Sioni sababu ya kuilaumu CCM na Mahakama Wakati aliyefungua Kesi ni Mwanachadema


wewe dogo una mambo ya kiboya sana. Sasa hapo kilichokufarahisha ni nini. Wewe ni mmoja kati ya vijana wa hovyooo
 
Kwanini mwanaccm aliyepinga uteuzi SSH kugombea urais bila kufuata utaratibu alifukuzwa uanachama na kutishiwa maisha?

CCM sio chama cha haki, ila kinaneemeka kulaghai watu kuwa kinalinda amani lakini kwa njia za vitisho na kuziba midomo na mawazo jenzi.
 

Unafikiri ni kwa nini ni Mzanzibar ndiye jaamua kuchukua hili jukumu? Tena Mwaka wa uchaguzi... Coincidence!!? Yah right!@
 
CHADEMA sasa hivi inajichuja, pumba zinaelea mchele unabaki chini. Hakuna mwanachadema mwenye akili timamu anayeweza kuishitaki Chadema chini ya uongozi wa mwamba Tundu Antipas Lissu.
#NO REFORMS NO ELECTION


Yan bado hujaconnect dot vzuri.

Je walioishitaki CHADEMA mahakamani ni Wana CCM ??

Kama ni Wana CHADEMA lawama zinaendaje CCM ??

Je mnapo mchagua kuwa mwenyekiti hamkumchuja vizuri mtu wa kumweka kwenye nafasi kubwa kama hiyo ?

Na vipi tunawezaje kuwaamini kuwapeni serikali kama mlishindwa kutuletea viongozi bora wa nafasi nyeti kama hizo ...
 
Kuna baadhi ya masuala hayahitaji uchambuzi wa kina ili kuonesha kwamba una akili, yanahitaji tu uchunguzi wa kawaida kubaini kuwa serikali inahusika moja kwa moja. Uchambuzi wako hauoneshi akili hata kidogo

Wewe mwenye akili ,
Heb ueleze umma wa Wana JF n kivipi mwenyekiti went alomaliza muda wake na bado anakadi Hai ya Chama chenu anaweza kuhusianishwa na CCM ??

NA IKIWA MNASHINDWA KUTEUA VIONGOZI WENYE WERED KTK NAFASI NYETI KAMA HIZO MTAWEZA KWELI KUUNDA SERIKALI ??
 
Unafikiri ni kwa nini ni Mzanzibar ndiye jaamua kuchukua hili jukumu? Tena Mwaka wa uchaguzi... Coincidence!!? Yah right!@


sasa anahusiana vipi na CCM ???

NINYI MNASHINDWA KUCHAGUA WENYEVITI WENYE AKILI mnachagua mapoyoyo. Wakianza kuwaleteeni uzutwa wao mnasingizia CCM.
 
Mkuu nilikuwa nakuona wewe ni mtu wa kusoma alama mapema sana, kumbe nilikuwa najidanganya

Ukiachana na macho ya kuwaona watu, hebu jitahidi uwe na hoja za kutetea Imani yako,

Sio ukiulizwa kuhusu mwenendo wa Chama unaanza kuwaona watu badala ya kuona hoja za kusupport argument za Chama chako.
 
mtu yeyote mwenye akili anajua hii kesi walifungua ccm sio chadema, wale machadema wametumiwa tu kama chambo ila ukifungua veil utakuta limbogamboga limetuama ndani yake bila aibu.
 


Okay CCM wanadeal na matatizo Yao kimya kimya bila kuwapakazia CHADEMA ...

chadema matatizo yenu na kuhukumiana , why mnayapeleka CCM ??
 
mtu yeyote mwenye akili anajua hii kesi walifungua ccm sio chadema, wale machadema wametumiwa tu kama chambo ila ukifungua veil utakuta limbogamboga limetuama ndani yake bila aibu.


Haupo sawa up stairs . Na unajiona genius .

Kushindwa kuteua viongozi wenye weredi na wesioyumbishwa imani zao kwa CHADEMA haiwezi kuwa kosa la CCM. Bali ni fursa.

It's simple logic.
 
No Reform No Election

Hakuna utekelezaji ... ni kauli mbiu sawa tu na ile ya utu na kazi.

Hii ndo bongo. Mtanyeta sio mda.

Wenzenu wanaongea huku wanatenda ...

Ninyi mnaongea huku mnazidi kuongea. ((Hamna utekelezaji)))
 

..Ni kweli aliyefungua kesi ni mwana Chadema.

..lakini wazo hilo nina hakika alilifanyia kazi kwasababu anajua mahakama haitendi haki kwa Chadema.

..mahakama yetu ingekuwa inajiweka mbali na dhuluma dhdi ya Chadema wahusika wasingefungua kesi hiyo.
 

Mimi binafsi siipingi CHADEMA .
ila naona wanazingua sana wanavokua watu wa kubwatuka kulalamika hata bila logic.
 
sasa anahusiana vipi na CCM ???

NINYI MNASHINDWA KUCHAGUA WENYEVITI WENYE AKILI mnachagua mapoyoyo. Wakianza kuwaleteeni uzutwa wao mnasingizia CCM.

Endeleni tu kutetea mipango miovu. Yakiharibika tunaharibikiwa wote. Endelea tu kufanya siasa za kishabiki kama Simba na Yanga.
 

Atleast point yako naweza iokota ....

Yani kiufupi ni sawa na tunavosema kuwa makosa ya mpinzani ndo magori kwako.

ila hatuwezi Sema makosa ya mpinzani ni makosa yako.
 
Endeleni tu kutetea mipango miovu. Yakiharibika tunaharibikiwa wote. Endelea tu kufanya siasa za kishabiki kama Simba na Yanga.

Kiongozi , tamaa yangu kubwa ni kuona tuna amka na tunaanza kufikiri kwa ku reason.

Hizi tabia za kulalamika za CHADEMA hazitaweza kuitoa CCM madarakani hata myaka 100 badae labda watu waanze kufikiri sawasawa . Badala ya kubwatuka.
 
Mmmh wewe ndio yule unajiitaga Tycoon wa fasihi ama ni mwingine?, mbona hizi akili hazifanani na za yule jamaa...ama ndo JF siku hizi watu wanaiba majina ya wengine kutafuta umaarufu tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…