Sioni namna Rais Samia anaweza kuinua uchumi wa Watanzania uliodorora

Jamani tumuamini Rais wetu. Nina muamini na matumaini juu yake.

Waziri asipowajibika ipasavyo atawajibishwa wasiwasi wa nini.
 
Mmh mkuu mbona mapema sana kuitana majina mabovu hivyo?

Amini nakuambia, kile udhaniacho ndio Kumbe sicho na kinyume chake.

Mimi si mfuasi wa hivi vyama lakini kwa huyu mama naamini kutakuwa na unafuu mkubwa sana kimaisha na kimaendeleo.
Hana vision wala Jipya polite.

Ni kupuyanga tu, bora kumekucha.
 
Wazanzibar inawezekana wakanufaika na Muungano kiliko kipindi kingine chochote kile. Hii inaweza kupeleka watanganyika kunyanyaswa Sana katika hii nchi. Time will tell
 
Wazanzibar inawezekana wakanufaika na Muungano kiliko kipindi kingine chochote kile. Hii inaweza kupeleka watanganyika kunyanyaswa Sana katika hii nchi. Time will tell
Watanganyika wanyanyaswe na wanzanzibari? mbona mtatafuta kila sababu. 😂😂
 
Hakutukwa na mapya sana chini ya utawala wake kuhusu uchumi ila ukatili wa kutisha naamini hautakuwepo.
 
Chini ya CCM, usitarajie jambo lolote jipya au la maana.
 
Tatizo ni kwamba, kusimamia na kuendeleza sera za Magufuli itakuwa ni challenge kwa mama. Mpaka sasa Mawaziri wengi hatujui utendaji wao kwa kuwa ulikuwa umefunikwa na Mwendazake. Kiuhalisia everything was him and about himself.
 
Sasa alipomteua Mwigulu kuwa waziri wa fedha ndio ameharibu kabisa. Nchi hii sasa inarudi kwenye ukoloni mamboleo na umasikini wa kutupwa!
 
Wazanzibar inawezekana wakanufaika na Muungano kiliko kipindi kingine chochote kile. Hii inaweza kupeleka watanganyika kunyanyaswa Sana katika hii nchi. Time will tell
Yaan watu 60m tukanyanyaswe na watu 1.5m ???
Unaota utakuwa
Watakaopitisha Sheria za kunyanyaswa NI wAbunge wetu au?
 
Unamshauri afanye nini mkuu tufunge uzi?
Wabongo tuko vizuri sana kwenye kukosoa na kulalamika. Dunia nzima sidhani kama kuna mtu anatuweza kwa hili..Shida ni kwenye kutoa masuluhisho na mawazo mbadala sasa. Hapo utalia maweee !!!
 
Kama Jiwe pamoja na ubabe wake wote Uchumi umedondoka kwa sasa tusitarajie maajabu
 
Yuko njia sahihi wasiwasi wako tu, timu ya mpira inaweza kucheza kiwango flani chini ya Kocha flani na vilevile kiwango kikabadirika akija kocha mwingine
[emoji3581]
 
Miminaichukia mno ccm lakini Samia atafanya vyema sana kuliko hayati.
 
Hakuna uchumi uliodorola kwa wanaojituma. Fanyeni kazi acheni deals mtafanikiwa

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…