Sioni namna Rais Samia anaweza kuinua uchumi wa Watanzania uliodorora

Sioni namna Rais Samia anaweza kuinua uchumi wa Watanzania uliodorora

kila mtu alitamani mtu wake ndio awe makamu wa rais ila mama amemchagua mpango.....

sidhani kama amekosea, kwani maamuzi ya kumchagua mpango hajafanya peke yake wamekaa vikao vingi na wakuu wa nchi hii na wakubwa wengine ndio wakamjadili na kukubaliana kumpa dhamana mpango.....

kazi kubwa ya mpango ni kufanya kazi kubwa na mama ya kurudisha uchumi na kutengeneza misingi bora ya kiuchumi etc......nafikiri ni mtu sahihi.
 
Ulitaka aje na fikra gani mpya wakati ILANI ya Uchaguzi ni ile ile aliyozunguka kuinadi ktk Uchaguzi Mkuu? Mawaziri ni wale wale ambao aliwateua yeye na Magufuli? Mama yuko vizuri
 
Kwa sasa hakuna mwenye dhamira ya dhati ya kumkomboa Mtz ,Nyerere tu ndio alikuwa na nia ya kulikomboa taifa waliobaki wote wapiga deal..
 
Hapana ebu tutoe mda kweli kazi anayo kwenye uchumi yamevurugwa mengi , mh Rais plus Vp wake, ongezeni Tim nzuri ya ushauri kwenye Mambo ya uchumi, tz inawatu wazuri mfano wakina prof lipumba n.k bila kujali vyama dini ,na mh shaurika Mambo yatakaa vizuri maana do
 
Mr Asp. Hali ni mbaya kwa watu Ambao hawana cha kufanya. Wengi Watanzania walikua Mission town Enzi za Jakaya.

Utawala wa JP uliendana na watu kufanya kazi na sio Udalali Brother.

Huna kazi mfumo wake ulikulazimisha ufanye kazi ili upate fedha na sio Fedha za Bure bure. Na ukwepaji wa Kodi.

Nchi zote Ambazo Ninyi mnazishabikia has a za Ulaya Kazi kwao na Kodi ni wajibu na sio hisani ya wanasiasa Uchwara wanaowadanganya watu kwamba mzunguko Umekua mdogo kwa sababu Serikali imebana Matumizi.

Nikweli Serikali yeyote Makini Au Baba makini ni lazima Adhibiti Fedha ili Kujenga Uchumi imara.

Huwezi kuendelea kama ujidhibiti na kuheshimu fedha unayoipata.

Watu hawajui kwamba Serikali ni kama baba anae hudumia familia, sasa kama baba asipokua na udhibiti wa Kipato chake akaachia fedha Watoto wanywee gongo mwisho wasiku baba utakua maskini na utapoteza Watoto.

Hivyo Ndugu Magufuli. Alitujenga sana kwenye kufanya kazi na hii imetujengea tabia hiyo. Hatutaki vya bure bure na udalali hapa Mjini.

Na mama Akandamizie pale pale watu wafanye kazi hakuna Pesa za Bure bure. Kama hufanyi kazi Mzunguko wa Hela utausikia kwenye Bomba Mr ASP.
 
Mnaanza ngojera zenu , haya tajeni basi mlitaka aweke akina Nani kwenye Baraza la mawaziri ?? Akina nchimbi na January?
Tulitaka amweke yoyote yule anayeona anafaa kuwa kwenye serikali yake LAKINI tupate muono (vision) ya kule anataka kutupeleka, tutajua hilo kwa kumwangalia huyo mteule wake.
 
Sera zake kiuchumi zilikuwa ngumu na hatari, kuendelea kuzibeba zilikuwa ni mzigo mzito kwake na kwa taifa, huenda hata Magufuli mwenyewe ipo siku huenda angechoka na kukubali yaishe, lilikuwa ni suala la muda tu.

Tujipe muda lakini tusichoke kuchambua!
Hiyo sentensi ya mwisho.
 
Kwangu mimi shida siyo baraza shida ni sera zitakazoongoza baraza.

Kuna baadhi ya vitu (sera) zikitekelezwa hilo baraza litatukuzwa.

Mfano kushirikiana na sekta binafsi, kodi rafiki, kukata doubl tax, kupanua wigo wa vijana kujiajiri, kipaumbele kiwe kilimo (siyo viwanda) katika kuelekea uchumi wa viwanda hua kinaanza kilimo n.k. so tuwe na subira kidogo.
 
