Mi ndio maana nawashangaa sana wanaompa credit Eng. Hersi kuwa ni kiongozi mahiri wakati kwenye administration yake tunaona kuna loopholes nyingi zinazo reveal kuwa he's not good enough to fit.
Lundo la cases za madai kutoka FIFA ambazo 90% zimetokana na kuwavunjia wachezaji mikataba kiholela pasipo kuwalipa stahiki zao.
Tena mostly ya hao wachezaji zilikuwa ni zile sajili za mihemko zenye shabaha moja tu ya kumkomoa mtani wake.
Kupoteza mechi mbili mfululizo tayari uongozi ume lose focus kila mtu kapagawa hakuna anayeamini kuwa wachezaji sio sehemu inayopaswa kuwajibishwa au kulaumiwa kufuatia kupoteza hizo mechi.
Badala yake wamefanya diagnosis wakaona tatizo ni uwanja, lakini wakamjumuisha na kocha kuwa yeye pia naye ni sehemu ya tatizo ya kufungwa mechi mbili.
Sasa angalia inavyoenda kuwa....miezi mitano iliyopita Hersi alinukuliwa kuwa wanamuongezea mkataba kocha wenye maslahi yaliyoboreshwa ili kumfanya azidi kusalia hapo Jangwani.
View attachment 3152818
Maana yake kama hii tetesi ni ya kweli, Yanga watalazimika kutoa pesa nyingi ili kuvunja mkataba na wakati huo huo ukumbuke Victor Osimhen tayari kashinda kesi na hukumu imetolewa kuwa Club haitoruhusiwa kufanya usajili mpaka bwana Osimhen alipwe.