Sio siri tena, Gamondi ameshafukuzwa sijui Yanga wanaficha nini?

Akina injinia wanatafuta kichaka? Gamond amewakosea nini? Au upigaji as well?
Ila kwa upande mwingine wapo sahihi, Gamondi anatabia ya jeuri na dharau na misimamo ya ovyo. Hakuna kitu huwa sikipendi kama kumpanga Azizi Ki anayeruka ruka uwanja hana faida yoyote zaidi ya kupoteza mipira huku mpambanaji Pacome akiwa benchi. Sijui anakomaa na mtu wakati kila mtu kaona ka floppy msimu huu.
 
Watakuwa wamekurupuka sana kumtimua Gamond. Wamechemka sana. Simba wanamgwaya sana huyu mwamba. Viongozi hawajamtendea haki kocha na mashabiki pia. Mechi mbili tu hizi tayari wamekosa imani nae?
 
Unampaje mkono wa kwa heri na bado akaendelea kukinoa kikosi chako? Hersi hawezi kuwa failure wa kiasi hicho kwenye maswala ya management. Gamondi mwenyewe atakuwa mjinga wa kutupwa
πŸ€ͺ
 
Akina injinia wanatafuta kichaka? Gamond amewakosea nini? Au upigaji as well?
Mi ndio maana nawashangaa sana wanaompa credit Eng. Hersi kuwa ni kiongozi mahiri wakati kwenye administration yake tunaona kuna loopholes nyingi zinazo reveal kuwa he's not good enough to fit.

Lundo la cases za madai kutoka FIFA ambazo 90% zimetokana na kuwavunjia wachezaji mikataba kiholela pasipo kuwalipa stahiki zao.

Tena mostly ya hao wachezaji zilikuwa ni zile sajili za mihemko zenye shabaha moja tu ya kumkomoa mtani wake.

Kupoteza mechi mbili mfululizo tayari uongozi ume lose focus kila mtu kapagawa hakuna anayeamini kuwa wachezaji sio sehemu inayopaswa kuwajibishwa au kulaumiwa kufuatia kupoteza hizo mechi.

Badala yake wamefanya diagnosis wakaona tatizo ni uwanja, lakini wakamjumuisha na kocha kuwa yeye pia naye ni sehemu ya tatizo ya kufungwa mechi mbili.

Sasa angalia inavyoenda kuwa....miezi mitano iliyopita Hersi alinukuliwa kuwa wanamuongezea mkataba kocha wenye maslahi yaliyoboreshwa ili kumfanya azidi kusalia hapo Jangwani.

Your browser is not able to display this video.

Maana yake kama hii tetesi ni ya kweli, Yanga watalazimika kutoa pesa nyingi ili kuvunja mkataba na wakati huo huo ukumbuke Victor Osimhen tayari kashinda kesi na hukumu imetolewa kuwa Club haitoruhusiwa kufanya usajili mpaka bwana Osimhen alipwe.
 
Nyie bakini na Mangungu wenu huko shirikisho, Hersi achaneni naye kabisa πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€ Huo mvurugano uliopo Yanga umeuleta wewe au waandishi mataahira wenzenu kina shaffih dauda πŸ˜€ mnahangaika sana kuforce kuilegeza Yanga kwa propaganda uchwara!
 
Mleta uzi Jikite shirikisho, Mambo ya Yanga waachie wenyewe. Huyo Gamondi aliyefukuzwa labda ni wa huko Buza πŸ˜€
 
Wataalamu hii habari ni ya kweli?
 

Attachments

  • Screenshot_20241115_130725_WhatsAppBusiness.jpg
    585.2 KB · Views: 1
jana kuna raia alisema yanga wanacheza na akili za watu sasa aseme hii issue ni kucheza na akili za watu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…