Sipaswi kulaumiwa

Sipaswi kulaumiwa

SEHEMU YA 17

Tayari siku mpya iliwasili ndani ya mtaa wa Geza, tunawajua jinsi walivyo watu wa mtaa huu, kabla jua halijachomoza wao tayari walitawanyika kwenye pembe nne za dunia kwenda kujitafutia kile ambacho wamekipanga, kupata ama kukosa hayo waliyachukulia kama majaliwa ya Mungu. Larah alimaliza kumuweka sawa mamaake na yeye mwenyewe, alimsogelea na kumkumbatia kama wafanyavyo siku zote.

"Mwanangu, furaha uliyonayo usoni mwako naomba idumu siku zote, nafurahi sana kuona mafanikio yako huku na mimi nikiwa hai, najivunia uwepo wako maana umeweza kuipigania afya yangu. Mheshimu sana Meddy maana yeye ndie ambae kila siku amekua mstari wa mbele kwetu, nakutakia kila la kheri kwenye kazi zako...Mungu awe mbele yako binti yangu" Mama Larah aliongea hayo kwa sauti iliyosheheni furaha.

"Usijali mama, nakuahidi mimi binti yako nitabaki kua mwema kwako na yeyote yule aliyeshiriki kunishika mkono wakati wa dhiki" Larah na yeye aliahidi huku akimimina mabusu usoni kwa mamaake.

Huyu mama na yeye hajui tu kama mwanawe tayari keshazagamuliwa zaidi ya mara tano, huyo Meddy anayemsemea aheshimiwe bintie tayari kafanya mume. Au inawezekana pia huyo mama Larah anaelewa kinachoendelea kati yao lakini tu anajizima data😄

Mguu mosi mguu pili hatimae alizipata hatua ambazo zilimsogeza hadi nje ya nyumba ambayo walipanga, akiwa hapo alibahatika kuona kundi la watu likiwa limeduwaa mbele yake likimtazama , kundi hilo liliongozwa na wapangaji wenziwe, mwanzo alidhani labda ni kwa namna ambavyo amevaa , alijikagua na kujiridhisha kua hakua na kasoro yoyote katika mpangilio wa mavazi yake licha ya kwamba yalikua ya kisasa zaidi, bado kundi lile liliendelea kumpa hofu maana nyuso zao zilionekana kuwa na hasira huku nyingine zikionekana kutibuliwa, hawakuishia hapo tu kundi lile lilionekana likionyeshana jambo kwenye simu zao za kisasa huku mikono yao ikiwa kwenye midomo yao wakionekana kushaangaa kitu..

Alijipa matumaini ya kua pengine mpango wake na Meddy utakua umeshakamilishwaa, alifurahi kwenye moyo wake licha ya kwamba hofu juu ya zile nyuso ilimrejesha nyuma, aliamua kusogeza hatua zake mbele ili kuwakaribia kwa ukaribu zaidi ila alisita baada ya kuona sura ya Meddy ikichomoza mbele yake tena ikiwa haina nuru ya tabasamu hata kidogo, haraka sana alimsogelea kwa hofu maana kengele ya hatari iligonga kichwani mwake.

"Meddy kuna nini mbona sielewi? Kwani umefanikiwa kufanya lile jambo? Na kama umefanya mbona jamii yangu inaonekana kuwa na nyuso zilizokosa tabasamu dhidi yangu?" aliuliza Larah kwa hofu huku akimkokota Meddy pembeni .

"Larah, usijitoe akili ! Hivi umewaza nini kabla ya kuachia huo upuuzi wako?" Meddy aliuliza hayo kwa sauti ya ukali.

"Upuuzi gani Meddy? Nyoosha maelezo usinivuruge na wewe! Kwani si tuliamua pamoja " Larah aliuliza kwa hofu kubwa maana hakua akijua kosa lake.

"Pamoja na nani ? Usiniigizie Larah, mimi ndio nilikua na wewe pale kitandani? tayari video na picha zako za utupu ukiwa kitandani na Romy zinasambaa kwenye mitandao yote ya kijamii, nadhani umefakiwa kuonyesha uhodari wako kama mwanamke kabla ya kilele chako kufika...." Meddy alifoka kwa hasira.

Taarifa hiyo ilimshtua mno Larah, hakutegemea kamwe kama siku yake ambayo aliikaribisha kwa tabasamu inaenda kuangukia kwenye dimbwi la huzuni, moyo ulimuenda kasi na kumfanya akae chini bila kutaka. Aliwaza mengi kwenye akili yake hadi alihisi kuvurugwa.

"Meddy, kweli mimi naweza kufanya hivyo? Huyo atakua Romy tu ........nakuapia" kwa sauti ya kilio Larah alijitetea.

"Romy eeeh....inawezekana ikawa kweli ni yeye maana hata account zako umeamua kumpa yeye adhihirishe mahaba yenu ? Kwanini usingesubiri tumalize tulichokipanga? Umejidhalilisha mno na umenivunja moyo, tayari unaangukia kwenye sifa mbaya na kutupiwa kila aina ya matu...." kabla Meddy hajamaliza maneno yake alishtukia Larah akimalizia kuanguka chini kama mzigo.

Kundi ambalo lilikuwa pembeni yao liliwasogelea kwa ukaribu zaidi, Meddy hakujisumbua kumnyanyua zaidi ya kuondoka bila kutoa msaada wowote , watu ambao walimzunguka walibaki wakichukua picha na video ili wapate kuendeleza story ambayo ilibamba mitandaoni. Wale wasiokua na simu basi waliona ule ulikua ni muda sahihi wa kumtupia Larah matusi na laana kibao.

Kwenye wabaya siku zote na mwema huwa hakosekanani, sote tunamkumbuka shogaake aliyeitwa Niffa, huyu ndie ambae kwa muda ule alikua ni msaada kwake, Niffa alibeba jukumu la kumkokota Larah na kumuingiza chumbani kwao, huko alifanikiwa kumkuta mama Larah akiwa kwenye majonzi mazito, hii ilidhihirisha wazi kuwa masikio yake yaliweza kunasa kelele na maneno ambayo yalikua yakiendelea kutupwa huko nje, alimhurumia bintie huku akimshukuru Niffa kwa wema wake.

**********

Kiti chake kwa siku hiyo alikichukia maana hakua na hamu hata ya kukaa, hasira zilimvaa hadi uso wake uliiva na kuzidisha wekundu kwenye pua yake ndefu, Ngumi zisizo na idadi aliamua kuzibamiza kwenye ukuta wa ofisi yake hali iliyopelekea mikono yake kuanza kuvuja damu, alilia na kujilaumu katika nafsi yake. Kichwani mwake yalizunguka maswali ambayo hakua na uwezo wa kuyajibu maana hakuwa na kumbukumbu ya tukio ambalo linaendelea kutapakaa kwenye mitandao, anaikumbuka vyema siku ambayo aliingia na Larah moja ya hotel kubwa Geza ila hakuwa na kumbukumbu ya yeye kushiriki tendo wala kurikodi tukio lolote, nani alifanya? kwanini video iachiwe siku ile?

"Kwanini Larah! kumbe wewe ni nyoka eeeh? Sikuwahi kufikiria kamwe kama unaweza kufanya upuuzi kama huu! Sawa mimi na wewe hatukua sawa lakini ndio ulipize namna hii tena kuelekea siku muhimu ambayo Geza nzima inatutazama? Nitakutafuta na lazima utalipia kwa hili , nataka nijue nani yupo nyuma yako kwenye hili? " Romy alibwata kwa hasira machozi yakiwa usoni mwake.

Hakika ungemuona basi moyo wa huruma ungekuingia, Romy alijiweka kipembeni na kuinamisha uso wake kwenye mapaja yake akilia kwa hasira, alijuta kumfahamu Larah kwenye maisha yake, alijilaumu kwanini alimuamini kupitiliza . Hakua na habari ya mlango wa ofisi yake kugongwa mfululizo, mamaake aliita kila jina ila hakuna alichoambulia zaidi ya ukimya ambao ulimtia mashaka, uamuzi aliochukua ni kuwaita walinzi ambao walianza kuuvunja mlango.

Ule usemi wa uchungu wa mwana aujuae mzazi ulionekana kwa Madam Ziya, hakujali kabisa mazingira machafu ya ofisi ambayo alikumbana nayo , yeye alimsogelea kijana wake ambae bado alijikunyata huku mikono yake ikiwa imerowana damu, alimkumbatia na kunyanyua pale alipokaa huku akimtaka waondoke eneo lile kuepuka mapaparazi ambao walijaa kutafuta taarifa za undani wa tukio ambalo lilijitokeza .

