Hana vision wala Jipya polite.Mmh mkuu mbona mapema sana kuitana majina mabovu hivyo?
Amini nakuambia, kile udhaniacho ndio Kumbe sicho na kinyume chake.
Mimi si mfuasi wa hivi vyama lakini kwa huyu mama naamini kutakuwa na unafuu mkubwa sana kimaisha na kimaendeleo.
Watanganyika wanyanyaswe na wanzanzibari? mbona mtatafuta kila sababu. 😂😂Wazanzibar inawezekana wakanufaika na Muungano kiliko kipindi kingine chochote kile. Hii inaweza kupeleka watanganyika kunyanyaswa Sana katika hii nchi. Time will tell
Yaan watu 60m tukanyanyaswe na watu 1.5m ???Wazanzibar inawezekana wakanufaika na Muungano kiliko kipindi kingine chochote kile. Hii inaweza kupeleka watanganyika kunyanyaswa Sana katika hii nchi. Time will tell
Wabongo tuko vizuri sana kwenye kukosoa na kulalamika. Dunia nzima sidhani kama kuna mtu anatuweza kwa hili..Shida ni kwenye kutoa masuluhisho na mawazo mbadala sasa. Hapo utalia maweee !!!Unamshauri afanye nini mkuu tufunge uzi?
[emoji3581]Yuko njia sahihi wasiwasi wako tu, timu ya mpira inaweza kucheza kiwango flani chini ya Kocha flani na vilevile kiwango kikabadirika akija kocha mwingine
Hahahaha, wazo zuri sanaUnamshauri afanye nini mkuu tufunge uzi?
Huyu mama ni kama debe tupu, sijui hata kama anajua anatupeleka wapi.
Miminaichukia mno ccm lakini Samia atafanya vyema sana kuliko hayati.Tanzania kwa sasa ina serikali mpya ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu baada ya kifo cha Rais Magufuli.
Kwa sasa hatuna sababu nyingine yoyote ya kusubiri kuufahamu utawala wa Samia Suluhu utakuwaje, maana sura nzima ya serikali yake iko tayari.
Utawala huu mpya kwenye uchumi una mtihani mkubwa sana wa kuendeleza yale yaliyofanywa na Magufuli sera (ikiwa tunaamini Magufuli alifanikiwa kiuchumi) ama kupindua yaliyofanywa na Magufuli ili kufanya upya kisera (ikiwa tunaamini Magufuli alishindwa kiuchumi).
Vyovyote atakavyochagua Rais Samia Suluhu, sioni namna yoyote ile anaweza kufanya kitu chenye mafanikio makubwa ya kiuchumi.
Kwa mfano, kama Samia ataamua kutaka kuvaa viatu vya kiuchumi vya Magufuli (kuwakazia mabeberu, kujenga miradi mikubwa ya miundo mbinu pasipo uwiano wa pesa za kibajeti, kununua ndege, kuibana sekta binafsi nk) bila shaka atashindwa vibaya. she will underperform!
Kwa sababu, ni Magufuli pekee yake (kama alivyokuwa akiamini hivyo) aliyekuwa na ujasiri wa kiwango kile kufanya vile. Sera zake kiuchumi zilikuwa ngumu na hatari, kuendelea kuzibeba zilikuwa ni mzigo mzito kwake na kwa taifa, huenda hata Magufuli mwenyewe ipo siku huenda angechoka na kukubali yaishe, lilikuwa ni suala la muda tu.
Upande mwingine, kama mama ataamua kubomoa sera za kiuchumi za Magufuli ili aanze upya kwa kujenga za kwake, bila shaka angepaswa kwanza kuja na watu wapya kabisa kwenye serikali yake. Yaani kuanzia makamu wa rais, waziri mkuu na angalau nusu ya baraza lake la mawaziri lingekuwa ni sura mpya kabisa katika serikali yake.
Kitendo cha zaidi ya 95% ya baraza la mawaziri kuwa watu wale wale tena katika nafasi zile zile ni kiashirio kikubwa kuwa mama Samia Suluhu hana mawazo mapya wala fikra zozote pana nje ya kile kile kilichokuwepo.
Tujipe muda lakini tusichoke kuchambua!
Heri mama kuliko hayati.Huyu mama ni kama debe tupu, sijui hata kama anajua anatupeleka wapi.
Hakuna uchumi uliodorola kwa wanaojituma. Fanyeni kazi acheni deals mtafanikiwaTanzania kwa sasa ina serikali mpya ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu baada ya kifo cha Rais Magufuli.
Kwa sasa hatuna sababu nyingine yoyote ya kusubiri kuufahamu utawala wa Samia Suluhu utakuwaje, maana sura nzima ya serikali yake iko tayari.
Utawala huu mpya kwenye uchumi una mtihani mkubwa sana wa kuendeleza yale yaliyofanywa na Magufuli sera (ikiwa tunaamini Magufuli alifanikiwa kiuchumi) ama kupindua yaliyofanywa na Magufuli ili kufanya upya kisera (ikiwa tunaamini Magufuli alishindwa kiuchumi).
Vyovyote atakavyochagua Rais Samia Suluhu, sioni namna yoyote ile anaweza kufanya kitu chenye mafanikio makubwa ya kiuchumi.
Kwa mfano, kama Samia ataamua kutaka kuvaa viatu vya kiuchumi vya Magufuli (kuwakazia mabeberu, kujenga miradi mikubwa ya miundo mbinu pasipo uwiano wa pesa za kibajeti, kununua ndege, kuibana sekta binafsi nk) bila shaka atashindwa vibaya. she will underperform!
Kwa sababu, ni Magufuli pekee yake (kama alivyokuwa akiamini hivyo) aliyekuwa na ujasiri wa kiwango kile kufanya vile. Sera zake kiuchumi zilikuwa ngumu na hatari, kuendelea kuzibeba zilikuwa ni mzigo mzito kwake na kwa taifa, huenda hata Magufuli mwenyewe ipo siku huenda angechoka na kukubali yaishe, lilikuwa ni suala la muda tu.
Upande mwingine, kama mama ataamua kubomoa sera za kiuchumi za Magufuli ili aanze upya kwa kujenga za kwake, bila shaka angepaswa kwanza kuja na watu wapya kabisa kwenye serikali yake. Yaani kuanzia makamu wa rais, waziri mkuu na angalau nusu ya baraza lake la mawaziri lingekuwa ni sura mpya kabisa katika serikali yake.
Kitendo cha zaidi ya 95% ya baraza la mawaziri kuwa watu wale wale tena katika nafasi zile zile ni kiashirio kikubwa kuwa mama Samia Suluhu hana mawazo mapya wala fikra zozote pana nje ya kile kile kilichokuwepo.
Tujipe muda lakini tusichoke kuchambua!
Huyu kafeli toka kwa Mpango ndiyo maana mi nilikataa toka mwanzo kuwa huyu hatafanya chochote cha maana.