Sio tu Dj Ommy Crazy hata Frida(Queen fifi) na King Smash hawana muda mrefu

Sio tu Dj Ommy Crazy hata Frida(Queen fifi) na King Smash hawana muda mrefu

mayowela

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
2,125
Reaction score
1,753
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia Eat Africa radio na Tv, wamekuwa ni walimu kwa watangazaji wanaotoka pale yaani watangazaji wanatoka wamekwiva ki maadili hadi utendaji.

Lakini ni kama swali najiuliza ni nini kunachowakimbiza hawa watu, ni Mshahara(maslahi), kujuana, unyanyasaji kazini au ni nini ambacho wanakikimbia na wanako kwenda wanakuwa dhahabu.

Orodha ni ndefu ya walioondoka tangu enzi za Bush baby, Steve ka fire, wale naweza sema labda waliona warudi nchini kwao wakaanze maisha ya huko. Hapa kati kati walioondoka ni wengi:
Dj AD aka Mafuvu baby, Anna Peter, Allan Lucky, Michael Lukindo, Sebastian Mwaikambo, Bahati Abdul, hivi karibuni wamepata pigo na si pigo dogo hasa kwa vijana waliowatengeneza kisha wakanyakuliwa ikiwa ni Kenedy the remedy, Dj sinyorita na Mammy Babby mara upepo haujatulia Dj ambae alionekana kuziba pengo la Mafuvu nae kaenda E-fm.

Tar 8 kwenye tamasha la Komaa concert jijini Mwanza alionekana Jukwaani akisimamia shoo kwa wasanii walio alikwa hakuwa mwingine ni Dj Ommy Crazy, ambae kwa muda amekuwa hasikiki redioni (Ea radio) na alikuwa akifanya yake nilihisi jambo ila nikasema acha muda uongee.

My take Ea radio kwa sasa mna Frida au Queen fifi na King smash ni kama hadhina mliobaki nayo ni watu ambao huchoki kuwasikiliza jaribuni kuwalinda kimaslahi na vinginevo waibebe redio, radio inakosa mvuto msipo kuwa makini hao hawana muda mrefu watawapokonya.

Program meneja wa Ea radio naamini atapita hapa.
 
Aiseee hapa kuna ukweli
Mtupu maana jamaa
Pale wanapukutika

Kama njugu na hawaend
Station zingne n efm na
Clouds tu

Ipp n sawa tu na club ya arsenal ambayo kaz yao
N kuwakuza na kuwafundisha
Kaz madogo af wakishajua

Wanashindwa kuwathamin
Na ndo kama hvo wanajichomoa mdogo mdogo
 
frida amani (queen fifi) na king smash nawakubali sana huwa wananifanya niisikilize EA radio sio wale kina nyambua hovyo kabisa...wana mambo ya ukale sana kifupi hawaendi na mazingira ya sasa ya muziki wao wanakomaa na enzi za kina nature wakati zilishapitwa na wakati

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
EA Radio na EATV ni wabinafsi,wanachuki na wanaroho mbaya sana,haswa Dullah wa Planet Bongo na Samwel Misago aka Sammisago na yule Program Manager wao ndio watu wanaohujumu hizi station,ila bila ya hao watu ni station nzuri sana kwa TZ na EA kwa ujumla.UKITAKA KUDHIBITISHA HILO,ANGALIA HAWANA MATANGAZO MENGI NA SABABU KUBWA MAKAMPUNI/TAASISI/WATU BINAFSI WANAONA HAKUNA WATANGAZAJI WENYE KUVUTIA WASIKILIZAJI.Kumbuka Radio/Tv zenye matangazo mengi maana yake zinapendwa na makampuni,na makampuni yanaangalia vipindi au watangazaji wenye kuvutia wasikilizaji/watazamaji pamoja na kusambaa hadi vijijini na mijini.
 
Aiseee hapa kuna ukweli
Mtupu maana jamaa
Pale wanapukutika

Kama njugu na hawaend
Station zingne n efm na
Clouds tu

Ipp n sawa tu na club ya arsenal ambayo kaz yao
N kuwakuza na kuwafundisha
Kaz madogo af wakishajua

Wanashindwa kuwathamin
Na ndo kama hvo wanajichomoa mdogo mdogo
efm tunae mmoja tu huyo dj ommy crazy ila nenda clouds sasa nusu ya watangazaji wao wamewatoa pale
 
EA Radio na EATV ni wabinafsi,wanachuki na wanaroho mbaya sana,haswa Dullah wa Planet Bongo na Samwel Misago aka Sammisago na yule Program Manager wao ndio watu wanaohujumu hizi station,ila bila ya hao watu ni station nzuri sana kwa TZ na EA kwa ujumla.UKITAKA KUDHIBITISHA HILO,ANGALIA HAWANA MATANGAZO MENGI NA SABABU KUBWA MAKAMPUNI/TAASISI/WATU BINAFSI WANAONA HAKUNA WATANGAZAJI WENYE KUVUTIA WASIKILIZAJI.Kumbuka Radio/Tv zenye matangazo mengi maana yake zinapendwa na makampuni,na makampuni yanaangalia vipindi au watangazaji wenye kuvutia wasikilizaji/watazamaji pamoja na kusambaa hadi vijijini na mijini.
iyo redio yao kama huna antena ya maana huwezi ipata zaidi ya chenga tu.... jamaa sijui wamefunga mitambo gani pale
 
Kwangu mimi EATV na EA Radio vituo bora zaidi kwa burudani hapa Bongo. Kile ni chuo kwani wanastahili pongezi wapo very professional. Huwezi kuzuia watu kuondoka ni sehemu ya maisha tu. Wanapita watakuja wengine wananolewa wanaondoka na maisha yanasonga. Wangebaki kina Bush baby pale hadi leo kuna Kennedy the Remy D wasingepata nafasi ya kushaini na kuonekana lulu.
 
Back
Top Bottom