******

"DEAL DONE" hayo yalikua ni maandishi mekundu makubwa yaliyoonekana kwenye ukuta mkubwa mweupe ambao ulipatikana ndani ya chumba ambacho kilikua na vijana wawili wa kiume. Maandishi hayo yalionekana kuchorwa muda mfupi uliopita maana rangi yake ilionekana kuchuruzika na kufanya michirizi.

"Nadhani mpango huu umekamilika, kinachofuata sasa ni kuendelea kuharibu imani zao kwa kuwaendesha vile ambavyo mimi nataka, nitahakikisha hakuna amani kati yao na jina la kampuni yao linakufa kama ambavyo alikufa baba yangu" maneno yenye hisia zito yalitolewa kinywani kwa sauti iliyojaa hasira huku akimgeukia mwenziwe.

Licha ya sura yake kuonyesha hasira lakini mavazi yake yalionekana wazi kabisa kuwa ni mtu aliyejiweza kiuchumi , muonekano wake kwa wakati ule ulionekana kubadilika kabisa! Naam huyu ndie Meddy 🙄 laiti mngemuona basi mngesema hakua yule Meddy wa Larah 😀 wala Meddy ambae alionekana na Wanageza akiranda ovyo mitaani ila ukweli hauwezi kujificha siku zote. Itawashangaza! ndio yeye kabisa .
 
*SEHEMU YA 16 *

Maswali ya Larah yalimfanya Mr.Romy ageuke bila ya kutaka , alimsogelea Larah ambae safari hii mwili wake hakua ameuziba hata kwa mikono, mara tu alipomfikia alinyanyua taulo kubwa ambalo lilikua chini na kumfunga Larah mwilini mwake.

Baada ya hapo alishindwa kudhibiti hisia zake na kujikuta akimkumbatia zaidi ya dakika mbili, Larah alijitahidi kujitoa kwenye kumbatio hilo ila ilishindikana maana alishikiliwa kisawasawa.

"Larah...." ilikua ni sauti nzito ya Mr.Romy ambayo ilikwenda kusisimua mwili wa bibie, hakua na ujasiri wa kuitika kwani hisia za utamu na uchungu zilimuandama na kujikuta akiubana kimya.

"Larah...." aliita kwa mara nyingine tena kwa upole baada ya kuona kimya kimezidi, Mr.rommy ni kama alihisi kitu hivyo alijitoa kwenye kumbatio na kuitazama sura ya Larah ikiwa imerowana machozi. Alisikitika mno.

Viganja vyake alivitumia kuyafuta machozi ya binti ambae alikua mbele yake, alimhurumia na kujikuta akimkumbatia kwa mara nyingine tena , ni kama vile alimchochomoa maana Larah alijikuta akilia kwa sauti japo sio kubwa sana. Hisia za mapenzi juu ya boss wake zilimuandama Larah ila alijikuta akimchukia kutokana na unyama ambao alimfanyia.

"Larah....umelia sana, naomba nipe nafasi nijieleze kwako, umekua ukinichukia mno ila mimi......" kabla hajamaliza alichotaka kusema walisikia mlio wa viatu ukikaribia usawa wa chumba walichokua huku jina la Larah likiitwa kwa sauti , haraka sana Mr.Romy alijificha nyuma ya mlango ili atakaeingia asimuone na yeye apate kuchomoka kwa urahisi.

Ni kitendo cha sekunde chache tu Madam Siti kuwa ndani ya chumba na Mr.Romy kupata upenyo wa kutokea nje , kuna kitu Madam Siti alikua anakitafuta maana alizunguka pembe zote za chumba ila hakuna alichokipata, hakika aliisikilizia harufu ya Mr.Romy mwanaume aliyebeba hisia zake.

"Larah....upo sawa? Halafu mbona uso wako umejaa machozi ! Nini shida? Madam Siti aliuliza huku akiusoma vyema uso wa Larah ambae alikua kama aliyepigwa shoti maana hakuelewa nini cha kufanya.

"Weeeh Larah......" aliitwa tena ila wakati huu alishikwa hadi na bega ili hisia zake zirudi.

Ingawa alishtuka ila hakua na muda wa kupoteza, haraka alivuta nguo zake na kuvaaa bila kumsemesha chochote aliyekua mbele yake. Baada ya kumaliza alisogea hadi kwenye dressing na kuvuta pochi yake ili atokomee nje ila alijikuta akizuiliwa kwa kushikwa mkono.

"Unasemaje? Larah aliuliza kwa ukali swali ambalo lilimshangaza Madam Siti, ni kama masikio yake hayakutegemea kusikia kile ambacho kiliulizwa.

"Weeh Larah! Umejisahau unazungumza na nani? Halafu mbona kama ulikua na mtu humu ndani, yupo wapi? Madam Siti alihoji mikono yake bado ikiwa imemshikilia Larah.

Larah ni kama vile alikua akipotezewa muda wake, hakua na muda wa kuendelea kubaki pale kabisa , alijua tu kama angeendelea kuwepo basi ingepelekea kuzuka kwa mjadala mrefu , alijitoa kwa nguvu mikononi mwa madam siti na kujiandaa kuondoka.

"Ukijaribu kuuvuka huo mlango utajua mimi ni nani! Hii kazi utaiona chungu" maneno hayo kutoka kwa madam Siti yalimfanya Larah abaki akiwa kashikilia kitasa cha mlango.

"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu, hivyo sijali wala nini! Sikuogopi..." Larah alizungumza hivyo tu na kuamua kutokomea nje huku akimuacha madam Siti mdomo wazi asiamini kile alichokisia.

Hakua na muda wa kupoteza, haraka na yeye alikwenda sehemu ambayo walikua wamepaki gari lao, aliwakuta watu wote kwenye gari wakimsibiri yeye tu. Alishangaa kumuona Mr.Romy ndani ya gari lake akiwa katulizana na dereva wake, alimtazama kwa jicho kali huku akijiapia kwenye nafsi yake kua ni lazima awe wake.

*********

Zilikua zimebaki siku mbili tu kueleke kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Larah alikua na furaha mno maana alitegemea kua kile alichokipanga kinakwenda kukamilika. Hata upande wa afya ya mamaake pia mambo yalikua sio mabaya maana tayari alitoka hospitali na alianza kufanya mambo mengi bila usaidizi wa binti yake.

Mr.Romy yeye bado hakua na amani wala furaha , alijitahidi kuweka ukaribu na Larah ila hakuna alichoambulia zaidi ya maumivu ya kupokea maneno mabaya ambayo yalizidi kumuumiza, hakuvunjika moyo na alijipa imani ya kua siku moja atapata tu nafasi kwenye moyo wa binti huyo na kumueleza kile ambacho kinamtatiza kwenye moyo wake.

Madam Siti na yeye alijitahidi kujipendekeza kwa boss wake ila hakuna alichokipata zaidi ya dharau na onyo kali, hata Madam Ziya ambae ni mama wa Romy na yeye hakua na msaada maana alichoka kumhubiria kijana wake juu ya mahusiano yake na Siti . Chuki kati ya Madam Ziya na Larah ilizidi kuongezeka ila hilo halikumfanya Larah atetereke maana alijua kinachomfanya aendelee kuwa pale.

Muda wote kwenye nafsi yake alikua akitabasamu, aliona kua ule wakati wa yeye kuwa na furaha unakaribia kwa kishindo, alitamani saa zikimbie ili bomu alilolitega liripuke na aliowakusudia waumie kama alivyoumia yeye, siku hiyo aliondoka kazini mapema na kuelekea sehemu ambayo Meddy alipanga.

Walipokeana kwa mabusu motomoto huku kila mmoja akiwa na nyuso ya tabasamu, walipohakikisha kutosheka na kinywaji kisichokata kiu walijisogeza hadi juu ya kitanda na kuanza kutazamana kwa macho ya matamanio.

"Meddy , hakika wewe ni mwalimu bora kwangu! Sio tu kwenye uwanja wa mahaba lakini pia kwenye uwanja wa maisha ambao napaswa kuweka huruma na hisia pembeni ili nipambanie kesho yangu na kile ambacho naamini kitairejesha furaha yangu iliyopotea. Nina furaha kubwa mno leo wacha niimalizie kwako" Larah alizungumza hayo huku akianza kupunguza nguo mwilini mwake.

