1. Kumfungulia mwanamke garia apandapo au kushuka na kumfunga mkanda kabla ya gari
kuondoka
2. Kumshika mkono kwenye hadhara wakati wa kutembea e.g evening walk au kwenye
ocassion kubwa inatokeaga siku ya harusi tu.
3. Kumsifia pale panopostahili e.g nguo imekupendeza kweli....u look excellent on those
clothes. U had wonderful presentation I rly like it.....
4. Kumpigia simu muda wa mchana kumtakia mlo mwema na kujua siku yake inakwendaje.
Au kumwachia ki-note asubuhi kwenye fridge au nyuma ya mlango chenye ujumbe wa
mapenzi e.g u luk so peaceful, beautiful and at peace when u sleep
5. Kumpa au kumnunulia maua katika vipindi tofauti
1. Kwanza gari lenyewe inabidi ulinunua kabla ya kumfungulia mlango mkeo. Angalia Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wana magari, hata Dar es slaam amapo ni mji mkuu ni asilimia ndogo tu ya wanaume walioa wenye magari hayo. tunaweza kuanza kujua kama utamaduni huo pale tunapoweza kununua magari au pale tunapokuwa na magari ya kutosha
2. Do we have places for evening walk? mimi nakaa manzese aambako kwa mara ya mwisho mtaa ulikuwepo wakati wa mkoloni sasa hivi ni mitaro inayonuka, vibaka, kila siku kuhangaika asuuhi mpaka jioni, where will i get this time for evening walk? why don't i just rest at home?
3. Wake zetu tunawasifia sana, na kumsifia mwanamke si lazima useme unaweza kumsifia kwa wengine au hata kwa vitendo. Mbona huwa tunawasifia sana kuwa wanawake wetu ni hodari zaidi kitandani kuliko wengine. Hata hivyo nguo zetu kama mabaibui au vitenge vyenyewe ni sifa tayari they do not need more sifa.
4. Nyumbani kwangu sina simu, sina uwezo wa kulipia gharama za simu na sina uwezo wa kununua simu ya mkononi. Mke wangu naye ni hivyo hivyo sasa hatuwezi kufikiri hata kupigiana simu kabla ya kununua hizo simu. Kazini kwangu au kazi yangu haihitaji simu, how can i call?
5 How can i buy her flowers wakati kuna bustani kubwa sana ya maua mazuri kuliko ujinga huu wa vimaua vidogo, mke wangu hapendi maua anapenda vitu vingine kabisa, she is not a baby girl she does not like that kind of things. Wakati mwingine ni kama kupoteza pesa kutumia shiling 5000 kununua maua wakati sijui kesho ntakula nini au wakati hata dawa ya mtu sina, leave alobe nauli ya kwenda msikitini.
Ningependa nianze kwanza kujiimarisha kiuchumi haya mambo ni secondary sana, na ni ziada sana. Ni sawa na kumpelekea mgonjwa aliyehospitali kadi ya well wishes ya shilingi elfu 50,000 wakati hata hela ya kitanda hana. Hatuwezi kuiga mambo meingine bila kuangalia hali yetu halisi kimaisha.