Sioni 'utupu' wa Gigy Money, mamlaka zimehuhukumu kwa mihemko na kukurupuka

Sioni 'utupu' wa Gigy Money, mamlaka zimehuhukumu kwa mihemko na kukurupuka

Ncha Kali

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2019
Posts
15,335
Reaction score
29,114
Na hii nasema ni ukweli wa dhati kabisa, mnyonge mnyongeni lakini haki yake msimyime.

Kwa binti mnenguaji huyu, lile vazi ni kazi ya sanaa na ubunifu kwa ajili ya jukwaa.

Kwanza ni vazi lililofunika mwili mzima kwa mtindo wa kubana, yaani sio la kuvua bali kumenya kama ngozi vile au ganda la mwili.

Ni wazi BASATA wamekurupuka, au labda kama kuna sababu zaidi ya hilo vazi, pengine wamekuwa wakimuwinda siku nyingi sasa ni kama kaingia kumi na nane!

Lakini pia, hata kama hilo ni kosa kwa mujibu wa taratibu zao bado adhabu ya MIEZI 6 kwa WASAFI TV haielezeki kwa hali ya kawaida. Labda kama nao tumewapania siku nyingi!

Call a spade a spade, BASATA hamjachelewa rejeeni upya hukumu yenu... na nyie ni binadamu hivyo 'mlipitiwa' hamkuona vizuri tutawaelewa.

Hakuna UTUPU pale, au nasema uongo ndugu zangu?
1609918680167.png

1609918503863.png
 
Btw
Kibongo bongo mwanamke akionesha eneo la magoti kuja juu mpaka kwenye kitovu inahesabika ameonesha utupu.

Mahali pengine panaposemwa ni kuonesha utupu ni eneo lote la manyonyo na mabega.

Ninachoshangaa inakuwaje TCRA hawajaufungia wimbo wa Diamond wa Waah maana wanenguaji wanaume wameonesha vifua wazi.

Kwanini 'utupu' ni kwa wanawake pekee?
 
Ni kawaida kuona mwanaume kavua shati kaweka begani na anaendelea na Mishe/safari zake

Lakini kwa mwanamke ni ngumu kidogo

Nirudi kwenye maada,mtoa post anasema Gigy alivaa vazi linalofunika mwili mzima.swali,,,

Ni kwanini kabuni vazi lenye rangi Kama mwili wa binadamu?

NB:napendekeza wasafi ingefungiwa at least two weeks up to one month.na faini ya pesa taslimu

Lakini pia BASATA wangedili na Gigy
 
Back
Top Bottom