Meddy alijipigia kofi za ushindi moyoni mwake, hahaaa😁 embe tayari limeiva mbele yake , kisu anacho mkononi , anaanzaje kuacha kulimenya ? siku hiyo mmiliki wa uwanja alikua ni Larah licha ya kuwa yeye alikua mualikwa, alihakikisha hampi Meddy nafasi ya kufurukuta , alimkamata vilivyo kijana wa watu aliyebaki kuweweseka kutokana na huba zito alililopewa. Ujuzi wote ambao aliupata kutoka kwenye mitandao ya kijamiii siku hiyo aliufanyia kazi mwilini kwa Meddy, bwana mdogo alibaki akiugulia maumivu tu ya raha huku akishindwa hata kutikisa ukucha.

Baada ya saa nzima kukatika hatimae mechi iliyokosa washabiki iliisha, Meddy hiyo siku alimtazama Larah bila kummaliza, alichopewa kwa siku hiyo hakutegemea kabisa kama atafanyiwa na Larah binti ambae hapo mwanzo waliishi kama marafiki walioheshimiana na kuoneana aibu.

"Meddy ......nilikuahidi kua nitakufanya ufurahi, nilikuapia kua nitakua kando yako siku zote , sijui huko nyuma uliyopitia na wala sitaki kujua ila naamini huu ni wakati bora kwetu, tuufurahie ushindi wetu ambao siku za karibuni utakwenda kuwaliza wale waliotuumiza" Larah alizungumza hayo huku akivuta pochi yake ambayo ilikua na flash.

Moyo wa Meddy uliripuka kwa furaha ambayo alishindwa kuizuia na kujikuta akimkumbatia Larah kwa nguvu, ni kweli siku ile alikua na furaha ambayo inaonekana aliisubiri sana. Mvua ya mabusu aliishusha kwenye mwili wa mwanamke ambae alikua akitabasamu mbele yake.

Mipango endelevu ilizidi kutengenezwa ili kukamilisha lengo lao, kama ni ng'ombe basi tayari ilibaki sehemu ya mkia tu kuliwa, na aliyetakiwa kukamilisha ni Meddy mwenyewe mwenye mipango yake........itaendeleaaaaaa
 
SEHEMU YA 18

Licha ya sura yake kuonyesha hasira lakini mavazi yake yalionekana wazi kabisa kuwa ni mtu aliyejiweza kiuchumi , muonekano wake kwa wakati ule ulionekana kubadilika kabisa! Naam huyu ndie Meddy 🙄 laiti mngemuona basi mngesema hakua yule Meddy wa Larah 😀 wala Meddy ambae alionekana na Wanageza akiranda ovyo mitaani ila ukweli hauwezi kujificha siku zote. Itawashangaza! ndio yeye kabisa Meddy mzee wa mipango.

Baada ya kula kiapo ambacho alikua na utayari wa kukitumikia basi aliamua kusogea kwenye meza ya kioo ambayo ilisheheni pombe na vileo mbalimbali, alitoa sigara moja kwenye pakti na kuiwasha huku akianza kuvuta kwa kasi mno kiasi cha kutoa moshi mwingi, alimwita mwenziwe kwa ishara ili wajumuike pamoja , walianza kunywa na kufungua mziki mkubwa ambao uliwavutia kucheza pia. Wataachaje kufurahi ikiwa kile walichokipanga kimetimia.

"Larah....utanisamehe kwenye hili, vigezo vyako ndio vimechangia utumike kwenye mpango huu" Meddy alijisemea kwenye nafsi yake huku akiendelea kulisakata rumba.

********
Masaa matano baadae Larah alionekana bado kajikunyata mapajani kwa mamaake , hakua na shauku ya kutoka nje hata kidogo kutokana na kilichotokea. Kwa vile Niffa tayari aliondoka basi mama na bintie walibaki kuusindikiza ukimya wa huzuni uliotawala chumba chao. Uvumilivu ulimshinda mama mtu na kuanza kuzipapasa nywele nyingi za bintie huku akimwita.

"Larah....unaweza kunieleza kwa kina kinachoendea au utabaki kutiririsha machozi ? Mama Larah aliuliza ila zilipita sekunde bila kujibiwa chochote.

"Kama umefanya kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au watu basi ni rahisi kupata tena kibali cha umma, Ingawa hio haitawafanya wakuamini tena kama zamani..... kwa sababu tayari umevunja kuta za uaminifu walizojenga juu yako, lakini tayari utakua umeiweka nafsi yako kwenye chumba cha uhuru" Aliongeza Mama Larah maneno ambayo kiasi fulani yalimfanya binti yake ajiinue na kukaa kitako.

Larah alimtazama mama yake usoni kwa dakika zisipungua tano , aliona wazi namna ambavyo kuna kila sababu ya kumueleza, alijipa moyo kua kivyovyote mamaake asingemtupa hata angekua mchafu kiasi gani. Hakukua na haja ya kuendelea kumficha maana kila kitu kulikua wazi licha ya kwamba hakuona. Alianza kumsimulia kila kitu kumhusu Rommy na jinsi alivyotaka kumsaidia kipindi ambacho alilazwa, hakuna tukio ambalo aliacha licha ya kwamba yalimuumiza mno , hata namna alivyoutoa mwili wake kwa Meddy ili alipize kisasi pia alisema. Kiufupi ni kwamba Larah hakuacha hata nukta kwenye usimuliaji wake.

"Mmmh Larah! Mbona umefanya mambo yote hayo bila kunishirikisha? Unadhani utaupata tena uaminifu wa Meddy? Au ndio...."

"Mama....sikua na chaguo jengine zaidi ya Meddy, yeye alionyesha wazi kuchukia ukaribu wangu na Romy, na kama hiyo haitoshi nilimuona kuwa ana uwezo na yeye ni mjanja mjanja, sikujua kama hili lingetokea kabla ya mpango wetu kukamilika " alijieleza Larah.

" Ulichokosea hapo ni kuishi na roho ya kisasi binti yangu, hivi umewaza kuwa kisasi chako kitaumiza wangapi? Haya Meddy huyo tayari hupo nae? Hadhi na utu wako pia vimepotea! Unadhani ni rahisi kujirejesha kua yule Larah aliyekua akiheshimika na kuwa mfano wa kila mtu hapa Geza? Umeyaharibu maisha yako mwanangu " Mama Larah aliongea kwa sauti fulani iliyoonyesha uchungu na hasira.

"Mama....Nitafanya kila niwezalo ili nimkomeshe aliyehusika na upumbavu huu, sitadhalilika peke yangu kwenye hili kabisa" alijitapa Larah huku akijiinua.

"Usijizidishie mambo mwanangu, nguvu za kumuadhibu unazitolea wapi? Ni bora uliache lipite maana mwisho wa siku binadamu watasahau na maisha mengine yataendelea , kwani ilikuwaje huo uchafu ukasambaa mitandaoni"

"Mama, kwenye kulipa kisasi naomba uniache kabisa! sikuwahi kufikiria kutumia simu za kisasa kwa sababu ya mambo kama haya, ila mwisho wa siku ilinilazimu maana biashara itangazwayo ndio itokayo! Huyu ni Romy tu aliyefanya hivi hakuna mtu mwengine, maana ni yeye pekee aliyekua anamiliki video na picha zote " sauti ya Larah alipozungumza hayo ilidhihirisha hasira akizokua nazo.

Mazungumzo kati ya mama na mwana yaliendelea, Larah aliushikilia msimamo wake wa kumkomesha aliyemzunguka licha ya kupokea ushauri mzuri kutoka kwa mamaake. Mwisho wa siku aliamua kufuta machozi yake na kuvaa nguo za kawaida na kuanza kuandaa chakula cha mchana, kwa vile kila kitu kilikua ndani basi wala hakusumbuka kwenda nje.

********

Kikao cha mtu tatu kilifanyika kwenye ukumbi mkubwa uliopambwa na kila aina ya samani, waliokaa kwenye ukumbi huo walionekana kuzama kwenye mjadala mzito wa kuinusuru kampuni yao isiangamie . Rommy ndie ambae sura yake ilionekana kukosa raha kuliko wote ambao walikua sebuleni hapo.

"Nisikilize kijana wangu, nadhani huu sio wakati wa kulaumiwa mtu, kama ni makosa uliyafanya wewe mwenyewe kwa kumuamini mwanamke ambae katokea hukoo mitaani, kila kitu kimeharibika na wale wote ambao walikua wana matangazo yao tayari wamesitisha" Madam Ziya ambae ni mama Romy alizungumza huku na yeye akionekana wazi kuchukizwa.

"Ni kweli Mr.Romy, nadhani tunapaswa kuchukua hatua za haraka kulisafisha jina lako na taasisi yetu ambayo imepakwa matope, nitahakikisha nakua mstari wa mbele kwenye hili kwa sababu mimi ndie niliyemkaribisha Larah na kumuaminisha kila mmoja kwamba yeye ni mzuri na anaweza! Sote tulishuhudia namna ambavyo tuliingiza mapato mengi kupitia yeye...." alisisita Madam Siti akiwatazama waajiri wake watasema nini.

