Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 11,191
- 35,870
Tukiwa bado tunanukia kinyumbani nyumbani vijana wa form 1, tumetimiza wiki moja au 2 mbili hivi, ilikuwa imefika mida ya kwenda kuchukua msosi wa jioni. Sasa si unajua vyombo tunatunza kwenye matranka so inakubidi urudi bwenini ukachukue.
Ile ndio form 1 tumeingia bwenini kuchukua vyombo, zikaingia njemba mbili ambazo zilionekana ni majamaa ya A-level. Na kipindi hicho njemba ya A-level ilikuwa imekomaa utafikiri graduate wa sasa na kipindi hicho uonevu mashuleni ulikuwa mkubwa mno.
Basi jamaa wakafunga mlango wa bweni na wakaweka sahani mbele wakatuambia madogo ili mtoke humu leo lazima kila mtu atoe shilingi 50, 50.
🤣
Aisee, na jamaa walikuwa kauzu kweli, ilibidi vijana tuanze tu kujichanga kutoa tu, wale ambao walikuwa hawana wakawa wanalia huku wanapigwa biti, jamaa walivyoona wamepata vishiringi shiringi hao wakasepa🤣
Aisee kama wale jamaa leo wako humu JF basi mlitupiga tukio hatari sana 🤣,natumaini hamkuishia kuwa matapeli.