Ni vile tu kulikuwa na kutishana na kupikwa kwa takwimu lakini hali yetu kiuchumi sio nzuri

Miradi mikubwa haijakamilika
Wastaafu mafao yao kizungumkuti
Watumishi mishahara mwaka 6 sasa
Biashara nyingi zimefunga wawekezaji wamepungi
Wakulima vilio
Deni la Taifa nimekuwa kubwa

Namuonea huruma sana Mama, kapokea mfupa mgumu mno, sijui ataanzia wapi. Kila la kheri.
Asante ndugu yangu kwa kuliona hilo. Kwenye uchumi, Mama Samia ana mlima mrefu wa kuupanda, lakini anataka kujifanya kama haoni vile, wakati mlima upo mbele yake.
 
Kwa upande wangu mimi naona ameanza vizuri, maana tukianzia na baraza la mawaziri alilolitangaza leo binafsi nina imani nalo kwa sababu kubwa moja ya kwamba mafanikio ya serikali ya mtangulizi wake kwa kiasi kikubwa yametokana na hili baraza alilolitangaza leo. Hivyo kwa upande wangu naona amefanya jambo la busara kuanza nalo hili baraza la mawaziri.

Kwenye upande wa utekelezaji wa miradi mikubwa kama SGR bado Nina imani kuwa atafanikiwa, na hii inatokana hasa na aina ya watu wanao mzunguka kwa tukianza na Mh.makamu wa rais kwangu mimi ninamuangazia kama mtu aliye tulia na asiye na papala kwenye maamuzi. Na ni dhahiri kuwa atamshauri vizuri kwenye utekelezaji wa hiyo miradi maana kwanza na yeye My.makamo wa rais ni mtu ambaye anataaluma kubwa kwenye masuala ya uchumi.

Lakini pia hata kwenye usimamizi wa fedha za serikali na utendaji wa shughuli mbalimbali za serikali bado ni imani Mh.Majaliwa ingawa bado haja mthibitisha kwamba ndiye atakae kua waziri wake mkuu lakini nadhani atamrudisha kwenye hiyo nafasi yake.

Kiujumla kwenye kasi ya ukuaji wa uchumi, ukiangalia mtangulizi wake kwenye miaka yake yote aliyoongoza uchumi ulikua ukikua kwa kasi ya zaidi ya asilimia 6.9 na hii ilitokana na utekelezaji wa miradi mikubwa nchini. Na bila shaka na yeye ataiendeleza hii miradi hivyo nategemea kuona kasi ya ukuaji wa uchumi ikizidi kuongezeka katika kipindi cha utawala wake.

Binafsi nina imani kubwa na utawala wake. Changamoto ninayoiona kwenye utawala wake ni jinsi ambavyo watu au watumishi watakavyokua wanamuangalia hasa kwenye maamuzi atakapo kua anachukua maamuzi magumu yenye kubeba mustakabali wa nchi moja kwa moja, mfano namna ambavyo atakabiliana na ugonjwa wa korona maana karibu nchi zote za Afrika Mashariki zimeshaanza kugawa chanjo ya korona. Je, na yeye akisema akubari chanjo watu watatoa maoni gani hasa ukiangalia mtazamo wajamii yetu kwenye maamuzi yanayotolewa na jinsia ya kike kwenye maamuzi magumu kama hayo. Kwa hiyo binafsi mimi naona hiyo ndy changomoto kubwa atakayokutana nayo.
 
Tupangie wewe baraza..kumbuka mawaziri ni lazima wawe ni wabunge..Twende kazi tupangie baraza hilo.
 
Ilitakiwa na sura za mawaziri ziwe mpya ,
Lakini mkuu nafanikio ya serikali iliyopita si yalitokana na hawa mawaziri aliowarudisha tena, binafsi sikuona haja ya kubadilisha mawaziri ateue tena wapya.
 
Magufuli hakuwa na nidhamu ktk matumizi ya fedha za serikali.

Angekuwa na nidhamu asingefanya matumizi ya hovyo kama ujenzi wa uwanja wa ndege chato, trillion 2 kununua midege toka kwa mabeberu, kuhamia dodoma, etc.

Hebu tueleze kuhamia Dodoma kuna faida gani zaidi ya kuonyesha ufahari kwamba tunaweza? Kwanini asingeelekeza fedha hizo kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, au viwanda?

Magufuli alikuwa na spidi nzuri ktk kukusanya fedha, lakini alikuwa na spidi kubwa zaidi ktk kutumia fedha vibaya.
 
Tumpe muda samia
Na mimi nasema tumpe muda, lakini tusiache kumchambua!
Kwa mfano tumempa muda wa wiki mbili ili atengeneze serikali yake, na ameunda serikali yenye watu wale wale, kwenye nafasi zile kwa 95%.
Unategemea nini tofauti hapo?
Kwanini tusimchambue?
 
Back
Top Bottom