Majadiliano yalikuwa mengi kiasi ambacho hakukua na muafaka mzuri kati yao, Romy kwenye kikao hicho hakuonekana kuwa sawa hata kidogo , kichwani mwake yeye hakuwaza kabisa kuhusu taasisi lakini aliiwazia hadhi yake, aliinuka na kuelekea kwenye maegesho ya gari huku kila mmoja akishangazwa maana kikao kilikua hakijamaliza.

"Mmmh! Siti, huu ni muda sahihi wa kua karibu na Romy ili umteke hisia zake, ukimsafishia jina tu basi naamini utaushinda moyo wake ambao umeweka ugumu siku nyingi kwako. Wewe ndie mkwe ninaekutambua" Madam Ziya alitamba baada ya Romy kuondoka.

Kwa uso wa aibu Siti alionekana kulikubali ombi hilo, yeye mwenyewe aliitaka nafasi hiyo muda mrefu ila hakuwahi kuipata, alijiapiza kumfurahisha kwa namna yoyote ile ili aingizwe kwenye moyo wa Romy kijana tajiri na mtanashati.

Baada ya Siti kuaga, Madam Ziya alionekana akizunguka ukumbini kufikiria jambo, kwenye akili yake aliwaza namna ya kumsaidia kijana wake ili taasisi iliyojengwa muda mrefu isianguke . Hata yeye alijisemea kuwa huo ulikua ni wakati wake wa kujionyesha kuwa yeye ni mama bora ambae anaweza kumpigania mtoto wake kwenye hali ngumu .

******
Giza nene ndilo ambalo lilitawala anga la mji wa Geza, ukubwa wa wingu hilo lililotanda ulikwenda kuwaogopesha wakaazi wa eneo hilo, kwa vile tayari ilikua ni majira ya saa kumi na moja za jioni basi kila mmoja alitaka awahi kujificha nyumbani kwake kabla ya mvua nzito kunyesha, ni muda huo ndio ambao bibie Larah alijiandaa kutoka.

"Mama, usiwe na wasiwasi kabisa kuhusu mimi.Ninachokwenda kukitafuta ni heshima na imani iliyopotezwa dhidi yangu" Larah alimbusu mamaake ambae alibaki tu kumtazama kwa kiulizo.

Larah hakutaka kabisa ngonjera za mamaake, alijua kua kuendelea kumsikiliza mamaake kungeweza kubadilisha maamuzi yake. Kwake kubaki ndani ilikua ni kama kujizidishia matatizo, hakutishwa na giza lilillokua nje bali aliongozwa na moyo wake ambao ulitaka pambano . Kwake yeye lile giza alilichukulia kama ni fursa maana watu wote walikimbilia majumbani mwao. Naam ukisikia vita ya panzi neema kwa kunguru ndio hii..itaendeleaaaaaa
 
*SEHEMU YA 16 *

Maswali ya Larah yalimfanya Mr.Romy ageuke bila ya kutaka , alimsogelea Larah ambae safari hii mwili wake hakua ameuziba hata kwa mikono, mara tu alipomfikia alinyanyua taulo kubwa ambalo lilikua chini na kumfunga Larah mwilini mwake.

Baada ya hapo alishindwa kudhibiti hisia zake na kujikuta akimkumbatia zaidi ya dakika mbili, Larah alijitahidi kujitoa kwenye kumbatio hilo ila ilishindikana maana alishikiliwa kisawasawa.

"Larah...." ilikua ni sauti nzito ya Mr.Romy ambayo ilikwenda kusisimua mwili wa bibie, hakua na ujasiri wa kuitika kwani hisia za utamu na uchungu zilimuandama na kujikuta akiubana kimya.

"Larah...." aliita kwa mara nyingine tena kwa upole baada ya kuona kimya kimezidi, Mr.rommy ni kama alihisi kitu hivyo alijitoa kwenye kumbatio na kuitazama sura ya Larah ikiwa imerowana machozi. Alisikitika mno.

Viganja vyake alivitumia kuyafuta machozi ya binti ambae alikua mbele yake, alimhurumia na kujikuta akimkumbatia kwa mara nyingine tena , ni kama vile alimchochomoa maana Larah alijikuta akilia kwa sauti japo sio kubwa sana. Hisia za mapenzi juu ya boss wake zilimuandama Larah ila alijikuta akimchukia kutokana na unyama ambao alimfanyia.

"Larah....umelia sana, naomba nipe nafasi nijieleze kwako, umekua ukinichukia mno ila mimi......" kabla hajamaliza alichotaka kusema walisikia mlio wa viatu ukikaribia usawa wa chumba walichokua huku jina la Larah likiitwa kwa sauti , haraka sana Mr.Romy alijificha nyuma ya mlango ili atakaeingia asimuone na yeye apate kuchomoka kwa urahisi.

Ni kitendo cha sekunde chache tu Madam Siti kuwa ndani ya chumba na Mr.Romy kupata upenyo wa kutokea nje , kuna kitu Madam Siti alikua anakitafuta maana alizunguka pembe zote za chumba ila hakuna alichokipata, hakika aliisikilizia harufu ya Mr.Romy mwanaume aliyebeba hisia zake.

"Larah....upo sawa? Halafu mbona uso wako umejaa machozi ! Nini shida? Madam Siti aliuliza huku akiusoma vyema uso wa Larah ambae alikua kama aliyepigwa shoti maana hakuelewa nini cha kufanya.

"Weeeh Larah......" aliitwa tena ila wakati huu alishikwa hadi na bega ili hisia zake zirudi.

Ingawa alishtuka ila hakua na muda wa kupoteza, haraka alivuta nguo zake na kuvaaa bila kumsemesha chochote aliyekua mbele yake. Baada ya kumaliza alisogea hadi kwenye dressing na kuvuta pochi yake ili atokomee nje ila alijikuta akizuiliwa kwa kushikwa mkono.

"Unasemaje? Larah aliuliza kwa ukali swali ambalo lilimshangaza Madam Siti, ni kama masikio yake hayakutegemea kusikia kile ambacho kiliulizwa.

"Weeh Larah! Umejisahau unazungumza na nani? Halafu mbona kama ulikua na mtu humu ndani, yupo wapi? Madam Siti alihoji mikono yake bado ikiwa imemshikilia Larah.

Larah ni kama vile alikua akipotezewa muda wake, hakua na muda wa kuendelea kubaki pale kabisa , alijua tu kama angeendelea kuwepo basi ingepelekea kuzuka kwa mjadala mrefu , alijitoa kwa nguvu mikononi mwa madam siti na kujiandaa kuondoka.

"Ukijaribu kuuvuka huo mlango utajua mimi ni nani! Hii kazi utaiona chungu" maneno hayo kutoka kwa madam Siti yalimfanya Larah abaki akiwa kashikilia kitasa cha mlango.

"Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu, hivyo sijali wala nini! Sikuogopi..." Larah alizungumza hivyo tu na kuamua kutokomea nje huku akimuacha madam Siti mdomo wazi asiamini kile alichokisia.

Hakua na muda wa kupoteza, haraka na yeye alikwenda sehemu ambayo walikua wamepaki gari lao, aliwakuta watu wote kwenye gari wakimsibiri yeye tu. Alishangaa kumuona Mr.Romy ndani ya gari lake akiwa katulizana na dereva wake, alimtazama kwa jicho kali huku akijiapia kwenye nafsi yake kua ni lazima awe wake.

*********

Zilikua zimebaki siku mbili tu kueleke kilele cha Siku ya Wanawake Duniani, Larah alikua na furaha mno maana alitegemea kua kile alichokipanga kinakwenda kukamilika. Hata upande wa afya ya mamaake pia mambo yalikua sio mabaya maana tayari alitoka hospitali na alianza kufanya mambo mengi bila usaidizi wa binti yake.

Mr.Romy yeye bado hakua na amani wala furaha , alijitahidi kuweka ukaribu na Larah ila hakuna alichoambulia zaidi ya maumivu ya kupokea maneno mabaya ambayo yalizidi kumuumiza, hakuvunjika moyo na alijipa imani ya kua siku moja atapata tu nafasi kwenye moyo wa binti huyo na kumueleza kile ambacho kinamtatiza kwenye moyo wake.

Madam Siti na yeye alijitahidi kujipendekeza kwa boss wake ila hakuna alichokipata zaidi ya dharau na onyo kali, hata Madam Ziya ambae ni mama wa Romy na yeye hakua na msaada maana alichoka kumhubiria kijana wake juu ya mahusiano yake na Siti . Chuki kati ya Madam Ziya na Larah ilizidi kuongezeka ila hilo halikumfanya Larah atetereke maana alijua kinachomfanya aendelee kuwa pale.

