Sioni umuhimu wa daraja la Aga Khan - Coco beach kwa sasa

Mkuu kipaumbele chetu kwa sasa ni kuwafanya mabalozi wasikae foleni kwa muda mrefu, daraja la jangwani linalotumiwa na walalahoi likifurika wao wanauwezo wa kusubiri hata wiki maji yapungue ndipo wapite hawana haraka kama mabalozi.
We jamaa hebu acha kupotosha watu kwa kifikra zako za kipumbavu. Sisi tunaotumia njia hiyo tunajua adha ya foleni iliyopo. Unaposema hilo daraja ni kwa ajili ya watu wa oysterbay na masaki unakosea sana.

Daraja hilo ni kwa ajili ya kupunguza msongamano katika barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Bagamoyo road kwa watu wanaotoka na kuingia mjini. Barabara hizo zinatumiwa na watu kutoka Kerege, Moga, Mbweni, Boko, Bunju, Tegeta, Ununio, Kunduchi, Mbezi ya Juu na Chini, Mwenge,Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala na Kinondoni. Wote hawa wanaingia mjini kupitia Ally Hassan Mwinyi road via Salender Bridge. Unaweza kuona burden iliyopo hasa nyakati za asubuhi na jioni.

Huwezi kuwa na njia moja ya kuingilia mjini inayoweza ku accomodate watu wote hawa bila kuwa na alternatives. Inavyoonekana huna exposure ya namna miji inavyotakiwa kuwa. Nenda kaone miji ya watu ilivyo. Njia za kuingilia mjini zinaweza kuwa hata 20 tena kwa kutumia njia mbalimbali za usafiri.

Kama vitu huvijui ni vema ukavifanyia utafiti wa kutosha kuliko kuja kuwapotosha watu.
 
Tunakwenda kujenga Flyover baharini
Wakati wananchi hawana maji safi na salama ya kunywa!

Tunapenda mamiradi ya show kuliko mahitaji ya msingi ya watu! . Pathetic
Ndugu yangu ukipingana na serikali hii jitahidi kuwa kipofu na kiziwi hivyo hivyo..ama sivyo utaumia sana..fuatilua taarifa za miradi ya maji ujue..amka ndugu
 
Sasa kama wewe unaishi Ununio utaonaje umuhimu... mkuu

Uende ukaishi

Masaki
Oysterbay
Coco

Ukiishi huko utajua umuhimu
 
Wafanyakazi mtaendelea kusubiria ongozeko la mshahara hadi tumalize kujenga miundombinu kwanza.
 
Huyu baba akilala anaota madaraja na ndege
 
Umuhimu mnao uona hapo ufipa ni wa biashara ya mwenyekiti wenu tu ( Madawa)
Mbona jibu lako haifanani na hoja ya daraja? Siasa itatupeleka shimoni. Maana kila kitu ni siasa tu hata ukitoa hoja ya msingi kwa vile wewe ni upande wa pili badala ya kujibiwa utatupiwa vijembe na kashfa.
Asifikiri wenzenu walioanza multiparty siku nyingi wanaendelea ni kwa sababu wao wanaendana na fact. Siyo tu kila kitu kikitoka upande upande wenu kuwe kibaya au kizuri kwenye ni kizuri kwa sababu mnatawala au mmeshika dola.
Siku za karibuni Uingereza mawaziri 3 wamejiuzulu akiwemo Boris Johnson kutokubaliana na Prime minister lakini ingekuwa kwetu hata Mr. President leo wakisema watu wote watembee uchi mjini nafikiri mawaziri wote watapiga makofi na kushangilia na polisi watahamasisha atakaye katana ni lockup.
Jitahidini kuishi na fact na mfahamu Magufuli siyo Mungu ni binadamu wa kawaida tena ana mapungufu mengi tu na asinge kuwa ma mapungufu asingefukuzwa Kasita Seminari
 
Una ushahidi....weka hapa hatua zichukuliwe.....
Angekuwa anauza kweli si wangepata sababu rahisi ya kumfunga. Hapo walipo kila siku wana tafuta sababu za kuunga unga ili wamfunge hawapati usingizi wako lala Mbowe wakiamka Mbowe.
 
Ndugu Kipande acha kupotosha watu, hao watu wa hizo sehemu ulizozitaja (Kerege, Moga, Mbweni, Boko, Bunju, Tegeta, Ununio, Kunduchi, Mbezi ya Juu na Chini, Mwenge,Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Mwananyamala na Kinondoni) watatumia njia gani kufika kwenye hilo Daraja? Ujue hilo daraja linaanzia Coco beach, let say mimi natoka Kerege au Mbezi beach, kwanza nitakutana na foleni kubwa sana maeneo ya Tegeta na daraja la mlalakua. Watu wote wa sehemu hizo tukitaka kwenda coco beach ili kuja mjini itabidi tupitie njia ya msasani karibu na TANESCO Mikocheni, njia hii ni mpya lakini ni nyembamba sana, haiwezi kuhimili magari yote ya kutoka sehemu hizo ulizozitaja. Pili ukifika maeneo ya Kimweri road kuna foleni kubwa sana zinazosababishwa na Daladala na magari madogo yaendayo Masaki mwisho, Bararabara yote ya Msasani kuanzia mandazi road inafoleni sana nyakati zote. Sasa mtu atafikaje kwenye hilo daraja la Coco beach?

