Sioni sababu ya kuilaumu CCM na Mahakama Wakati aliyefungua Kesi ni Mwanachadema

Sioni sababu ya kuilaumu CCM na Mahakama Wakati aliyefungua Kesi ni Mwanachadema

Kwani unadhani Kuna ugumu kwa mke wako kupagawishwa na jamaa jingine na mwisho wa siku kukukana kuwa wewe si mume wake hata kama mmefunga naye ndoa..?

This scenario is relevant to this one...

Hao walikuwa wake wa CHADEMA. Wameolewa na CCM/serikali. Ghafla wamemgeuka na kumkana mume wao CHADEMA...

Wa kulaumiwa hapa na huyu mwanaume anayerubuni na kuchukua wake za watu...!

Hata hivyo, kesi inaendelea. Kitakachofanyika ni huyu mume aliyeporwa mke kwenda na ushahidi kuwa huyu ni mke wangu halali kisheria akiwa na ushahidi wa hati ya kisheria ya ndoa..

Mchezo utaishia hapo...

Nipo kwenye vita na Rashidi, wote tumeoa na tunawatoto.

Rashid katumia mtoto wangu kunishambulia au kamrubuni Mke wangu akanisaliti.
Lipi kosa la Rashid kumtumia Mke au mtoto wangu kushinda vita yake na Mimi?

Kumbuka CCM na Chadema wapo kwenye vita vya Kisiasa.
Kuibiana wanachama ni Jambo la kawaida kwenye vita hiyo.

Ni kama M23 kuwalaghai wanajeshi wa Kongo.

Ambacho sitataka kuona na Sisi tusio na chama ni uonevu na mauaji lakini hiki kinachoendelea ni Makosa ya kawaida ya chadema ambayo CCM wanayatumia
 
Mtibeli, una hakika kuwa Salumu Mwalimu ni Chadema? Au yule amvaye yuko Chaumma wamefanana tu majina?

Vv

Hao wote walikuwa Chadema.
Ni kama wale Askari wa Kongo waliojiunga na M23.

Kwa hiyo Mkuu huoni makosa ambayo chadema wanatakiwa kuyafanyia kazi kabisa?
 
Huyu mwamba mtoa mada nilikuwa namheshimu sana ila leo amenishangaza saaana yaani hajuhi adui anatumia mbinu zote.ata chauma atawalaumu chadema??

Nachojaribu kuwaambia msilalamike, wenzenu wanatumia weakness zenu kwa nini ninyi hamtumii zakwao?

Mkiendelea hivi shughuli itawachachia nawahakikishia.

Ukitaka kumuua nyoka gizani anzia kumulika miguuni. Ninyi mnamulika mbali wakati nyoka wapo miguuni mwenu. Mkiambiwa hamtaki.

Sawa
 
Eleza how does that concern CCM wakati wanaoshitakiana ni Wana CHADEMA.

 how ???
kivipi. ???
Wewe nikikujibu utajinyea..............kwanza kamsikilize Jebra Kambole Wakili wa Chadema, Kama unaweza ku-connect dots utaelewa nani aliyoko nyuma ya haya yote. Fungua bongo utaelewa.
 
Eleza how does that concern CCM wakati wanaoshitakiana ni Wana CHADEMA.

 how ???
kivipi. ???
CHADEMA sasa hivi inajichuja, pumba zinaelea mchele unabaki chini. Hakuna mwanachadema mwenye akili timamu anayeweza kuishitaki Chadema chini ya uongozi wa mwamba Tundu Antipas Lissu.
#NO REFORMS NO ELECTION
 
Hamjambo Wote!

Sipendi watu wanaolaumu wengine Kwa Makosa Yao. Kulaumu wengine kwa Makosa uliyoyafanya ni kukimbia uwajibikaji.

Kwenye Pambano lolote, huwezi mlaumu adui au timu pinzani kwa kutumia watu wako Wasiowaaminifu.

CHADEMA wanachangamoto ya watu Wasiowaaminifu ambao ni rahisi kutumiwa na Maadui zao.

Fikiria Chadema walikuwa wanalalamika CCM inawanunua Watu wao. Badala ya wao kujilaumu kwa kuwa na wanachama ambao hununulika.

Sio kosa kwa CCM kununua Wanachama wengine upande wa upinzani.

Haya SASA CHADEMA yazuiwa kufanya shughuli zake na Mahakama kutokana na Kesi iliyoanzishwa na Mwanachama mwenzao kutokea Zanzibar.

Hivi hiyo inakuingia Akilini kweli?

Hapa hatuwezi walaumu CCM au Mahakama. Mwenye tatizo hapa ni CHADEMA wenyewe.

Chadema inapitia kipindi kigumu ambacho kitachuja makapi na kubakiza wapinzani halisi. Sasa sijajua watabaki wangapi maana numbers matter.

Watu kama Tundu Lisu wapo Wangapi Chadema? Hilo ndio swali.
Maana hao ndio wataweza mikikimikiki.

Soma Pia: Rasmi, Mahakama yapiga marufuku shughuli zote za CHADEMA

Kuliko hawa ambao wananunulika.

Hii pia inamaanisha Chadema kwenye kuchagua viongozi inatakiwa iwe Macho katika kuchagua mashujaa kwelikweli. Vinginevyo watawakatisha wengi tamaa!

Haya! Sisi tupo! Tunatazama.

Robert Heriel
Taikon Master
Dar es salaam
Mkuu nilikuwa nakuona wewe ni mtu wa kusoma alama mapema sana, kumbe nilikuwa najidanganya
 
Kuna baadhi ya masuala hayahitaji uchambuzi wa kina ili kuonesha kwamba una akili, yanahitaji tu uchunguzi wa kawaida kubaini kuwa serikali inahusika moja kwa moja. Uchambuzi wako hauoneshi akili hata kidogo
 
Back
Top Bottom