Muda wote kwenye nafsi yake alikua akitabasamu, aliona kua ule wakati wa yeye kuwa na furaha unakaribia kwa kishindo, alitamani saa zikimbie ili bomu alilolitega liripuke na aliowakusudia waumie kama alivyoumia yeye, siku hiyo aliondoka kazini mapema na kuelekea sehemu ambayo Meddy alipanga.

Walipokeana kwa mabusu motomoto huku kila mmoja akiwa na nyuso ya tabasamu, walipohakikisha kutosheka na kinywaji kisichokata kiu walijisogeza hadi juu ya kitanda na kuanza kutazamana kwa macho ya matamanio.

"Meddy , hakika wewe ni mwalimu bora kwangu! Sio tu kwenye uwanja wa mahaba lakini pia kwenye uwanja wa maisha ambao napaswa kuweka huruma na hisia pembeni ili nipambanie kesho yangu na kile ambacho naamini kitairejesha furaha yangu iliyopotea. Nina furaha kubwa mno leo wacha niimalizie kwako" Larah alizungumza hayo huku akianza kupunguza nguo mwilini mwake.

Meddy alijipigia kofi za ushindi moyoni mwake, hahaaa😁 embe tayari limeiva mbele yake , kisu anacho mkononi , anaanzaje kuacha kulimenya ? siku hiyo mmiliki wa uwanja alikua ni Larah licha ya kuwa yeye alikua mualikwa, alihakikisha hampi Meddy nafasi ya kufurukuta , alimkamata vilivyo kijana wa watu aliyebaki kuweweseka kutokana na huba zito alililopewa. Ujuzi wote ambao aliupata kutoka kwenye mitandao ya kijamiii siku hiyo aliufanyia kazi mwilini kwa Meddy, bwana mdogo alibaki akiugulia maumivu tu ya raha huku akishindwa hata kutikisa ukucha.

Baada ya saa nzima kukatika hatimae mechi iliyokosa washabiki iliisha, Meddy hiyo siku alimtazama Larah bila kummaliza, alichopewa kwa siku hiyo hakutegemea kabisa kama atafanyiwa na Larah binti ambae hapo mwanzo waliishi kama marafiki walioheshimiana na kuoneana aibu.

"Meddy ......nilikuahidi kua nitakufanya ufurahi, nilikuapia kua nitakua kando yako siku zote , sijui huko nyuma uliyopitia na wala sitaki kujua ila naamini huu ni wakati bora kwetu, tuufurahie ushindi wetu ambao siku za karibuni utakwenda kuwaliza wale waliotuumiza" Larah alizungumza hayo huku akivuta pochi yake ambayo ilikua na flash.

Moyo wa Meddy uliripuka kwa furaha ambayo alishindwa kuizuia na kujikuta akimkumbatia Larah kwa nguvu, ni kweli siku ile alikua na furaha ambayo inaonekana aliisubiri sana. Mvua ya mabusu aliishusha kwenye mwili wa mwanamke ambae alikua akitabasamu mbele yake.

Mipango endelevu ilizidi kutengenezwa ili kukamilisha lengo lao, kama ni ng'ombe basi tayari ilibaki sehemu ya mkia tu kuliwa, na aliyetakiwa kukamilisha ni Meddy mwenyewe mwenye mipango yake........itaendeleaaaaaa
Hii nayo umerudia, weka kuanzia sehemu ya 19 maans tumeishia ya 18
 
SEHEMU YA 19
Akiwa zake juu ya kitanda kwenye chumba chake cha uswahilini ghafla alisikia mlango wa chumba ukigongwa, alijiinua kiuvivu na kwenda kuufungua. Hakushtuka wala hakujali kwa kile ambacho alikiona ila ndio kwanza alikirudia kitanda chake na kujitupa kama mzigo. Larah aliyekua pembeni yake alibaki kumtazama huku asijue aanzie wapi kuzungumza, kumsogelea alitaka ila uoga ndio ulimzuwia.

"Utabaki umesimama hadi saa ngapi?" Sauti nzito kutoka kinywani kwa Meddy ilivunja ukimya.

"Sa...sam...samahani Meddy..." Larah alijitutumua kusema kwa sauti ya kusitasita iliyosindikizwa na uoga.

"Hahaaaa unachekesha...muda huu ndio umekua hujui kuzungumza? Larah wewe sio mtoto tena...sema kilichokuleta kabla sijakubadilikia" Meddy alifoka kwa ukali huku akiinuka na kumsogelea Larah kwa ukaribu zaidi.

Hofu na uoga vilimuandama Larah huku akisahau hata ule ujasiri ambao aliubeba alipotoka kwao, hakujua mbele ya Meddy angejitetea vipi! Alitamani nguvu za ajabu ziingie mwilini mwake ili aweze kushawishi na kuaminika tena .

"Larah....hemu niambie umewezaje kubadili mpango wetu? Meddy alimkandamiza Larah swali zito ambalo liliibua machozi yake.

"Najua itakua ngumu kueleweka ila ukweli ni kwamba sihusiki na chochote" Larah alijieleza licha ya kwamba bado hofu ilimuandama hii ni kutokana na kusogelewa kwa ukaribu zaidi na Meddy.

Kilichofata hapo yalikua ni mazungumzo kati yao, Larah alijitahidi kumueleza Meddy kuwa hahusiki kabisa na uvujaji wa picha na video zake chafu, ingawa Meddy aliujua ukweli ila alibaki kumkandamiza Larah ili abaki kwenye utumwa wake. Mwisho wa mazungumzo alimsamehe ila ilikua kwa sharti.

"Meddy... sharti gani tena?" Aliuliza Larah kwa upole.

" Tuendelee alipoishia......kama yeye kafanya kwa ajili ya kukukomoa basi nataka na yeye tumkomoe" Meddy alisema hayo akimtazama Larah.

"Sijakupata bado, una maana gani? Larah aliuliza kwa shauku maana na yeye akili yake ilimtuma kumkomoa Romy.

"Larah, nina uhakika Romy atakutafuta , na sababu kubwa ni kwamba hadhi yake na taasisi yao imeanguka tofauti na vile ambavyo alitegemea. Larah tumia ushawishi wako akuamini kua kile kitendo hukufanya wewe na umueleze tukio lote huku lawama ukimtupia yeye, mfanye awe chini yako mkubalie na uanze mahusiano rasmi , baada ya hapo tutatengeneza tukio ambalo tukifanikiwa kulicheza kwa usahihi basi utakua umelipiza kisasi na hatokaa ainuke kamwe" Meddy alizungumza hayo kwa sauti ya chini mno huku mikono yake ikianza kutalii sehemu mbalimbali za mwili wa bibie .

Larah alionekana kuzubaa huku akionekana kushangazwa na mpango huo, Meddy hakujisumbua kumuelewesha ila ndio kwanza aliendelea kutembeza mikono yake sehemu nyeti za bibie Larah, uvumilivu wa kushindana na hisia zao uliwashinda na kujikuta wote kwa pamoja wakizama kwenye ulimwengu wa huba.

Mvua kubwa iliyosindikizwa na radi ndio ambayo iliusindikiza mchezo ule kwa jioni ile , Larah alijiachia akiamini kua ndio njia rahisi ambayo itamfanya apokee msamaha haraka na atimize malengo yake ya kulipiza kisasi. Akilini mwake alijijua kua hakua na kosa na wala hakuwahi kufikiria kuvujisha picha za namna hiyo. Meddy na yeye moyoni mwake aliufurahia ujio wa Larah , hiyo siku aliifurahia mno maana aliamini atamtumia Larah atakavyo ili kukamilisha mpango wake ambao aliupanga muda mrefu.

*****
Romy aliamua kuzimalizia hasira zake kwa kujimiminia pombe tumboni mwake, siku hiyo aliamua kupoteza mawazo kwa style hiyo, aliamini kufanya hivyo kungeweza kuweka sawa akili yake ambayo ilivurugwa. Kila alipokua akinyanyua glass basi hakuacha kuzitazama picha za Larah kwenye simu yake, na alipozitia machoni mwale basi alizisindikiza kwa matusi na maneno ya kashfa.

Wengi ambao walikua pembeni yake walimtazama kwa masikitiko kutokana na kile ambacho kilitokea kwenye mitandaoya kijamii, wapo ambao waliamua kumpiga picha kwa makusudi lengo ikiwa ni kuendelea pale ambapo aliyeanza alifikia, siku zote palipo na wabaya basi mwema na yeye hakosekanani, licha ya tabia zake mbaya aliyokua nayo ila nafsi yake ilijikuta ikikosa amani baada ya kumshuhudia Romy akidhalilika, alimhurumia mno na hapohapo aliitoa simu yake na kuanza kupiga.