Simply hili Daraja litakua la wakaazi wa kile kinachoitwa MSASANI PENINSULA (MASAKI NA OYSTERBAY) ONLY. Na walengwa wakuu hapa ni Mabalozi, wazungu karibia wote wanaishi huko, Matajir na Viongozi wa serikali walio PORA NYUMBA ZA UMMA.

Suluhisho la foleni Dar liko kwenye sehemu kuu tatu.

1. Kuondoa junction na traffic lights kwenye maungio ya barabara kubwa kuu kama Morroco, Magomeni, Mwenge n.k. Nakujenga interchange kama ya Ubungo.
2. Upanuzi wa bararabara, na zijengwe kisasaa, mfano pale Sarender bridge, Daraja linaweza kutanuliwa pamoja na barabara yote ya Ali Hassan Mwinyi na kuwa na jia 12, njia 3 za kushoto kabisa ziwe za watu wa kinondoni, 6 za katikati za watu wanakwenda moja kwa moja Mwenge, na 3 za kulia za watu wa hiyo Msasani Peninsula.
3 Tuache kuingiza siasa kwenye mambo ya kiutaalamu, Kwa Raisi kuruhusu wafanya biashara ndogo ndogo (Machinga) kufanya biashara kwenye barabara kumeathiri sana barabara zetu. Mfano ukienda Kariakoo na Arusha mjini njia nyingi zinapitika kwa tabu sana kwa sababu hawa wamachinga wanapanga bithaa mpaka barabarani.
 
Ushahidi ni kujaa kwa mateja ufipa
Kwa akili yako ndogo unafikiri wale mateja wanakula real cocaine? Pole cocaine kama cocaine ni expensive wale ni mixture ya petroli sulphuric acid na taka taka kibao.
Hainiingii akilini ununue cocaine kwa mamilioni amlipe mamilioni mtu wa kubeba halafu ulete Tanzania u supply kwa Kikwete tsh 500
 
Kuna umuhimu feasibility study ya hili daraja iwekwe wazi kwa umma ili tujue vigezo gani vilitumika kufanya maamuzi ya kujenga hapo na sio sehemu nyingine
 
Da umeonekana we MTU.Nimekumiss kitambo.
Mkuu nipo siku zote ila kuna wakati huwa nabaki kuwa mtazamaji lkn sio kuwa naogopa, pa kukosoa nakosa ya kushauri nashauri.

Huwezi kujenga daraja la salenda ukaacha kupanua barabara ya Kimara halafu ukasema unapunguza foleni.
 
Kuna barabara nyingi tu za vumbi zinaunganisha mikoa inayotoa mazao kwa wingi. kuziweka lami kungesaidia sana kukuza uchumi wa Taifa
 
Jadili hoja acha kuita wengine wapumbavu.

Hakuna mtu asiyeijua foleni ya Salender, lkn solution sio kujenga daraja la Coco beach.

Panua au jenga daraja la jangwani, panua barabara ya Kimara - Mlandizi, panua barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Old Bagamoyo, panua barabara ya Mwenge-Tegeta-Bunju, bila kupanua hizo barabara zitakazopokea magari yatakayoshuka Coco beach bridge unafanya kazi bure ni sawa na kuhamisha foleni ya Salender kuipeleka Mwenge na Mikocheni.
 
Sio lazima uone umuhimu kwa sasa, ila kwa daraja la Jangwani unalolitetea hapo tuache unafiki. Lile daraja linatosha sana kukidhi mahitaji ya pale katika kuyamudu maji. Ni upumbavu wa mkandarasi aliepewa uboreshaji wa mito ya mji huu. Uliwahi kuona wapi mto mkubwa wa namna ile unaongezwa upana bila ya kuongeza kina cha mto?
 
Hapo ni maeneo ya daraja la jangwani halionekani limezama unalosema linakidhi mahitaji.

 
Mkuu wengine hatupingi miradi bali priorities, unajenga daraja unaacha feeder roads, OK magari yakishuka Coco beach bridge yanaenda wapi, ile barabara ya tanesco mikocheni ambayo hata kupishana magari mawili ni shida sanasana umehamisha foleni ya Salender Bridge kuipeleka Mlalakuwa bridge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…