mzito kuelewa........lkn ndo mlivyo slow learner! na sie wataalam hatuchoki kuwakumbusha!
Wewe ni mkaguzi wa elimu za watu hapa JF? Hakuna kitu umeandika zaidi ya pumba na majivuno. Kwasababu hapa JF hatujuani baki na mtazamo wako.
 
Kama ni kweli pia hupaswi kusema. Nchi na vijana wa mseleleko
 
Back
Top Bottom