"Larah, njoo haraka Paradise Bar" hayo yalikua ni maongezi ya yule binti mara tu baada ya simu yake kupokelewa.

Hakusubiri hata majibu ya upande wa pili tayari alitoweka hewani, moyoni mwake alionekana kuwa na donge na hasira za waziwazi, licha ya kwamba alimsogelea kwa ukaribu Romy ila alijitahidi asionekanwe nae, alizidi kumtazama na kumsoma baadhi ya mambo ambayo alikua akiyafanya na maneno aliyotamka, hii ilimfanya hata yeye agundue kitu.

Baada ya kuona dakika nyingi zinakatika na Larah hajichomozi aliamua kumfuata hukohuko kwao, akiwa kwenye geti la ile bar alimuona Larah akiwa anakuja mithili ya mtu aliyechanganyikiwa, alimvutia pembeni kama kawaida yake na kuanza kumtazama bila kumwambia chochote.

"Niffa....sasa ndio nini kusumbuana hivi!! Halafu nakuja hapa unabaki kunitazama tu! Unajua nimemuacha Meddy kwenye hali gani? " Larah alianza kulalamika.

" Mpuuzi wewe....!! yaani hapa natafuta sehemu ya kukushika , nikutikise, nikutoboe halafu nikiamua kukuingiza maneno basi nipafunike ili yasikutoke.." Niffa alijibu huku akiwa bado anamtazama Larah ambae alibaki kaduwaa.

Akiwa bado kazubaa alishtukia akivutwa tena na kuingizwa ndani ya bar ile hadi sehemu ambayo Romy alikuwepo, Larah alijikuta anakasirika baada ya kumuona Romy meza ya nne kutoka pale ambapo wao walikaa, muonekano ambao alimuona nao ulimtilisha huruma ila kiupande mwengine alijikuta ni mshindi maana kile ndicho ambacho alikitamani ndio kimetokea, alikiachia kicheko kikubwa ila hakikudumu baada ya kutandikwa kofi zito la kichwa.

"Nimekupiga ili huo ubongo wako ushtuke na ufanye kazi vizuri na hii itakua endelevu pale ambapo nitakuona unaenda kinyume na vile ambavyo nataka" Niffa alisema maneno hayo baada ya kuona aliyempiga alikua akimtazama kwa jicho la hasira.

"Niffa iwe ni mwisho sasa!! Kwanini unanifanyia mambo ya ajabu? Wewe ndie ambae ulinileta hapa na kufanya nionane na huyu mtu na mwisho wa siku akafanya kile ambacho kimeshusha hadhi na thamani yangu" Larah aliongea kwa hasira na kuwafanya wale wa karibu yao wawatazame isipokua Romy tu ambae kwa wakati huo hakuweza hata kuunyanyua uso wake kutokana na mzigo wa pombe uliopo kichwani mwake.

"Larah!! kama ni thamani basi umeishusha wewe mwenyewe na sio Romy, ufinyu wako wa fikra na kukumbatia watu usiowatambua ndio umekufikisha huko " Niffa na yeye alipayuka na kufanya kila mtu amsikilize yeye.

Watu wa pale walikua wakimtazama sana Larah kutokana na kile ambacho kilitokea kwenye mitandao ya kijamii, Niffa na yeye alimlaumu mno Larah huku akimtaka aamke kwenye usingizi mzito ambao alilazwa. Kiupande wa Larah yeye aliendelea kulaumu huku akilalamika kukatishwa starehe zake kwa mambo ya kipumbavu.

"Larah... huyu Romy nitaondoka nae ila nakuhakikishia kua ipo siku utamfuata ukiwa tayari umechelewa" Niffa alizungumza hayo huku akisogea usawa ambao Romy alikuwepo.

Ingawa alipata tabu ila alijitahidi kumkokota na kuelekea usawa wa vyumba ambavyo vilipatikana kwenye Bar ile. Larah yeye alibaki akiwa kwenye mshangao baada ya kuona kile ambacho rafiki yake anakifanya , moyo wake ulimuuma maana kuna upande ulikua una chembe za upendo ila hakuzipa nafasi zaidi ya kuweke mbele kisasi chake. Macho ya watu ambao walikua wakimtazama pia yalimfanya ajisikie vibaya na kutoka zake nje kwa hasira kuelekea kwao .

Giza ambalo alikutana nalo nje lilimfanya angalau ajisikie amani kwa maana macho ya watu yangemfanya azidi kujisikia vibaya, hakuwahi kuongelewa kwa sifa yoyote mbaya Geza ile hivyo tukio hilo lilimuathiri vibaya. Kichwani mwake pia maneno ya Niffa yalijirejea kila muda na kumfanya azidi kuchanganyikiwa. Aliamua kuchukua usafiri wa haraka ili amuwahi mamaake ambae kamuacha muda mrefu......Itaendeleaaaaaa
 
SEHEMU YA 20
Huko ndani ya chumba Niffa kibarua kilimkuta, alitukanwa na kutapikiwa ovyo na Romy. Kuna muda alijuta hata kuingilia yasiyomuhusu ila aliishangaa jinsi nafsi yake ilivyokua ikimuuma kutokana na mateso aliyokua akiyashuhudia kwa kijana yule. Licha ya fujo na uchafu wote aliofanyiwa basi hakuudhika wala kukata tamaa, alifanikiwa kumtoa nguo, kumsafisha na kumlaza vyema kitandani.

"Oooh!! Masikini Mr.Romy, najua hili tukio limekuumiza sana na ndio maana umefikia hatua hii. Siamini kabisa kile ambacho wanakiamini wao licha ya kwamba sura sio roho ....... ila moyo wangu unakataa kabisa kama hili jambo umelitenda wewe!! Nakuahidi kua nitakua upande wako, ni moyo wangu tu unanisukuma na sio kitu kingine kabisa" Niffa alijisemea huku akimtazama kwa huruma Romy aliyelala.

Kwa vile usiku ndio kwanza ulikua unaelekea kua mkubwa aliamua kwenda kujitafutia mteja wa karibu ili aingize kile ambacho alikitoa , siku hiyo hakutaka mteja wa usiku mzima maana alitamani arudi mapema ili azungumze machache na mgeni wake ambae alilala fofofo.

*****
Madam Siti na yeye alimpigia Meddy na kupanga wakutane sehemu ambayo siku zote wanakutana, siku hiyo Meddy alionekena kufurahi mno maana muda wote meno yake yalikua nje. Mara tu baada ya Meddy kufika alipokua Madam Siti basi alimzawadia busu zito ambalo lilipokelewa kwa tabasamu licha ya kwamba halikutoka moyoni.

"Meddy ...nadhani ulichokitaka kimetokea, tuusitishe huu mchezo na tuondoke kabisa kwenye huu mji kabla Romy hajasanuka"

"Siti kipenzi, hili goma ndio kwanza limetoa mdundo , yaani hata muziki haujachanganya bado . Yale maumivu ambayo nataka wapitie hata bado hayajafikia thumni yake , sijapata chochote zaidi tu ya kuchafua jina lao unadhani naondoka kirahisi? Meddy alizungumza hayo huku akivuta vizuri kiti chake na kujisogeza karibu zaidi na Siti.

"Ila mwisho wake nauona sio mzuri , tumeshawaingiza hata wale wasio na hatia hemu achana na kisasi Meddy mbona kama tatizo ni maisha mazuri mbona nimekupatia?

"Siti , nadhani unanijua vyema zaidi ya mtu yoyote yule Geza hii. Nimehangaika sana huko nyuma na wala sikua na mtu wa kunishika mkono sababu ikiwa ni hawa watu , Siti ....... najua kuna wengine hawahusiki ila na wao wapo kwenye mpango wangu, unaumia najua ila hatuna budi kuvumilia ili maumivu yetu mwisho wa siku tuwakabidhi wao" kwa upole Meddy aliyasema hayo huku akimshika mikono kipenzi chake.

Hapa ndio tunajua kuwa kumbe Meddy na Madam Siti ni wapenzi wa muda mrefu, hapo walibembelezana na kupeana moyo huku wakipanga mikakati madhubuti ya kuiangamiza PERFECT ADVERTISING AGENCY iliyokua chini ya Mr.Romy, walidhamiria kuiangusha kabisa huku wakiwa na mpango wa kuiba kiasi chote cha fedha .

Wakiwa kwenye mazungumzo hayo bila kujua basi Niffa aliweza kumuona Meddy akiwa na muonekano wa kitofauti. Ilimshangaza na kumtia mashaka kwa maana yule wa pale sio Meddy aliyezowea kumuona mtaani kwao, aliyafikicha macho yake na kuyatoa nje kwa ukaribu zaidi ila alikumbana na sura ileile , naaam huyo ndie Meddy halisi. Hapohapo alijikuta akipanga njia za kumtoroka bwana aliyeambatana nae kwenye Lodge ile ili afuatilie jambo lake.

Bwana wake hakua na shida , alimpa ruhusa ya kwenda chooni huku akimuelekeza sehemu ambayo angemkuta baada ya kurudi. Niffa hakulaza damu hapohapo alijisogeza kwa umakini hadi sehemu ambayo Meddy na Siti walikaa, ilikua ni meza ya pili na karibu mno kiasi ambacho hakukua na ugumu wa kusikiliza mazungumzo yao, masikio aliyategesha ili kunasa vyema mazungumzo yao.

Mipango ambayo aliisikia ikisukwa juu ya Mr.Romy ilimfanya azidishe huruma kwa mtu huyo. Lakini pia alijikuta akimhurumia shosti wake Larah kwa namna ambavyo anatumiwa bila ya yeye mwenyewe kujitambua. Alijua ni ngumu kiasi gani kuwaelewesha watu uchafu wa watu wale , hivyo alichomoa simu yake na kuitegeshea kwa kuanza kupiga picha na kurikodi maongezi yao. Naam kazi kwa siku hiyo ilikua ni hiyo hata yule mteja wake hakumjali tena na alikua yupo radhi kumpoteza.

********

Mwanga wa jua uliofanikiwa kupenya vyema kwenye dirisha ndio ambao ulimtoa Romy usingizini, kichwa chake alikihisi kizito pale ambapo alijaribu kukinyanyua. Aliyapeleka macho yake kila pembe na kugundua ugeni wa mazingira aliyopo, maswali mengi yalianza kukisumbua kichwa chake ambacho kilizidi kumuuma, ilimshangaza zaidi pale alipofunua shuka na kujikuta mtupu kama alivyozaliwa.

Licha ya maumivu aliyokua nayo ila hakutaka kabisa kuendelea kuwa pale, ugumu wa tatizo ambalo lilimpelekea kua hapo ulimjia tena kwenye kichwa chake hasa pale alipojikuta mtupu. Alijitahidi kujinyanyua na kuanza kupiga hatua za uchovu ila hakufika popote maana alitaka kuanguka na aliwahi kujishikiza na kitanda, akiwa hapo akikusanya nguvu za kupiga hatua nyingine alishtukia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na binti mrembo ambae sura yake haikua ngeni machoni mwake , haraka alivuta shuka na kujistiri mwili wake.

"Weweee.....umefata nini hapa? Mnataka nini kwenye maisha yangu ? Tokaaa!!!" Ni kama vile Romy alichanganikiwa maana aliuliza maswali mfululizo tena kwa hasira.

Aliyemuuliza hakua na muda wa kumjibu zaidi alimsogelea kwa ukaribu na kumsaidia kukaa kitandani huku akimfunika shuka vizuri , alimtazama kwa yale macho ya huruma ila aliyetazamwa yeye macho yake yalijaa hasira.

"Naitwa Niffa, nipo hapa kwa lengo la kukusaidia tu na sio kingine" Niffa alijieleza kwa ufupi.

"Unisaidie au unizidishie matatizo? wewe ulinileta humu eeeh? Sihitaji mtu yoyote kwa sasa naomba nibaki peke yangu!!" Alisisitiza Romy.

Niffa hakujibu chochote zaidi alinyanyuka kuelekea mlangoni ambapo mhudumu alifika, alipokea breakfast na mfuko mdogo ambao ulikua na nembo ya ZURI FASHION .

Kwa vile alitaka waelewane na zile chuki kuziweka kando Niffa alianza kumsimulia jinsi ambavyo alimkuta usiku wa jana na kumsaidia hadi kulala hapo, licha ya kwamba alijieleza vyema ila bado hakuweza kuuteka uaminifu wa Romy dhidi yake.

"Mr.Romy, naomba uoshe mwili kidogo , unywe na hii supu ili tuingie kwenye mazungumzo mazito na muhimu sana. Nitarudi hapa baada ya dakika 20" Niffa alizungumza hayo na kutoka nje akimuacha Romy akiwa kaduwaa.

**********

Hekaheka za asubuhi pia zilimkumba Larah, kama kawaida yake hadi kufikia saa mbili tayari alimaliza kazi zote na kubaki pembeni ya mamaake tu akimtazama kwa masikitiko.

"Larah....mbona unanitazama hivyo binti yangu? " Mama Larah aliuliza huku akijiinua na kukaa kitako, tayari afya yake ilitengamaa na kuleta matumaini makubwa.

"Mama..naifikiria sana kesho yangu, sijui Mungu kanipangia nini ila naiona jinsi ilivyokua nzito..." kwa sauti iliyokata tamaa Larah alizungumza huku macho yake yakiwa usoni kwa mamaake.

"Mwanangu, Mungu alikua na maana yake ya kutuwekea pazia zito kwenye hizi nyakati tunazopitia. Hakika kama angetupa uwezo wa kutambua yalio mbele basi tungekua ni wenye tamaa au tuliokosa subra. Huu ni mtihani kama mitihani mingine, mtafute Meddy akupe kazi nyingine achana na ile taasisi Larah! Ubaya haulipwi kwa ubaya binti yangu" kwa upole na unyenyekevu mama Larah alijitahidi kumueleza bintie.

Kuna muda Larah alitamani kuufuata ushauri wa mamaake ila alipomkumbuka Meddy na ahadi alizompatia basi alijikuta akirudi nyuma, hata pale ilipomjia sura ya boss wake Rommy alijikuta roho ya kulipiza kisasi ikimvaa, nafsi yake ilijaa kisasi na ahadi zake kwa Meddy. Alitaka ajisafishe kwa kipenzi chake ili amkomoe Romy ambae ana uhakika kua anampenda.

"Mama, natoka kidogo nitarudi baadae......" kauli hiyo ilimtoka Larah na bila kusubiri majibu alianza kubadili mavazi yake , mamaake aliyekua pembeni hakua na usemi tena zaidi ya kumtazama tu....itaendeleaaaaaa
 
SEHEMU YA 21

Zile dakika ambazo aliahidi kukaa nje kumsubiri mtu wake zilipepea kama upepo, alimuongezea na tano za ziada maana alijua ubinadamu ulivyo. Kwa mwendo wake wa madaha alianza kujiinua na kuelekea usawa wa chumba , akiwa njiani alijiapiza kivyovyote amueleze Mr.Romy kile ambacho alikigundua usiku wa jana yake.

Mikono yake milaini aliitumia kugonga mlango ambao ulikua mbele yake, dakika mbili zilikata akiwa kwenye zoezi hilo ila hakuna majibu zaidi ya ukimya , aliusukuma mlango ambao haukuleta ubishi kufunguka, naam alikaribishwa na na uleule ukimya ambao ulimkumba awali, alisogea hadi mlango wa bafuni ila hakusikia hata zile sauti za kumwagika maji, aliita kwa jina ila pia hakukua na majibu yoyote na hata alipojaribu kuufungua mlango basi alikuta kweupee! bila ya shaka hakukuwepo na dalili za uwepo wa mtu .

Wasiwasi ulimuandama, alianza tena kukagua mazingira ya chumba na kuona ule mfuko ambao ulikua na nguo ukiwa chini tena hauna kitu, hata ile breakfast ambayo aliileta basi pia ilikua imeliwa yote. Alifurahi kimoyomoyo na kuahidi kumtafuta ili atimize lengo lake .
**********
PERFECT ADVERTISING AGENCY ilizungukwa na wanahabari wengi wakiwa na lengo la kutambua zaidi kile ambacho kimeachiwa kwenye mitandao ya kijamii, walinzi walijitahidi kuwazuia wasiingie ndani ya jengo lile ila haikua rahisi maana wanahabari walionekana kupania jambo hilo , imepita siku nzima hawajapata ufanunuzi wa tukio hilo wanaachaje kung'ang'ana?

Mr.Romy ambae alikua juu ofisini kwake alibaki kuchungulia kwenye dirisha akishuhudia vurugu lile, alishusha pumzi nzito huku akionekana kufikiria jambo fulani, akiwa kwenye mawazo alirejesha umakini wake kwenye mlango wa ofisi yake unaofunguliwa , macho yake yaliishia kumtazama Madam Siti ambae alisimama mbele yake akionekana kutaka kusema kitu .

"Mr.Romy.... nadhani hakuna haja tena ya kuendelea kujificha . Ni wakati wa kuinuka na kuanza kurekebisha pale tulipoharibu " Madam Siti aliamua kuanzisha mazungumzo.

"Una maana gani Siti " Mr.Romy aliuliza kwa upole.

"Wewe bado ni kijana Mr.Romy, kuna mengi hapo mbele yatatokea yenye kuumiza zaidi ya haya, adui sio mtu wa kukimbiwa kabisa msogelee na umkumbatie ili ajue kua hila zake hazijakuteteresha kamwe. Ipo tiba moja ya kila kitu kinachotokea au kuendelea kwenye maisha. Tiba hiyo ni muda. Kila kitu kinapita, hakuna chochote kinachodumu milele, hata wewe mwenyewe.......Mr.Romy twende tukaongee na wanahabari" maneno ya Madam Siti yalimshawishi Romy na kumfanya aingiwe na nguvu mpya , kwa hiari yake alijikuta akimshika mkono na kutoka nae nje ya ofisi hiyo.

Kiu ya wanahabari iliongezeka mara tu baada ya kushuhudia Mr.Romy na Madam Siti wakiwakaribia mbele yao, waliongeza ukaribu zaidi huku wakiweka sawa vipaza sauti na camera zao.

Kabla Mr.Romy hajazungumza chochote aliiona sura ambayo hakutegemea kabisa kama ingekua pale kwa muda ule, sio mwengine huyo alikua ni Larah ambae alipendeza mno , mavazi yake na mwendo wake uliosindikizwa na mlio wa viatu ndio ambao uliwafanya hata wanahabari wamuelekee yeye, naam camera na vipaza sauti vilihama kwao na kuhamia upande wa Larah

Larah kabla ya kuzungumza alimtazama boss wake ambae alibaki mdomo wazi huku hasira za wazi zikionekana juu yake, alimtabasamia huku akijongea usawa ambao alikuwepo na kufanya wakaribiane kwa ukaribu zaidi, kwa vile wanahabari ni nyuki basi walifuata mzinga ili walambe asali.

"Unapaswa kutulia hii ngoma niachie mimi" Larah alimnong'oneza Mr.Romy ambae alibaki kumtazama Madam Siti kama mshauri wake ila aliishia kupewa alama ya utulivu.

"Ndugu wanahabari na nyote ambao mnanisikiliza , sote hapa tunatakiwa kutambua kuwa baadhi ya watu ni kama mishumaa inayojichoma ili kuwaangazia wengine lakini mishumaa hiohio licha ya kutoa mwanga basi huunguza na kuleta athari kwa wengine. Nilipokelewa kwenye taasisi hii kwa uaminifu na imani kubwa, nilijituma na kuisogeza pale ambapo malengo yao yalikuwa, nimesikitika na kuumia mno kuona nachafuliwa mimi na taasisi inayonilea , walioucheza huu mchezo wanajijua wenyewe na wala sitohangaika kuwatafuta ila nawasikitikia kwa maana hii tunaichukulia kama ni changamoto na siku zote changamoto ndizo ambazo huibua fursa...." Larah alisita kidogo baada ya kuongea hayo, ni kama alikua akitaka kuziteka hisia za wasikilizaji wake.

"Ndio, ...... nitahakikisha taasisi hii inasimama zaidi ya hapo mwanzo, nguvu na juhudi zangu zote nitaziwekeza bila kujali kilichotokea" Larah aliendelea huku wengi ambao walikua wakimsikiliza kupitiaa vyombo ya habari wakiweka umakini.

"Nikiwa na akili zangu timamu na binti ninaejielewa siwezi kabisa kufanya uchafu ule, sijui ni njia gani na ufundi gani ulitumika kunichafua ila nakiri tena kwenu hatujawahi kufanya hivyo kabisa mimi na Mr.Romy licha ya kwamba ni wapenzi ambao penzi letu ni changa na lilikua la siri mno, ni ngumu kuaminika najua..... maana sura zetu zilionekana wazi na hata account ambazo zimetumika ni za kwangu" alimaliza Larah na kuwa kimya kwa muda, ni kama alivizia wanahabari wamuulize chochote ila aliwateka maana wote walibaki kimya wasijue waulize nini.

Mr.Romy alishangazwa na namna ambavyo Larah alijieleza, sio yeye tu hata wale ambao walikua mbele yao pia walizama kwenye mshangao. Wanahabari walihamia kwa Mr.Romy, huko walipekenyua kuhusu ukaribu na mahusiano ya Madam Siti na Mr.Rommy, kwenye hilo Mr.Romy aliruka pima mia na kujibu kua uhusiano wao ulikua ni kwenye kazi tu na hapo hapo alimsogelea kwa ukaribu zaidi Larah na kumshika mkono kwa lengo la kuondoka mbele ya wanahabari. Madam Siti alibaki kucheka ovyo ila moyoni mwake alimlaani na kumtukana vilivyo Mr.Romy na Larah huku akiahidi kumkomesha kwa kumdhalilisha.

Waandishi walimsogelea Madam Siti na kumhoji baadhi ya mambo kuhusiana na sakata lile, hata yeye alionekana kuitetea taasisi hiyo huku akiwataka wawekezaji na wafanyabiashara wote kufanya nao kazi kama ilivyokua zamani, mwisho Madam Siti aliomba radhi kwa niaba ya taasisi yake na wale ambao wanawategemea.

Naam mahojiano yaliishia hivyo hakuna mabadiliko yoyote ndani ya taasisi hiyo na watu wote walikaribishwa kutangaza biashara zao, licha ya kwamba bado maswali ya picha na video chafu yaligonga vichwa chao ila waliamua kufunika kombe maana hakuna aliyetaka kuufunguka ukweli.

Larah na Mr.Romy walikua kwenye mazungumzo juu ya kile ambacho kimetokea, Larah aliona kua ile ndio nafasi pekee ambayo anaweza kukamilisha lengo ambalo yeye kalipanga, alijiinua pale alipokaa na kumsogelea Mr.Romy kwenye kiti chake kwa ukaribu zaidi. Aliyapeleka macho yake na mikono yake hadi kwenye tai iliyopo shingoni mwa Mr.Romy, aliishika na kuanza kuichezea kwa madaha.

"Muda ukipotea hauwezi tena kurudishwa hata kama utafanikiwa kufanya jambo ambalo muda wake umepita , jua ya kwamba utalazimika kutumia muda wa leo au kesho kulifanya na sio wa jana ambao uliuchezea , Mr.Romy....najua kua wewe ndie dereva wa mchezo huu nikiwa kama msafiri wako basi naomba ukubaliane na masharti yangu ili niendelee kua na faida kwako" Larah alichombeza kwa sauti ya upole ambayo masikioni kwa Mr.Romy ilikua ni kama makelele.

"Unamaana gani Larah!! Hivi hujamaliza tu michezo yako? Nani kakutuma? " kwa ukali kidogo Mr.Romy aliuliza.

Larah aliamua kujitetea kutokana na tuhuma ambayo anapewa, alianza kumkumbushia juu ya tukio ambalo lilitokea hotelini siku ambayo alimchukua mikononi kwa Niffa , kuhusiana na picha ama video pia lawama alimtupia yeye , hakuacha kumueleza juu ya mtu ambae alimfuata akidai kuachia picha na video endapo atakataa kufanya kazi kwenye taasisi hiyo, hakuishia hapo tu alimpa sharti la kua ampe kila ambacho atataka na kamwe asije akathubutu kwenda kinyume maana atamchafua kama ambavyo alichafuliwa yeye. Maelezo yote hayo Larah aliyatoa huku machozi yakimtoka na sura ya huzuni iliyojaa hasira ikionekana.

Kijasho kilimtoka Mr.Romy, maelezo ya Larah yalizidi kumchanganya na kumnyinya nguvu kabisa. Alijihisi ni mwenye hatia baada ya kugundua kua kachezewa mchezo ambao hata haukuwa kwenye mpango wake, alimpenda mno Larah na alitamani awe wake ila sio kwa njia hii ambayo ilitumika. Alizidi kujilaumu pale Larah alipomueleza kua yeye ndie mwanaume wa kwanza kumuingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi. Alimtazama Larah aliyekua mbele yake ambae uso wake uliokosa hatia ulikua kwenye huzuni na hasira za wazi.

"Larah..."aliita Mr.Romy kwa upole huku zile hasira zote akiziweka pembeni, Larah mwenyewe alibaki kumtazama kwa jicho la sitaki nataka.
"Naomba nikwambie kitu....." Itaendeleaaaaaa.
 
Back
Top Bottom